Laki ni pesa nyingi sana haswa kama huna aibu ktk biashara utakayoifanya tafuta sehemu nzuri anza biashara ya mahindi ya kuchoma ,au tembeza karanga za kuchemsha kama upo dar au ktk majiji na miji yote ya Tanzania inalipa
Fanya hivi ndugu...tafuta mtu anaefuga kuku WA mayai kwa wingi halafu muombe akuuzie bei ya jumla..huku nilipo mm Ni 5000 bei ya jumla halafu WW tafuta wateja wa chips wauzie 6500 sabab maduka mengi wanauza 7000 hiyo itakuwa imekupa WW competitive advantage...kwahiyo bas utaanza na tray 10 ambazo zitagharimu 50000 Tu..
ukienda kununua tray ya kubebea hayo mayai bei yake haizidi 10000...mpaka hapo umetumia 60000... Hapa cha kuangalia Ni kuhakikisha unapata faida ya sh 1000 kwa Kila tray na usambaze kumi kila siku...ile sh 500 inayobaki kwa kila tray ifanye kama running cost...cha muhim hakikisha sehem unayotolea mayai haipo mbali na wateja Wako kusudi upunguze gharama zisizo za lazima na mayai kuvunjika...
mimi nilianza na mtaji wa elfu 80000 na sasa Nina uwezo wa kusambaza tray 150 kwa siku....usikubali mtu yeyote akukatishe tamaa eti mpaka uwe na mamilion ya pesa ndio ufanye biashara inayoeleweka...jiamin na mshirikishe Mungu hiyo pesa Ni nyingi sanaaa...go big...
kama upo jirani na shamba la miwa nenda ukanunue ya tsh 5000 harafu kaa pembeni ya barabara katakata vipande weka kwenye mfuko, kila kimfuko tsh 500, itakulipa na utakuza mtaji.
Unaweza fanya biashara ya kuuza juice, we nenda soko kuu nunua maparachichi, changanya na yale yalioregea kabisa ambayo hayafai kununua, blenda nunua ya elfu 40, garoni ya lita 5 utanunua tsh 1000 au omba kwa mtu, umeme tumia kwa kificho hapo unapoishi ukipata mtaji mkubwa changia luku, barafu nunua 1 buku liponde ponde kisha changanya kwenye juice.
Soko la juice beba garon lako la juice na glass zunguka nalo kwenye mikusanyiko ya watu hasa muda wa mchana.
NB ; matunda usinunue mazima nunua yale yanayokaribia kuharibika(munapatana bei) kisha unanunua kitunguu swaumu kwaajili ya kukata harufu.
Makazi yako ni wapi? Angalia mazingira yanayokuzunguka huduma gani inapatikana kwa uhaba halafu angalia na kiasi ulichonacho kama kinaruhusu tumia fursa. Usiogope changamoto kwani hakuna jambo lolote lisilokuwa na changamoto hapa duniani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.