Mambo makubwa ambayo wengi hawayajui kumhusu Nabii Ibrahim

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,894
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Licha ya Umashuhuri wa jina lake, ambao mpaka leo hakuna mzee wa nyakati zake ambaye anamfikia kwa umaarufu na umashuhuri. Umashuhuri wa jina lake umebebwa na Ufuasi wa kufa kuzikana, machozi, jasho na damu kwa waumini wa dini zenye Chimbo lake ambazo ni Wayahudi, Wakristo, Waislam ambazo ndizo dini zenye ushawishi katika ulimwengu huu.

Pamoja na umashuhuri huo lakini Watu wengi kuna mambo makubwa yanayomhusu Nabii Ibrahim ambayo Wafuasi wake hawayajui. Na hicho ndicho nitakachofafanua leo kwa ufupi kama ifuatavyo;

1. Mama yake(Edina) Ibrahimu alikuwa Tasa;
Hii ilimfanya Baba yake Ibrahim aitwaye Tera kuoa mke wa pili ambaye alikuwa mtoto wa Mfalme wa Haran. Kumbuka Tera ametokea Uru ya ukaldayo(Iraq ya Leo). Pia Haran(ambayo leo ni Uturuki) ilikuwa sehemu ya Dola la Mesopotamia (Iraq ya leo).

Tera akiwa na miaka 39 akazaa mtoto wa kiume kwanza kwa huyo mke wa pili, mtoto hiyo akaitwa Haran akichukua jina la Babu mzaa Mamaake. Kisha ndipo Mke mkubwa akamzaa Nahori alafu akamzaa na Ibrahimu kwa kuchelewa, halafu mke mdogo akamzaa binti aitwaye Sara.

2. Ibrahimu na Sara ni Mtu na Dadaake. Baba mmoja mama mbalimbali. Ibrahim kazaliwa kutoka kwa mke mkubwa wakati Sarah akiwa amezaliwa kutoka kwa mke Mdogo.

3. Ibrahim alifukuzwa kwasababu Hakuwa Mrithi Halali wa Mali kutoka kwa Baba yake. Ibrahim alikuwa mtoto wa pili, na kwa sheria za zamani mtoto wa pili sio mrithi isipokuwa mtoto wa kwanza ambaye ni Kakaàke aliyeitwa Nahori.

Weka Akilini pia Mrithi wa mali sharti atoke kwa mke Mkubwa(wakwanza) hivyo Haran naye hakuwa sehemu ya Warithi ingawaje alikuwa mtoto wa kwanza kwa Tera hii ni kutokana na kuwa mama yake alikuwa mke mdogo.

Hata hivyo Haran alitarajiwa arithi kiti cha ufalme cha Babu yake aliyekuwa Mfalme wa Haran, lakini kwa bahati mbaya Haran alikufa mapema kabisa akiwa ameacha mtoto mdogo ambaye aliitwa Lutu.

Ibrahim alipewa tuu zawadi za kubeba kisha akaambiwa aondoke. Kama yeye baadaye alivyomfanyia ISHMAEL mtoto wake.

4. Ibrahimu alikuwa Uzao wa Shemu "sem"(uzao wa Semites) lakini alizaa pia na Hamites(Uzao wa Hamu) kupitia Hajiri Mmisri.

Wengi waliowahi kuzaa na Hamites ni pamoja na Nabii Musa alizaa na muethiopia aitwaye Sipora akazaa watoto wawili. Pia Suleiman naye alizaa na Malkia wa Sheba.

5. Ibrahimu kuondoka Uru wa ukaldayo ilikuwa ni lazima na wala sio Optional. Sababu kubwa ilikuwa ni Mambo ya Urithi na wala sio Mambo ya kiiimani kama inavyosimuliwa. Ni kama Ishmael alivyoondolewa yeye na Mamaake, Hajiri pale Canaan.

6. Mke wa Sarah alikuwa Mzuri kwa sababu Baba yake Terah alizaa na Watu wa Haran.

7. Ibrahim baada ya kifo cha Sarah Mkewe alimuoa tena, binamu yake aitwaye Ketura.
Huyu alimzalia watoto sita (wakiume), kati yao kuna mtoto anaitwa Midiani ambaye ndiye anatoa taifa la Wamidiani.

Ishmael alizaa watoto ambao pia walioa na kuoleana na Wamidiani ambao wanatoa sehemu ya Waarabu wa Saudi Arabia. Wamidiani ndio waliomnunua Yusufu kutoka kwa wana wa Yakobo (Waisraeli). Esau(Edom) alioa moja ya mabinti wa ISHMAEL(baba yao Mkubwa) katika watoto aliowazaa mmoja anaitwa Amaleki ambaye ndiye Baba wa Waamaleki.

8. Jumla ya watoto wa Ibrahim ni nane(hawa ni wakiume pekee waliohesabika), na hao ndio wanaunda mataifa yaliyopo hapo Mashariki ya kati hivi leo. Na hiyo ndio inabeba maana ya jina la Ibrahim "Baba wa Mataifa" kama alivyoahidiwa na Mungu wake.

Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kwahiyo wewe vyanzo vyako vipo sahihi zaidi kuliko vitabu vya dini vinavyosema Ibrahim aliambiwa na Mungu aondoke kwao aende nchi ya mbali.
 
Ungeambatanisha na chanzo cha hii historia ingekuwa vizuri zaidi.

Ni nzuri ila hapo namba 5 sikubaliani na hayo maelezo maana chanzo changu yaani mwanzo 12:1-4 hakisemi hayo ya mali ila ni Mungu ndiye aliyemuita Abram (Ibrahim).
 
Kibiblia pale mashariki ya kati ni ugomvi wa ndugu. Tukalime.

Tuje kwa Wamidiani. Wamidiani ni uzao wa Ibrahim na Keturah. Waliishi maeneo ya kusini mwa Israeli. Mke wa Musa anayeitwa Ziporah alikuwa mtoto wa kuhani wa Midiani aliyeitwa Yethro. Tunaambiwa kuwa huyu Ziporah alikuwa ni Muethiopia(Ethiops au Kush linamaanisha mtu mweusi na si nchi). Sasa hawa waarabu weupe wa Uarabuni walitoka wapi?

1700050496456.png
 
View attachment 2814508

Ndivyo Historia inavyodai
 
Back
Top Bottom