Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Mnapoteza muda kubishana na mtu huyu ambaye hajui hata hoja iliyo mezani zaidi ya kubisha kila linalotoka nje ya magamba. Dawa yake nyie endeleeni na mjadala, mwacheni abishane na hewa. Akiona vema aanzishe hata thread achangie mwenyewe.
Ndivyo tulivyomfanya malaria sugu.
 
Hamna zaidi ya kutukana na kuongelea watu. Nawaonea huruma Watanzania wanaowachagua.

Asante dada Regia kwa thread yako nzuri na kututegulia kitendawili.
kumbe FaizaFoxy ni mwanaume? Sasa ya nini kujivalisha hijab? Yaani ni dume jike,lol ptuu! Kazi unayoifanya humu JF ni ngumu na huwezi shinda nguvu ya umma..ptuu!
 
Huyo ndio Rosti Tamu..............Dhambi ya kuichagua Magamba kwa mara nyingine lazima iwatafune wana wa Igunga kwa kurudia makosa yao.
 
Hamna zaidi ya kutukana na kuongelea watu. Nawaonea huruma Watanzania wanaowachagua.

Asante dada Regia kwa thread yako nzuri na kututegulia kitendawili.
kumbe FaizaFoxy ni mwanaume? Sasa ya nini kujivalisha hijab!? Yaani ni dume jike,lol ptuu! FF kazi unayoifanya humu JF ni ngumu na huwezi shinda nguvu ya umma..ptuu!
 
Asante dada Regia kwa thread yako nzuri na kututegulia kitendawili.
kumbe FaizaFoxy ni mwanaume? Sasa ya nini kujivalisha hijab? Yaani ni dume jike,lol ptuu! Kazi unayoifanya humu JF ni ngumu na huwezi shinda nguvu ya umma..ptuu!

Unanchekesha. Hata haya hamuoni? Nyie na mbunge wenu baada ya kudondokea pua Igunga mnakuja kuongolea ishu za Rostam Aziz. Lohhh, nawashangaa sana, halafu ndio mpewe nchi? hivi hajioni kuwa mnatafuta visababu ili ishu muhimu za kwanini mmedondokea pua Igunga hamziongelei. Mmeshaona mlango wa kutokea ni Rostam?

Daaah. Mnanshangaza sana. Hivi mnajiona wa maana na Mbunge, kweli Mbunge, kajiona kaleta topic ya maana sana kuja kuongolea oooh Rostam alikuwa na ushawishi hakufanya hivi hakufanya vile? khaaaaa! hata haya hakuna? huyo ndio kiongozi anaetegemewa? poleni sana.
 
Unasikitisha kwa sababu umerun away from the logic!

Logic, talking about a former MP and what he should have done and you are calling it logic? how will it help you or any Tanzanian? He did not do so what? why cry? Go and do it.
 
Unanchekesha. Hta haya hamuoni? Nyie na mbunge wenu baada ya kudondokea pua Igunga mnakuja kuongolea ishu za Rostam Aziz. Lohhh, nawashangaa sana, halafu ndio mpewe nchi? hivi hajioni kuwa mnatafuta visababu ili ishu muhimu za kwanini mmedondokea pua Igunga hamziongelei. Mmeshaona mlango wa kutokea ni Rostam?

Daaah. Mnanshangaza sana. Hivi mnajiona wa maana na Mbunge, kweli Mbunge, kajiona kaleta topic aya maana sana kuja kuongolea oooh Rostam alikuwa na ushawishi hakufanya hivi hakufanya vile? khaaaaa! hata haya hakuna? huyo ndio kiongozi anaetegemewa? poleni sana.
Da Faiza,
Kama huko ni kudondoka basi Chadema imedondokea pazuri. Kutoka zero hadi asilimia 44% ya kura za Igunga si haba eti. Kumbuka Rostum alikuwa akishinda kwa kishindo kila mara. Sasa leo kuona kura zenu zinapukutika mnajiliwaza kuwa heri hata ushindi wa kura moja tu. Ushindi wa kishindo umekuwa historia. Kama tungekuwa darasani na tunapima umaarufu wa CCM na Chadema ni dhahiri chati ya CCM inashuka wakati ile ya Chadema inapaa.
 
Nakushangaa sana unaposema 'kawaulize wananchi wa Igunga' na wakati kila kitu kinaonekana wazi!! Kafanya nini la maana zaidi ya kujipalilia ufisadi wake. Rostam ni mnafiki na hafai kabisa kwa wananchi na kwa kudhihirisha hilo ndo kajikinga kwenu magamba wenzake na kawashika masikio kwelikweli kiasi kwa hata pale aliponyea nyie mnalamba tu!

Rostam ananhusu nini baada ya nyinyi kudodondokea pua Igunga? Yeye mmeshaona hajafanya, nyinyi mmefanya nini? hata Ubunge mmeukosa. Tuonesheni huko mklikokuwa na viti mnafanya nini sio fulani (ambae hayuko) hakufanya nini. Ukiuliza watu waliokuwepo na hawapo hawajafanya nini, uanze na kina Nyerere na ujiulize kwa nini hawakuyafanya yote huko na ndio waliokaa kwa muda mrefu zaidi? Na wabunge waliokuwepo kabla ya Rostam walifanya nini? wacheni hizo, tunatazama ambacho hakijafanyika, tunakifanya! sio kuja hapa kusema ooohhh "hasameheki" wewe Mungu? au nani aliokupa cheo cha kusamehe na kutokusamehe? wacheni upupu huo, kueni wabunifu, siasa za majitaka hazijengi zinabomoa kila kukicha.
 
Asante dada Regia kwa thread yako nzuri na kututegulia kitendawili.
kumbe FaizaFoxy ni mwanaume? Sasa ya nini kujivalisha hijab? Yaani ni dume jike,lol ptuu! Kazi unayoifanya humu JF ni ngumu na huwezi shinda nguvu ya umma..ptuu!

Ulitaka nikabandike nywele za kihindi kama hiyo picha hapo juu? tena nasikia za maiti ndio wanavaa watu wenye mshiko.
 
Da Faiza,
Kama huko ni kudondoka basi Chadema imedondokea pazuri. Kutoka zero hadi asilimia 44% ya kura za Igunga si haba eti. Kumbuka Rostum alikuwa akishinda kwa kishindo kila mara. Sasa leo kuona kura zenu zinapukutika mnajiliwaza kuwa heri hata ushindi wa kura moja tu. Ushindi wa kishindo umekuwa historia. Kama tungekuwa darasani na tunapima umaarufu wa CCM na Chadema ni dhahiri chati ya CCM inashuka wakati ile ya Chadema inapaa.

Unanchekesha! wala usijifurahishe kwa hilo, hakuna kudondoka pazuri. Huko ni kujipa moyo. Kushindwa ni kushindwa tu. Rostam inamuhusu nini? Watu wanapigania kura moja ya ushindi. Halafu huko "future" watajuana, mla mla leo mla kesho kala nini?
 
Unanchekesha! wala usijifurahishe kwa hilo, hakuna kudondoka pazuri. Huko ni kujipa moyo. Kushindwa ni kushindwa tu. Rostam inamuhusu nini? Watu wanapigania kura moja ya ushindi. Halafu huko "future" watajuana, mla mla leo mla kesho kala nini?
Bibie utacheka sana mwaka huu. Chadema imedondokea pazuri. Kuna watu walikuwa wanasema Chadema ni chama cha mjini. Sasa hata Igunga kipo.
 
Hivi Rostam si ndiye yule aliyeanzisha Hoja ya Duo Citizenship?

Dada Regia umesema kweli,kama mtu umefika igunga hali inasikitisha sana,hao wanaotembea uchi ni wataturu na wanalalia ngozi,nilishawahi kushuhudia mama mjamzito anaumwa amebebwa kwenye tela linalokokotwa na ng'ombe pale simbo.Kiufupi hali ya igunga ni mbaya na zaidi inachangiwa na ukosefu wa elimu
 
Logic, talking about a former MP and what he should have done and you are calling it logic? how will it help you or any Tanzanian? He did not do so what? why cry? Go and do it.

Na wewe cha ubishi Siasa na history haviachani. Kwa hiyo hata baada ya miaka 20 RA atakuwa kwenye historia na Siasa za Igunga iwe ni kwa mazuri na mabaya . Si unaona kuna thread mzee wetu mmoja anayekumbusha historia ilifyofichwa na nyerere .
 

Na wewe cha ubishi Siasa na history haviachani. Kwa hiyo hata baada ya miaka 20 RA atakuwa kwenye historia na Siasa za Igunga iwe ni kwa mazuri na mabaya . Si unaona kuna thread mzee wetu mmoja anayekumbusha historia ilifyofichwa na nyerere .

Mara baada ya kurudi mkiwa majeruhi mnaongelea history? makubwa haya! Au King Maker ndio aliwanyima ushindi? mnhhhhh! mie naona hijab ndio iliwanyima ushindi, maana mpaka Mbunge kaitaja hapo juu, mkiiona mnaweweseka, muiweke hijab kwenye historia yenu, si Rostam ambae kwa sasa hayupo tena kwenye siasa uchwara.
 
