Kwaherini JF

Status
Not open for further replies.
madokta na ubora wa vifaa vya hosp vinatofautiana.
Hii ni kweli kabisa, nina uzoefu na hili.

Nilipatwa na changamoto flani mwaka juzi, daktari mmoja akaniambia kama nina bahati sana nitaenda mwaka na nusu, na kama nikinusurika nitakuwa kipofu. Mara tena akasema sijui itabidi nifanyiwe upasuaji wa ubongo...

Nikaja kuonana na daktari mwingine akaniambia kuna dawa naweza kujaribu, ila hazifanyi vizuri kwa kila mtu. Nikazitumia na kwa bahati nzuri zikanikubali, nipo nadunda nazo tu.

Kwahiyo matumaini yapo.
 
Dah
Pole sana Depal🥹
Umepitia mitihani na hatujui💔
 
Hey people,

Uzi huu ni wa kuwaaga wanaJF wenzangu

Nimekutwa na cancer ambayo kimsingi nimepewa taarifa kwamba ndani ya miezi miwili sitakuwepo

Naumia lakini sina jinsi
Joanah
Ni wewe?
Kweli upo serious, na hiki ulichoandika ni kweli?

Kama ni kweli
Basi Jipe moyo,
Hautakufa sasahivi Joanah,
Unao muda bado wa kuishi.
Sidhani kama umeshaimaliza kusudi lako hapa Duniani .

Mungu aliye tabibu Mkuu arejeshe afya yako na kukupa miaka mingine Tena ya kuishi.

Heaven Sent
 
Hey people,

Uzi huu ni wa kuwaaga wanaJF wenzangu

Nimekutwa na cancer ambayo kimsingi nimepewa taarifa kwamba ndani ya miezi miwili sitakuwepo

Naumia lakini sina jinsi
Pole sana kipenzi Joanah. Hiyo cancer ni ya eneo gani la mwili? Na huduma ya mionzi imeshindikana kabisa?
One love mamii❤️
 
Hezekiah alipewa taarifa ya kufa kwake siku chache zijazo ila aliikataa hiyo taarifa na kuomba Mungu, Mungu alimpa miaka mingine 15 ya uhai.

2 Wafalme 20
1 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,

3 Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

4 Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,

5 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.

6 Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.

Madaktari hawana hatima ya maisha yako, nikimaanisha hawajabeba mwisho wako wa kuishi kwako, wao wamekupa tu majibu ya kitaalumu, unaweza kuyakataa kwa kuelekeza uso wako mbele za Mungu.

Mungu anaweza kufanya jambo jipya kwako, mwamini sasa.

Usiogope lipo tumaini la kuishi tena.
 
Bro acha basi.

Kuna auntie yetu (shoga yake mama) aliambiwa mwaka jana mwenzi wa 11 ata RIP lakini mpaka leo navyoandika yupo. Ana kansa ya titi.

Juzi hapa ameambiwa sijui cell mpya zimezaliwa sijui nini (lugha ya kidaktari kuna muda siielewi)

Kwahivyo bado kuna hope, Pole…
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…