Namna bora ya kumsaidia Bwana Mdogo mtaji wa Biashara

thatHUMBLEguy

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
223
522
Mwaka 2014 kuna bwana mdogo, alikataa shule akiwa form two, akidai kuwa hapandishi, ni kweli hakuwa akifanya vizuri darasani. Akawa ni mtu wa kwenda minadani tu.

Mwaka 2018, aliomba msaada wa sh 210,000 ambapo alidai anaenda nunua mbuzi kwa ajili ya kuanza kuuza. Sikua na mawasiliano naye ya mfululizo, lakini mara chache niliweza kufuatilia progress yake, just out of interest, Ilikuwa ni nzuri. Kwa kweli si haba, tumekutana wote nyumbani sikukuu amepiga hatua kubwa kiuchumi. Kwa ufupi, hivi sasa ni Mfanyabiashara wa Mbuzi minadani.

Sasa, jana baada ya Pilau ya Christmas, tulikaa kikao cha familia. Na moja ya agenda, kuna kijana mwingine, kapewa mtaji—fremu kalipiwa mwaka mzima, imesanifiwa vyema, na mtaji wa nguo kiasi cha sh Mil 3. Sasa hivi mtaji umeshuka, almost to zero, na maelezo yadaiwa ni starehe za dogo. Dogo ni muhitimu wa Chuo mwaka 2021, ajira ikawa ngumu ndipo ikaamuliwa asaidiwe mtaji.

Kwa kweli nilishindwa mlaumu yule dogo, zaidi nilimlaumu kaka yangu aliyempa mtaji kuwa yeye ndiye chanzo. Kwanini niliamlaumu yeye?

Ndio sababu ya kuandika uzi huu, ili tuweze kushare mawazo pamoja namna gani tunaweza saidia wadogo zetu kiuchumi katika namna ambayo ni yenye ufanisi zaidi.

Kwa mtu yeyote yule anayefanya biashara anakubaliana kuwa biashara ni ngumu sana kuliko kuajiriwa. Wengi tunaweza mudu kazi ya kuajiriwa na kulipwa mshahara, lakini wachache ndio wakamudu biashara.

Biashara ni ngumu sana kwa sababu;
I. INAHITAJI KULINDA NA KUKUZA MTAJI

II. KUWA MBUNIFU SANA.

Kwa uzoefu wangu wa biashara, hilo la kwanza ni gumu sana na ndio hapo wengi na ndugu wengi huishia kugombana pindi wasaidiapo mitaji ya biashara. Nitagusia hilo la kwanza tu, kwani hapo ndio mtego ulipo.

Vijana wengi wanaohitaji mitaji ya biashara, wanahitaji si kwa sababu wanayo mawazo fulani ya kibiashara hivyo wanahitaji kuyatekeleza, bali ni kwa sababu wamekosa ajira. Tukiwa bado watoto, tunaondoka majumbani kwetu, tunaenda mashuleni, huko kwa muda wa takribani miaka 20, tunafunzwa maisha ya ofisini—SIO BIASHARA—kisha tunakosa hizo kazi za ofisini ndio sasa tunatafuta mitaji ya biashara ambayo toka utoto wetu hadi kufikia muda huo ambao tunauhitaji, hatujafunzwa chochote kuhusu biashara. Tatizo kuu linaanzia hapa.

Nimesema hapo juu kuwa maisha biashara inahitaji Kulinda na kukuza mtaji. Vipi kuhusu kuutafuta?

