Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Kwa nini alilaaniwa Canaan ambaye hakujua kosa na si aliyemchungulia?
Just simple hasa kama wewe ni mzazi..uchungu wa mwana aujuaye mzazi na hata maumivu ya shida zozote za watoto huwa yanamtesa mzazi zaidi.Hii ni personal observation sie wazazi tunaelewa
Wana ndio huwa wanabeba dhambi za wazazi wao hasa akina baba ko tuepuke kudondosha machozi ya watu matokeo utayaona kwa wanao hapo ndipo utaisoma namba
 
Hebu nami nitupie machache ktk huu mjadala, kadri ambavyo nimerudia rudia tena na tena kusoma hii incident ya Noah najiwa na maswali mengi baadhi ni kama hivi!
1.Je ni muda gani ulipita tangu family hii itoke ktk safina mpaka tukio hili lilipofanyika.?
2.Canaan alikua mtoto Wa NNE Wa Shem , je huyu mtoto alikuaje kuaje mpaka Noah hakuingiwa na huruma yoyote kumpa laana nzito vile?
3. Je Ham alifuata nini ktk Tent la baba yake mpaka akamkuta ktk hali ile ilihali alikua ni MTU mzima mwenye mke na watoto na makazi yake?
6.Na kama ilikua bahati mbaya kwanini akaenda kuwasimulia nduguze tukio hilo kama vile it was funny ?
7.Yawezekana hakuwa na nia mbaya(ovu) alikwenda kwa baba yake may be kuzungumza but akamkuta amelewa akakereka na hilo hivyo kwa hasira akawambie nduguze "Ah baba mlevi kweli nilienda kuongea nae nmekuta yuko uchi kalala huko ndani" ndipo nduguze wakaenda kumfunika, lkn waliwezaje kumfunika pasipo na wao kumwona utupu ???.
Mwisho kabisa Noah alitambuaje yote haya wakati alikua hana ufahamu kwa pombe ?? Na kwanini hakutoa hata muda kutaka kujua jambo hilo kabla hajatoa hukumu ?
Ukihoji sana utaambiwa ni kufuru mambo ya Mungu hayahojiki amini hivyo hivyo,sasa inageuka kuwa imani ya mashaka na dilema
 
Mkuu zitto junior ili uweze kuelewa ni kwanini Nuhu alimlaani Caanan na siyo Ham aliyetenda kosa, kwanza unatakiwa ulielewa na kuliamini NENO la MUNGU. Ili ulielewe NENO la MUNGU, kwanza lazima uliamini. Binadamu hatuwezi kumwelewa MUNGU, lakini tunaweza kulielewa NENO lake ambalo ametupa ili litusaidie katika maisha ya sasa na yale yajayo.

Tatizo linakuja pale ambapo watu walio wengi hawataki kuielewa Biblia wala kuiamini, wengi wanaona kile kilichoandikwa kwenye Biblia ni kama hadithi tu, ni kama porojo tu ambazo hazina maana. Ukweli ni kwamba, Biblia ni zaidi ya hadithi, ni zaidi ya Historia, na ni zaidi ya Unabii ambao umekuwa ukitimia kila siku. Kwa kulitambua hili, mimi nitakupa majibu ya Kibiblia ni kwanini Nuhu alimlaani Caanani badala ya Ham. Majibu yote yapo ndani ya Biblia na nje ya Biblia huwezi kupata majibu.

Iko hivi; zamani zile Wazazi hasa baba walikuwa wanatoa baraka au laana kwa kizazi cha watoto wao na siyo kwa mtu mmoja peke yake. Kama ni baraka, baba alikuwa anatoa baraka hizi kwa watoto wake wa kiume na vizazi vyao vyote vinavyofuata kwa sababu walikuwa wanaamini kuwa kizazi hakiishii kwa watoto, bali kinaendelea na kuendelea. Pia huu ndiyo ulikuwa utaratibu waliojifunza kutoka kwa BWANA MUNGU, pale alipotoa laana ya kwanza kwa mwanadamu na nyoka;


"nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino". MWANZO 3:15







Hapo juu utaona hiyo laana siyo kwa Eva na nyoka peke yao, bali ni kwa uzao wao wote utakaotokea duniani. Hii inaonekana kuwa wazee wale wa kale walijifunza pia kutoa laana au baraka kwa kizazi na kizazi. Hebu tuone baraka ya Isaka kwa Yakobo.

"Mataifa na wakutumikie, na makabila wakusujudie. Uwe bwana wa ndugu zako, na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakaye kulaani, alaaniwe na atakayekubariki, abarikiwe". MWANZO 27:29







Hapa pia utaona Yakobo anabarikiwa na baba yake, tena siyo baraka kwa ajili yake tu katika maisha yake yeye kama Yakobo, bali ni kwa ajili yake na uzao wake wote utakaofuatia baada yake. Hivi ndivyo ilivyokuwa, hivi ndivyo wanadamu walijifunza kutoa baraka kwa wana wao au laana. Pia unaweza ukasoma kitabu hicho cha MWANZO sura ya 49, na utaona jinsi ambavyo na yeye Yakobo alivyotoa baraka kwa watoto wake 12.

Tukirudi upande wa BWANA MUNGU, pia tutaona jinsi alivyombariki mzee Ibrahimu, hakumbariki yeye tu kwa wakati ule, bali alimbariki yeye na uzao wake wote utakaofuatia baadaye.


