Hivi Bungeni ni lazima kila mbunge achangie hoja? Babu Tale anatia aibu Sana

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,564
50,403
2020 kulikuwa na uchaguzi mkuu (hapana, uchafuzi mkuu ) uliowaingiza bungeni watu wasiofaa kuwa hata mabalozi wa nyumba kumi.

Hawatambui hadhi yao,
Hawatambui majukumu yao,
Hawajui chochote.

Miongoni mwa watu hao ni Babu Tale. Akisimama bungeni ili atoe mchango wake mimi huwa naanza kuona aibu.

Anaongea vioja na vihoja muda wote. Maelezo yake yanakosa mtiririko mithili ya mtoto anayejifunza kuongea, yaani hana hoja, hajui anachotaka kusema na anarudia rudia neno moja hata mara 5 ili kupoteza muda.

Narudia tena, Babu Tale akisimama bungeni ili kuchangia mimi naona aibu.

Sasa nauliza; ni lazima kila mbunge achangie bungeni? Kama hakuna ulazima Babu Tale akae kimya.

IMG_20220622_183632_921.jpg
 
Back
Top Bottom