Ukweli ni kwamba, mtu aliyeacha shule akiwa kijana mdogo ndiye haswa anayeenda kuutafuta mtaji. Umri wake bado ni mdogo, anaweza enda popote na kufanya chochote. Katika maisha hayo ya kuhangaika na kuutafuta mtaji mfano anaweza ajiriwa akawa muuza karanga, kwa ujira wa malazi, milo miwili na mshahara wa sh ef 40 kwa mwezi. Hapo anapata mambo matatu; anadunduliza na kutunza hela, anajifunza misingi na miiko ya biashara na kubwa zaidi anajifunza nidhamu ya fedha. Mtu huyu hadi anafikia miaka 25, tayari ana elimu kubwa kuhusu biashara, huku mwenzake ambaye yeye aliendelea na sekondari, chuo yote haya hana nafasi ya kuyajua. So, kijana anayeingia mtaani toka chuo, zaidi ya miaka 24, umri wa kutafuta mtaji umeshampita. Pia anayo haiba ambayo ni ngumu kwake kufanya kazi ambazo primary/secondary school dropout angeweza zifanya na kupata mtaji. Huyu anapaswa pewa mtaji. Bahati mbaya, anakosa mambo hayo mawili ya msingi—Si kwa kutaka kwake—Hajui misingi na miiko ya biashara, hana nidhamu ya fedha—sababu hajapitia maisha ya kumfunza nidhamu ya fedha kibiashara.

Kijana huyu, yuko nyumbani. Ajira hana, anamsumbua bimkubwa kwa vocha na mizinga ya hapa na pale. Anawasumbua nyie ndugu zake. Sometimes vitu vinapotea pale nyumbani, mnasikia kamtia mtu mimba. Mabro, mnaamua, hapana tumpe mtaji. Mnamuambia aseme biashara gani anataka. Naye sababu amekuwa trained for 20 years kuwa destiny yake ni white collar jobs, naye anatafuta 'white collar business'. Mpesa, Duka la nguo, Pombe Shop, Pub, Kuchoma CDs n.k!

Makosa yanapoanzia.

I. Kijana anatafuta kibanda cha biashara na mnalipa kodi yote takiwa.
II. Mnamkarabatia kila kitu dukani.
III. Mnalipia leseni zote.
IV. Mnapa mtaji, afuate mzigo wa Milioni Tatu, Kariakoo au Makoroboi au Uganda.
Then, tunakaa pembeni tukiamini tayari tumemkomboa kiuchumi mdogo wetu. ITS A GRAVE MISTAKE.

Tumempa mtaji dogo, jambo jema! Je, tunahakika gani kuwa ataulinda? Je ataukuza? Tukishampa mtaji dogo, hiyo ni just 10% ya wajibu wetu, the remaining 90% ni jukumu letu kuhakikisha kuwa mtaji huo unalindwa na kukua. Hakuna jambo geni nitaloeleza, bali ni mambo ambayo hatuyatazami sawa sawa.

Nini kinaua mtaji wa biashara?

Jibu ni moja tu; MAISHA BINAFSI. Biashara yoyote inaathiriwa na maisha yako binafsi. Maisha yako binafsi yasipokuwa na nidhamu, basi hata biashara yako itaathirika kwa sababu zifuatazo.

i. Mfano, kijana anakaa nyumbani. Muda mchache tu anapopata mtaji, anataka kwenda kupanga na kujitegemea kimaisha. Hili ni kosa, kwani anaongeza gharama zake binafsi za maisha, anaongeza uhuru wake binafsi wa kimaisha ambao unaweza mpelekea kwenye mienendo ambayo si rafiki mfano, umalaya, pombe, clubbing, kurogwa na hatimaye kuathiri biashara yake.

ii. Anaweza kuwa anakaa nyumbani, lakini hakuna mtu ambaye anaweza mdhibiti maisha yake binafsi ili yawe na nidhamu.

iii. Hatuzingatii hulka za muomba mtaji na kumbe zinaathiri ufanisi kwenye biashara. Mfano, unampa vipi mtaji mdogo wako ambaye unajua ni mlevi? Ambaye ni malaya? Ambaye anapenda kuzurura hovyo?

Hivyo ili tusaidie wadogo zetu na wafanikiwe pasi na kupoteza fedha bure, haya ni ya kuzingatia sana.

1. Tuzijue tabia halisi za wadogo zetu. Maisha ya chuo ni maisha ya hovyo sana. Ndipo sehemu watu hupindukia kwenye mitego ya pombe, umalaya na kamari. Wengine hata kwenye familia zetu hatujui, sababu vyuoni ni mbali nasi. Unaweza mpa mtaji mdogo wako, kumbe ana shida ya siri ya ulevi au kamari. Tuwajue kwanza. Jua kila kitu cha mdogo wake, hata mademu zake wajue ili uweze mshauri sawa sawa.

2. Tuhakikishe, wanaishi sehemu ambazo tunaweza wamonitor, hasa nyumbani. Mtu anayeomba mtaji, hapaswi kupewa uhuru wa kupanga kwanza hadi atakaposimama vyema kiuchumi. Mama pale nyumbani, ni rahisi kumchunguza na akashare nanyi kama mpo mbali.

3. Tupeleleze uhalisia wa biashara zitakiwazo. Mfano, kijana anaomba capital afungue duka la nguo. Lakini, je ni kweli inatoka? Na hiyo biashara anayoitaka kweli anaimudu, au anaomba kama fashion au shinikizo.

4. Simple to Complex approach. Kama anataka mtaji wa kufungua Mpesa, badala ya kuchukua Frame town centre, ambayo unalipa Kodi Milioni 2 kwa mwaka, tengeneza banda simple la Ceiling Board au mbao kwa laki 3, liweke mazingira ya kawaida na mtaji hata wa Milioni tu za float, tena msajilie mtandao mmoja tu. Kama anaakili timamu, utamuona anajiongeza kusajili zingine. then aanzie hapo huku ukimonitor trend na anajenga uzoefu wa biashara ambao hana. Mtu hawezi jenga uwezo kwa kuanzia mazingira complex, ndio maana hata ajira, mtu hawezi toka fresh from school akawa MD wa Taasisi, anaanzia junior officer kupata practical education ambayo shule haipo ndio anapanda. Unampaje mtu mtaji unamuwekea CRDB, NMB, MOBILE PESA ZOTE, NA FLOATING CAPITAL YA MIL HATA 2 MKONONI, ambaye hajawaji hata fanya biashara, si zitamuheusha? Utamlaumu kweli huyo bwana mdogo au ni wewe bro ndiye mwenye makosa?

5. Utenge mtaji wote utakiwao, lakini tutoe kidogo kidogo huku tukisoma trend. Mfano, kodi badala ya kulipa mwaka, lipa miezi mitatu then muambie biashara yake ndio italipa kodi ya miezi inayofuatia. Lakini, itenge pembeni, bila ya yeye kujua, ikitokea amekwama ndani ya miezi mitatu, basi unaweza chip in ila kwa kauli ya kukopesha. KAMWE USIMPE MTAJI, MKOPESHE. BILA MINDSET YA DENI, HAKUNA BIASHARA ATAKAYOFANYA. SERIOUSNESS COMES FROM RESPONSIBILITIES. Kama mtaji wa nguo hesabu ameomba Mil 3. Aanze na laki 5 tu. Hii inatoa nafasi ya yeye kujenga uzoefu huku ukimsoma wewe kabla ya kutoa hela zaidi.

6. Monitor accounts. Fedha yote ya biashara iwe kwenye akaunti, tena ya bank. Mauzo yote ya kila siku yawekwe bank. Akaunti iwekwe pia namba yako ya simu, ili ikiingia na kutoka hela ujue. Hii itampa woga wa matumizi ya hovyo na pia itakuepushia wewe pia na surprises. AJUE KUWA WEWE NI MKOPESHAJI WAKE HIVYO MNAUBIA WA PAMOJA.

7. Mahitaji yake binafsi yawe budgeted na yatoke kwa mwezi. Ni lazima ana mahitaji yake; uyajue kwa mwezi ni kiasi gani, na yatoke mara moja tu kwa mwezi na yatoke kwenye faida itayozalishwa baada ya gharama zote za biashara kutoka. Hii itamuongezea nidhamu ya fedha na maisha na kudhibiti matumizi yake.

Hakuna ajira, tusaidie wadogo zetu kibiashara, ila tusiwasaidie kijuha.
 
Seen.
 
Ili jamaa lina akili
 
Back
Top Bottom