"Nami nitakufanya wewe kuwa Taifa kubwa na kukubariki, na kulikuza jina lako nawe uwe baraka. Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa". MWANZO 12:2-3








Mpaka hapa tutakuwa tumeona jinsi baraka na laana zilivyokuwa zinatolewa na inaonekana wazi kabisa namna ya kutoa baraka au laana, Wanadamu wa kale akiwemo mzee Nuhu walijifunza kutoka kwa MUNGU. Tukumbuke kuwa Nuhu alikuwa ni Nabii wa MUNGU, na aliongea na MUNGU mara nyingi tu katika njozi na maono. Hivyo basi Hamu alipokosea kwa kumwangalia baba yake akiwa uchi na kumcheka, alilaaniwa Caanani ambaye alikuwa ni uzao wa Hamu, yaani kizazi chote cha Hamu kikawa kimelaaniwa.

Huo ndiyo ulikuwa utaratibu wa kutoa laana au baraka, tena ni utaratibu ambao ulikuwa na baraka zote toka kwa MUNGU. Caanan hakumcheka Nuhu, lakini alilaaniwa sababu yeye alikuwa ni uzao wa Hamu, Caanan alikuwa anabeba damu ya Hamu ndani yake na alipaswa kulaaniwa. Pia tukumbuke jinsi MUNGU alivyosema katika zile Amri kumi;


".........nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu". KUTOKA 20:5-6








Nuhu hakukosea kumlaani Caanan, nasema hakukosea sababu Nuhu alifuata utaratibu uliokuwepo. Utaratibu ambao hata BWANA MUNGU aliutumia kwa mara ya kwanza pale Eva alipokula matunda ya mti aliokatazwa asile. Tukihoji kwanini Nuhu Nabii wa MUNGU alimlaani Caanan kwa makosa ya baba yake, itakuwa kama tunataka kuhoji pia ni kwanini sisi leo hii tunabeba laana ya Eva na Adamu wakati siyo sisi tuliokula tunda. Nafikiri hakuna mwanadamu anayeweza kusimama na kumuuliza MUNGU kwanini ulifanya hivyo, kwanini ulitulaani sisi? (Soma ISAYA 45:9 au WARUMI 9:14-21)

MUNGU hakosei na wala MUNGU hamuonei mtu wala kumpendelea mtu. Nuhu alikuwa ni Nabii wa MUNGU, hivyo basi laana ya Nuhu kwa Caanan ilipata baraka zote toka kwa MUNGU. Kama Nuhu angekuwa ametoa laana kwa uonevu bila kufuata utaratibu unaokubalika na MUNGU; basi MUNGU asingekubali Caanan alaanike, angeizuia hiyo laana isitokee.

Nina imani kwa maelezo hayo, utakuwa umeelewa ni kwanini Caanan alibeba laana ya baba yake, tena siyo Caanan tu, bali ni yeye na uzao wake wote uliofuatia. Hata sisi Waafrika tunabeba laana hiyo mpaka leo, lakini tukumbuke kwamba MUNGU aliyetupiga kwa laana, ndiye YEYE huyo huyo aliyetuletea UKOMBOZI kupitia kwa Mwanawe YESU KRISTO.


"Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam Mimi ndiye, wala hapana MUNGU mwingine ila Mimi; naua Mimi, naponya Mimi, nimejeruhi tena nimeponya; wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu". KUMBUKUMBU LA TORATI 32:39







Mkuu zitto junior hatuwezi kumwelewa MUNGU hata siku moja, akili zake, wala mawazo yake, hayachunguziki na Mwanadamu wala Malaika. Lakini tunaweza kulielewa NENO lake, kuliamini na kumtii Yeye kama MUUMBA wetu.
Kwa hiyo mzee baba unapingana na hitimisho la mtoa mada na unataka tukubali tu kuwa tumelaaniwa tena kwa kuwekwa alama nyeusi kwenye ngozi yetu ili waliobarikiwa watunyanyase vizuri na kutunyanyapaa? Not fair at all
 
Ham ndiye baba wa Canaan (Canaan imetumika Kama jamii,Ukoo,Kabila) hivyo Nuhu alipomlaani Canaan Ina maana uzao wa Ham (Yaani jamii au ukoo) wa Hamu ndio uliolaaniwa kwamba wawe watumwa kwa ndugu zao (Jamii, Koo za kina Shemu na Yaphet).
 
Alipompeleka mstari wa mbele askari wake ili auliwe halafu amle mke wa huyo askari,adhabu ilitolewa kwa mtoto aliyezaliwa(at least ni hekaya tu hakijawahi kutokea kitu kama hicho)
Characters zote za kwenye yale maandishi ni za kufikirika tu..
Kumbe ni hekaya.....
 
Kwa nini alilaaniwa Canaan ambaye hakujua kosa na si aliyemchungulia?
Kwa tunaosoma bible na protocol za ki Mungu Nuhu asingeweza kumlani Hamu mwanae maana amezaliwa chini ya baraka ya baba yake then kwa kuwa hamu amefanya ujinga na dhambi ana hatia kwahyo mwanae hana ulinzi wa baraka ya baba yake na laana inampata kirahisi kwa maana nyingine Nuhu angemlaani hamu angekuwa amejilani mwenyewe mfano Suleiman alikosea lakini kwa sababu ya daudi baba yake Mungu hamuadhibu Suleiman ila anakuja kuadhibiwa mwanae Suleiman means angemwadhibu Suleiman ni kama amemwadhibu Daudi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom