Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,762
- 26,051
Mkuu BAK, kula tano.
Unafahamu kitu kimoja, yees old skool umenikumbusha mbali sana masuala ya Casanova.
Unafahamu miaka ile kati ya 80s na 90s muziki ulikuwa ni wa nje tu, kila ukiingia nyumba za walokuwa na uwezo, seti za televisheni zao zilikuwa zikipiga miziki tu ni miziki kwa sana.
Vikao kwenye magogo vya washikaji, mechi za mpira pale Gymkhana, Muhimbili au Oysterbay (pale kwenye kamzunguko kelekea shuleni) na stories za ngumi za hapa na pale kugombania totos kati ya washikaji enzi zile akina Kinje ( huyu kaanza ukorofi miaka mingi) Idi Janguo na vijana wengine wenzetu wengi tu.
Saramanda pale makutano ya Mansfield na Mkwepu pamoja na Snow Cream, pia umenikumbusha enzi zangu za kuhakikisha magazeti yote ya mzee wangu (Mungu amrehemu huko mbele ya haki alikotangulia) aliyokuwa akileta nyumbani ninayakusanya na kuyauza kwa akina mama ntilie kwa ajili ya kupakia maandazi na vitumbua.
Nilikuwa sikosi angalau shilingi ishirini mfukoni ili niwahi Avalon au Empire Cinemas kama sio Drive Inn.
Aisee we acha tu, vijana wa miaka ile tulijifunza kushughulika na kuchakarika na hapa tulipo leo kwenye mid 40s tunapaswa kujikumbusha mambo haya na kuwasimulia wanetu na kuwafunza kuwa wastahamilivu kwenye maisha.
Namtakia kila mwana JF kheri ya mwaka Mpya wenye furaha na amani miyoyoni na kwa wewe BAK na wale wapenzi wa mpira wengine basi kesho tukutane pale kwenye jukwaa letu tukufu la Arsena Thread.