Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
1. Unapoona pale Bunge linashindwa kuweka maridhiano kati ya Wabunge kwa jambo dogo, jua Spika ni tatizo!
2. Unapoona Spika anatoa maamuzi ya haraka na ya jazba ya jambo lililopaswa kupelekwa na kujadiliwa kwanza na kamati za bunge ujue ni vigumu sana kuleta umoja wa wabunge.
Bahati nzuri, mimi ni mfuatliliaji na mtizamaji kupitia media mbalimbali za mabunge ya nchi za Jumuia ya madola nk.
Mfano Bunge la Uingereza, Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini nk. Mojawapo ya kazi kubwa ya Spika ni kuwaweka Wabunge sawa pale hoja zinapokinzana ha hata inapotokea kuvurugana au kugomea bunge. Mfano issue ya Brexit pale bunge la England lilipokuwa likijadili jambo hilo. Au bunge la Kenya pale walipoparaganyika kuhusu issue ya Raisi na Makamu wake kushtakiwa ICC.
Tuliona pia pale Uganda issue ya majuzi kuhusu Raisi Museveni kuweka muswada wa kurefusha umri wa Rais.
Kwa mifano hii mitatu kwa mtu aliyefuatilia,angegundua tofauti ya aina ya uendeshaji wa bunge letu katika judgements hasa za spika, weledi na uthamini wa wabunge na Mabunge hayo niliyoyataja.
Hapa kwetu, ni mara nyingi Spika analoose self control ya jambo dogo ambapo Kamati za Bunge zingeweza kumsaidia na bunge likaendelea vyema na mambo ya msingi!
Mfano. Spika,bila kutaja msingi wa hoja anasema" Piga ua pamoja na Corona iliyopo,lazima bajeti zote zipitiwe na hakuna kusimama na hakuna mbunge kuondoka " Wakati huo huo, Waziri wa Afya yuko bungeni na anatoa maelekezo kuwa" Inapotokea mtu kapatikana na Corona case, lazima walioshiriki nae karibu wasakwe wawekwe karantini"!
Kwa case kama hii mfano,inatokea Mbunge ndani ya Bunge kaugua Corona,what next? Je, hapo kwa akili ya kawaida kama Spika,tegemea mpasuko wa Bunge ambao hauna tofauti na ule wa Brexit,kuwa tutoke au tubaki?
Nilitaraji hapa Spika ( kwa hoja na ushauri) aunganishe bunge na Wabunge ili maamuzi ya busara yafanyike! Tukumbuke, Wizara imeshatamka hatua za kuchukua, Spika naye alishatamka hakuna kutoka!
Hili,nasikitika na sina uhakika kilichofanyika kati ya Wabunge ndiyo njoa sahihi ya mshikamano wa Kibunge.
Kauli za utengano zilionekana waziwazi,wengine wakatoka,wengine wakabaki! Hata hivyo,viti vilionekana wazi zaidi kuashiria kuna waliotoka kimyakimya!
Madhara yake tumeyaona:-
1. Spika na KUB kutupiana lawama na maneno yasiyofaa!
2. Wabunge baadhi kufukuzwa uanachama na kuongeza mtafaruku wa Bunge.
3. Kudaiana kirudisha posho ( ambalo ni jambo la aibu kabisa)
4. Huenda hili lisiishie hapo,hata familia za wabunge, wapiga kura, wanachama wa vyama vya wabunge hao, chama chao nk. vikaingia katika mizozo isiyokuwa ya lazima.
Kwa maoni yangu, mambo kama haya yangeweza kuepukika pale tuu awali, ambapo nguvu ya Spika ingetumika ipasavyo kuunganisha bunge na Wabunge kwa ujumla wake bila kujali tofauti ya vyama.