Kwaherini JF

Kwaherini JF

Status
Not open for further replies.
Sio wote mkuu watapitia mateso.. mf. Si baba yetu niseme week yake ya mwisho ndio alipitia maumivu ya kiuno wkend.. j3 akafanyiwa vipimo.. hata majibu hayajatoka akapumzika mazima. Na hiyo siku alimka fresh.. vikabadilika ghalfa na ndani ya masaa matatu akapumzika.

Maybe inategemea na aina ya cancer..

Huu uzi niliusoma alfajiri kikawaida.. now nasikia hadi moyo unauma
Sijui anayefariki anajisikiaje.. kazi ipo kwa wanaobaki.
Joanah kama uzi wako una ukweli.. basi wape taarifa nduguzo wa karibu. Vifo vya ghafla vinaumiza sana wanaobaki 🙌

Mungu akutie nguvu..
Mimi bado nipo njia panda, kuna saa ukisoma maoni unaona kama masihara ila kuna saa inakuja kama kweli!.

Acha niendelee kukataa kwamba si kweli,mauti na uzima zi kinywani mwa mtu.
Joanah hauta kufa , dunia inakuhitaji sana, jamii bado ina haja nawe.
 
Hey people,

Uzi huu ni wa kuwaaga wanaJF wenzangu

Nimekutwa na cancer ambayo kimsingi nimepewa taarifa kwamba ndani ya miezi miwili sitakuwepo

Naumia lakini sina jinsi
Pole usihofu,Mungu mkubwa,Kuna Mtu yupo ujerumani,aliuza nyumba yake hapa Dodoma ili wadogo zake wagawane Hela,kwani yeye aliambiwa hatakaa zaidi ya mwaka!Huu ni mwaka wa15 yupo na mdogo wake mmoja aliyefaidi mgao,ndie kafa!
 
maisha ya mtu hupangwa na Mungu,Mungu pekee ndiye anayejua mwisho wa maisha ya mtu,yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.
USIKIRI mauti ,KATAA roho ya mauti,sema sitakufa bali nitaishi ili kuyasimulia matendo makuu ya Mungu.
Mungu wetu ni wa kutenda makuu yale yasiyowezekana Amini YESU anaweza kukuponya kabisa.
Kwa kupigwa kwake Yesu na kwa damu yake Yesu,tumepokea neema ya kuponywa na kupata uzima.

AMINI kuwa Mungu hajakuacha ,Mungu anakupenda anakuwazia mema anapenda upone ,ndio maana kamtuma YESU ili wote wanaomuamini waponywe.
 
Bro me sikutishi, nimekupa uhalisia uliotokea kwetu..
pia madokta na ubora wa vifaa vya hosp vinatofautiana. Sie kwa baba, Hosp M.. walipomaliza operation na matibabu kuna dawa wakamzuia baba kuzitumia (hiyo ni last year) akawa fresh kabisaaa.
Huo mwezi kuelekea week yake ya mwisho alianza kupoteza hamu ya kula. Nyama ikichemshwa tu anakula fresh, ikiungwa akila anatapika.. akawa anabagua vyakula.. tukaona anadeka, tukawa hatumuamini.. maana alikuwa fresh haumwi .. ni kama sahvi hapa ambavyo hatukuamini..
Hali ilikuja kubadilika ghafla mno… kwenda hosp Lu.. kwanza wakasema kule M walikosea.. zile dawa hakutakiwa kuziacha..

Hizi hosp baadhi bana ni Mungu tu atusaidie
Namjua mtoto wa mtu ambaye alifanyiwa OP ya kidole tumbo. Kumbe hakuwa na hiyo shida, ikapelekea watingishe utumbo. Imagine mtoto anamaliza miezi 3/4/5 bila kupoop.. akitaka kupoop ni lazima apigwe bomba.. wakabadili hosp sana sana mpaka wakaja kuponea hosp X

So nakushauri.. rudia vipimo bro
Kisha washirikishe familia yako
Mwenyezi Mungu akutangulie…
Umenitisha rasmi

Nilikuwa na hopes kwamba vipimo vitakuwa vimekosewa kwasababu sijisikii kuumwa, kumbe naweza kupitia maumivu wiki za mwisho 🥺
 
Pole sana mkuu@joanah usikate tamaa kabisa kwani anayeamua hatima ni Mwenyezi Mungu.

Nakushauri usiwapuuze hata wataalam wa tiba asilia watafute unaweza kupata suluhu ya changamoto yako.

Pole sana mkuu!!
 
Huu ushauri wa kupima tena nipo nao natarajia kufanya vipimo tena ndani ya wiki hii inayoanza

Kimsingi sijui ni how nimepewa majibu hayo, sina maumivu na wala sijisikii kuumwa kabisa lakini taarifa iliyopo ni hiyo
Vyema kama utafanya hivyo mjukuu

Babu yako nina mawazo ya hovyo, kwamba vipi kama hayo majibu amekupatia yule daktari aliyekuomba mzigo na ukamkatalia

Ama yule X wako uliyemuacha miaka 2 iliyopita amechonga na rafiki yake daktari ili aone ukipoteza maisha kwa mawazo ya ugonjwa fake wa cancer

Again, Mungu aendelee kukutunza kwaajili ya sisi Babu zako 🙏🙏🙏
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom