Kwa hoja za Babu Tale bungeni, ninakiri kuna ulazima wa marekebisho ya Katiba kwa sifa za mtu kuwa Mbunge

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,090
22,361
Ninawasalimu kwa jina la Chama Pendwa CCM.

Ninaandika nikiwa nina hasira kali sana dhidi ya mbunge aitwae Babu Tale kutokana na hoja zake zilizokosa weledi huko bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara inayohusika na sanaa. Huyu babu kwa kukosa weledi alitaja majina ya wasanii katika hali iliyoonyesha kabisa ni chuki dhidi ya baadhi ya wasanii wakati alipaswa kuwa mwakilishi wa wasanii wote. Ni kauli ambazo sina haja ya kuzirudia hapa maana zinatrend kwa sasa.

Ninamkumbusha Babu Tale kujua kwamba anapokuwa bungeni anakuwa mwakilishi wa watanzania wote na sio mwakilishi wa WCB wala Tiptop. Kitendo cha kumtetea Kasim Mganga na kumponda Luludiva sio cha kiungwana. Pia ninamshauri mwaka 2025 atafute kazi nyingine za kufanya kwasababu wabunge mizigo hawatarudi bungeni.

Tunapaswa kubadili katiba ili angalau bungeni wasiingie vilaza kama kina Tale na kuchafua hadhi ya bunge.

Mbunge Babu Tale akichangia bajeti ya wizara ya utamaduni​
 
Mbunge anayejiita chawa unategemea aseme nini sasa,Mwingine huyu hapa yaani utadhani bunge limeingiwa na mahurani,
JamiiForums-911532656.jpg
 
Nilimuona hata mimi wakati anachangia mawazo yake wakati Waziri mwenye dhamana ya Michezo na burudani/utamaduni alipokuwa akiwasilisha bajeti yake!

Kiufupi Babu Tale anaumudu Umeneja tu wa timu yake ya Wasafi na Tiptop Connection! Ila siyo Ubunge. Maana muda wote aliutumia kuwasema BASATA na COSOTA kwa sababu tu wamekuwa na utaratibu wa kufungia Wasanii wasio jitambua, na pia nyimbo zilizo kinyume na maadili ya Mtanzania!

Ifikie wakati 2025, watu wasio na sifa ya kuwa Wabunge, wafanye tu shughuli zao za kila siku za kuwaingizia kipato! Na hivyo Bunge jipya liundwe na watu smart kichwani!
 
Unafanya kosa alilolifanya yeye la kumsahambulia msanii, na ww unamshambulia yeye.
Nina haki ya kumshambulia kwasababu hela nazolipa kodi kuna ambazo analipwa yeye kuniwakilisha bungeni. Ubunge wake sio suala lake binafsi.
 
Hapo mmeshashiba machalali mmeshushia na mbege basi mnaropoka tu vijana wa tapeli wa taifa.

Hoja ya Babu tale ipo very clear kuna upendeleo kwenye kufungia muziki na kugawa loyalties kwa wasanii.

Mtu akiimba haleluya wimbo unafungiwa mwingine akiimba kumamak wimbo unapewa tuzo.
 
Haya ndo madhara ya vilaza kuingia bungeni..
Hakuna kilaza anaingia bungeni nyinyi washamba mliopita madarasani inabidi nchi itenge bajeti mpewe exposure. Bado hamuilewi dunia ndio maana mastermind street smart kama Tale mnamuona kilaza.
 
Hapo mmeshashiba machalali mmeshushia na mbege basi mnaropoka tu vijana wa tapeli wa taifa.

Hoja ya Babu tale ipo very clear kuna upendeleo kwenye kufungia muziki na kugawa loyalties kwa wasanii.

Mtu akiimba haleluya wimbo unafungiwa mwingine akiimba kumamak wimbo unapewa tuzo.
Loyalties = Royalties... wakati mwingine uwe na adabu unapochangia uzi wa kisomi.
 
Hakuna kilaza anaingia bungeni nyinyi washamba mliopita madarasani inabidi nchi itenge bajeti mpewe exposure. Bado hamuilewi dunia ndio maana mastermind street smart kama Tale mnamuona kilaza.
Mastermind kwa familia yake na huko WCB. Mtu aliyeliambia taifa kwamba huwa hafui chupi zake baada ya mkewe kuaga dunia ni wa kupuuzwa tu.
 
Ninawasalimu kwa jina la Chama Pendwa CCM.

Ninaandika nikiwa nina hasira kali sana dhidi ya mbunge aitwae Babu Tale kutokana na hoja zake zilizokosa weledi huko bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara inayohusika na sanaa. Huyu babu kwa kukosa weledi alitaja majina ya wasanii katika hali iliyoonyesha kabisa ni chuki dhidi ya baadhi ya wasanii wakati alipaswa kuwa mwakilishi wa wasanii wote. Ni kauli ambazo sina haja ya kuzirudia hapa maana zinatrend kwa sasa.

Ninamkumbusha Babu Tale kujua kwamba anapokuwa bungeni anakuwa mwakilishi wa watanzania wote na sio mwakilishi wa WCB wala Tiptop. Kitendo cha kumtetea Kasim Mganga na kumponda Luludiva sio cha kiungwana. Pia ninamshauri mwaka 2025 atafute kazi nyingine za kufanya kwasababu wabunge mizigo hawatarudi bungeni.

Tunapaswa kubadili katiba ili angalau bungeni wasiingie vilaza kama kina Tale na kuchafua hadhi ya bunge.
Hayo ndiyo mazao ya jiwe baada ya kubaka uchaguzi
 
Back
Top Bottom