Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Unajua chadema ni mabingwa waku exagerate vitu, km hali ndio iko hivyo kwa nn wananchi wameichagua CCM na kuwaacha nyie km kweli hayo mliyokuwa mnayasema ni ya kweli ? . Dada maelezo yako yanatia mashaka isije kuwa watafuta umaarufu tu wa kisiasa humu ndani km kawaida yenu
Mpumbavu huwa hafundishiki, nakushangaa kujiita 'Genius Brain' ni bora ungejiita 'dull brain'
 
We lovu you dada Regia lol!!!

Jamaa alikuwa hana huruma na watanzania,alitumia ubunge kama nafasi ya kupiga deal tu....Lakini upande wa pili dada Regia,chama chetu kimejipanga vp kukabiliana na mazingira ya namna hii....maana CCM ilitumia ujinga na umaskini huu kutushinda.Nasikia japo sija-prove hili kuna mama/bibi mmoja alienda kupiga kura kwenye kituo fulani akasema "Nataka kile chama cha kwa Nyerere" sasa kwa mazingira haya sidhani kama ni rahisi kupenyeza sera zetu kirahisi...Chama kimejipanga vp?

Lakini kuna mawazo ya kuchangia chama na mambo kama hayo kwa sisi wana-JF hili sijaona comments za kwenu kama makamanda wetu,mnaonaje? na wazo la kuanzisha kitu kama kuchangia kupitia M-PESA,TIGO-PESA nk...nilikuwa Arusha wiki moja iliyopita watu wanapenda sana kuchangia ukombozi wa taifa hili,kuna tajiri mmoja nilimsikia akisema,yeye atatoa gari lake 2015 au hata before 2015 kutembea Arusha nzima kuelezea ushenzi wa CCM na viongozi wake...Tupeni muongozo dada.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Chadema,Mungu mbariki dada Regia...
 
Mkuu mfano wako ni mzuri lakini ni irrelevant hapa.Wananchi wa Tanzania siyo watu wazima peke yao.Unless utuambie mtu mzima ni nani kwenye definition yako?Unapozungumzia Tz unazungumzia pia na vijana.Kama na wao umewaweka kwenye kundi la "Utu uzima" basi niwie radhi.Kwenye hiyo research ya coaching factors za umri ziliwekwa?Given the fact that umetaja "utu uzima" kama kigezo.

Mtu mzima ni yule ambaye yuko eligible kupiga kura.
 
Napenda kueleza kidogo kuhusu Igunga, mimi siyo Magamba wala swahiba wa Rostam ila penye ukweli nitasema. Nikiwa mmoja wa wanaIGUNGA, mzaliwa wa kijiji cha Ndembezi. Suala la elimu Rostamu amejitahidi sana, shule nyingi za msingi zimeanzishwa, na baadhi ya vijiji kuwa na shule mbili hadi tatu katika kijiji kimoja mfano Vijiji vya Ndembezi, Nkinga na Mwisi. Kwa sekondari, wakati Rostam anaingia kulikuwa na sekondari tatu wilayani, moja St.Peters Alban Ussongo ya misheni na mbili Nanga ss na Igunga ss za serikali, leo kuna zaidi ya Sekondari 15, zikiwemo za kata na binafsi 3. Ni kweli wananchi hasa wa jamii ya wafugaji hasa wasukuma na wataturu hawajui kusoma kutokana na kuendekeza mifugo zaidi. Suala la maji, nilipokuwa mdogo kulikuwa na mabomba lakini yalikufa, Rostamu kachimbisha visima vingi sana na mabwawa pia kuna vijiji vingine kuna miradi ya maji inaendelea na wananchi wanapata maji mfano Ndembezi. Suala la barabara karibu vijiji vyote vina barabara zinazopitika mwaka mzima, tatizo la uharibifu wa barabara ni kubwa kutokana na kutumiwa na mifugo. Kuhusu mawasiliano kata karibu zote zina mawasiliano ya simu hasa Airtel na Vodacom. Kuhusu kabila la kutembea uchi hakuna, wako jamii ya wafugaji wataturu wanafanana na wamasai mila zao, labda watoto wao chini ya miaka 10 ndio hukaa uchi. Suala la Tv siwezi kulisemea sana ila kuhusu umeme nadhani ni mojawapo ya wilaya zenye coverage kubwa, kuanzia Simbo, Nkinga, Ndembezi, Ziba, Iborogelo, Nyandekwa, Nanga, mpaka Igunga kuna Umeme. Rostamu alikuwa mbunge aliyetakiwa kuipigia kelele serikali kuleta maendeleo, mengi mazuri kafanya. Simpendi Rostamu kwa ufisadi wake lakini namkubali kwa yale aliyochangia Igunga. Nawasilisha
 