Bibie utacheka sana mwaka huu. Chadema imedondokea pazuri. Kuna watu walikuwa wanasema Chadema ni chama cha mjini. Sasa hata Igunga kipo.

Kipo Tanzania nzima, hakuna ubishi, lakini Igunga ndio kwanza Mbunge wa CCM kachukuwa kiti, ngojeni mjaribu tena baadae. Kwa sasa mnhhh mnhhh.
 
Mtu mzima ni yule ambaye yuko eligible kupiga kura.
Ok,basi kwenye kubadilika kati ya hao watu wazima,kuna vijana ambao wa kuanzia miaka 18 maybe hadi 30 or 35.Hao huwezi kuwajumuisha na hao watu wazima wasiotaka kubadilika.Ndio maana nikakuuliza kama umri ulikuwa kigezo zaidi tu ya utu uzima.Vijana ni more likely ku embrace new ideas na kutaka mabadiliko ama maendeleo.Hapo mwanzoni kabla ya jibu lako hili, niliwachukulia hao watu wazima wasiotaka kubadilika kama watu wazima haswa na siyo watu wazima wenye miaka 18 ambayo ni halali kupiga kura.
Kwa ujumla elimu ingewasaidia zaidi wananchi wote kwa ujumla wao.Kwani wakijuwa haki zao na kuijuwa connection kati ya well being yao ie umasikini, na uamuzi wao kwenye sanduku la kura.Kwamba wanaweza kuleta mabadiliko ie kuondokana na umasikini kwa kutumia sanduku la kura.Basi watabadilika.Hiyo connection ikishawaingia kwenye akili yao basi hakuna tabu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kama nilivo sema,hakuna chama cha siasa kitafanya yaliyo tofauti na yale yanayo fanywa na ccm.
Kama ni ufisadi utakuja kwa kasi ya ajabu,...

Sisi tulio zaliwa enzi za utawala wa Mwinyi tunaamini kwamba bora kumchagua tajiri atakula
kidogo,...kuliko kumchagua maskini asie kuwa na chochote maana ataanza kujishibisha mwenyewe
ndio aanze kufikiria wananchi wake.


Kama walivo sema Igunga walijiandikisha zaidi ya 170 elf na wakajitokeza kama 53elf hivi.
Hao 120 elf ni wale wasio kuwa na imani na chama chochote cha siasa,na sio wanachama wa chama chochote
kile,.....so suluhisho hapo ni kuruhusu mgombea binafsi,labda angepata kura za hawa wote.

Vyama vya siasa ni vitega uchumi,...atakae bisha EITHER NI MNAFIKI AU HAJUI KWAMBA HUO NDIO UKWELI.

Kweli sina shaka na umri wako binti!
Kwamba huyo mgombea binafsi yeye ni malaika. Na kwamba mtu akishakuwa na kigezo hicho basi hawezi kufanya hayo niliyo-highlight kwa kijani.
Get life binti!
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
Dada Regia, hii ndio hali halisi ya watu wetu huko vijijini! na ili tuweze kuyaondoa haya ni kuendelea kuwahamasisha wananchi wengi wa vijijini wafunguke na kujitambua ili wadai haki yao.
 
Nimeshukuru kuona thread hii imeendelea vizuri tangu jana ukiondoa wavurugaji wachache. Nilitaka kufahamu Dada Regia kama alipata nafasi kuongea na wadau wengine wa maendeleo ya Igunga kama DED, DC, MADIWANI, WENYEVITI wa SERIKALI za vijiji na hatimaye wanaIgunga wenyewe. Mbunge peke yake asingeweza kuibadili Igunga. Mtu kama DED anapelekewa pesa nyingi tu za miradi ya maendeleo. Kwa kukosa USIMAMIZI mapesa haya wanagawana na kuyatafuna kuanzia kwa Waziri wa TAMISEMI, Naibu wake, Katibu wa Wizara, Wakurugenzi wa wizara,.....
Mfumo huu wa kugawana mapesa haya katika nchi yetu upo wizara nyingi tu. Matokeo yake hakuna wa kumsimamia mwingine. Haya ninayoyaandika hapa yapo na yanafanyika kwa usiri mkubwa tu.
Ndio maana utakuta barabara, madaraja, majengo ya madarasa, nyumba za walimu vinajengwa kwa viwango duni sana au havijengwi kabisa. Bila ya kuwa na sheria kama zile za CHINA hapa tulipo hatutatoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom