Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mkuu unataka uwekeze kivipi,kwenye Equity Market,au Money market? sielewi una maanisha nini....
 
Nina laki moja naweza kuiwekeza wapi ili nipate faida mara mbili au zaidi?
muombe mtu anaejua kukaanga karanga kwa kiwango kizuri akuelekeze kisha nunua uzinunue nunua karanga kwa jumla anza kukaanga na zifungashe vizuri kisha tafuta vijiwe maeneo ya stand,mashuleni,na sehemu zote zenye mkusanyiko wa watu,,kwa mtaji uo unatosha sana usione haya we fanya pia zingatia usafi na ww muda wote uwe smart,,,,ujasema uko wapi mimi niko arusha nauza karanga na mchele kwa bei ya jumla unaweza ukaniPM
 
Waweza anza biashara ya samaki,unaenda zako feri/mwaloni unachukua wabichi,ukirudi unawakaanga,kisha unauza,wallah utarudi kuniambia,Kikubwa,wenzio huwa wanawakaanga kwa kuwatia chumvi tu,wewe unaweza kuwaroga wateja kwa kuongezea ndimu/limao,vitunguu saumu na tangawizi ,ladha haitakuwa kama ya competitors wako.

Kama uko sehemu yenye joto kama Dar funga Ice cream,Barafu za Ubuyu weka kwenye Deli peleka shuleni,hasa shule za msingi,utashangaa,huwa zinatoa faida double,kikubwa ziwe laini ubuyu ukolee,mpaka watu wazima watakufata nyumbani(Hii nna Experience Nayo)

Waweza uza vinywaji Baridi kama Soda,Maji na Juice....


Kila la Kheri Mkuu
 
Back
Top Bottom