Mkuu sikubaliani kabisa unapodai eti hao wananchi hawataki kubadilika.At least kwasababu uchaguzi umeshakamilika na matokeo ya idadi za kura umeyaona.Then tatizo haliwezi kuwa eti hawataki kubadilika.Mkuu weka maanani pia namba ya wale ambao walinyimwa fursa ya kupiga kura,na wale ambao walishindwa kwenda kupiga kura kwa sababu mbali mbali siwezi kuzitaja hapa zote.Tizama idadi ya wananchi walioipigia ccm kura uchaguzi huu na zile zilizopita.Its just a matter of time wananchi watafunguka macho kwa wingi zaidi.Wewe umepewa hadi ukweli kuwa hata vijana wadogo hawajui kusoma.Sasa hapo ndipo penye shida hata kama ni kweli wamekataa kubadilika,ukweli ni kwamba uelewa wao ni mdogo na solution si kusema tu hawataki kubadilika.Bali kuwasaidia kwa kuwapa elimu na pia ile ya uraia.Na pia kwa sababu ya uelewa wao mdogo,ndio maana bado idadi ya wapiga kura ni ndogo sana kulinganisha na population kwa ujumla.Kuhusiana na wabunge wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa sina comment kwa sasa.Pia sikubaliana na generalisation yako ambayo intention yake ni ku neutralise hoja.Hata kama tatizo ni la kitaifa na si la RA kama unavyodai.Bado RA ndiyo ametokea kuoneka onekana kama Fisadi papa lao.From sijui Kagoda to EPA to Richmond yumo.Sasa at least angewaonea huruma wananchi masikini.Kuongoza TZ inahitaji huruma nilishasema mara nyingi tu hapo nyuma.

There you go my friend. Mtu yupo radhi kupingia mtu kura kwa sababu ya ucheshi wake. Huyo utambadilishaje? Utamfunguaje macho?

Tatu sisi wana Igunga tunampenda sana Rostam kwa ucheshi wake ambao unaleta amani utulivu; hatupendi viongozi wanaotoka kwenye vyama vya kumwagiana Tindikali na kuvua watu hijabu, hivyo ROSTAM hata kama angegombea tena katika uchaguzi ulioisha juzi bado tungempa asilimia 80 ya kura zote na huyo mgombea wenu asingepata hata asilimia 5.
 
Zipo nyingi Mkuu,nitazitaja chache

1. Vituo vya kupitia kura vimewekwa mbali mno,mtu anatembea hadi 13kms kufuata kupiga kura.
2. Wengine unakuta familia nzima hawajui kusoma na kuandika hivyo anaona tabu kutafuta msaada wa kusaidiwa kupiga kura
3. Wapo wengi waliotoa malalamiko ya kupoteza shahada zao na hawakupata msaada.
4. Wapo waliuza shahada zao sababu ya fedha ndogo
5. Siku ile ya kupiga kura kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na shughuli nyingine kama vile minada hivyo wengine wala na bora wajitafutie chochote kuliko kwenda kupiga kura.
6. Si wote waliojiandikisha lengo lao lilikuwa ni kupiga kura,wengi walijiandikisha kwa lengo la kuwa na kitambulisho kitakachowasadia katika shughuli zao nyingine,hivyo kupiga kura kwao ni subsidiary kwakuwa hajui faida wala hasara za kupiga kura
.
Sababu ya 5 na ya 6,ambazo ndizo sababu kubwa hapa, zinawawakilisha hawa watu, hivyo wanaona badala ya kupoteza muda wa kwenda kupiga kura ni heri waendelee na shughuli zao za kila siku.

.. kutopiga kura inatuonyesha kwamba hawana imani na siasa zetu, hawana imani ya uchaguzi wala wagombea wake kwa sababu wanajua hapatakuwepo na mabadiliko yoyote. .
 
Zipo nyingi Mkuu,nitazitaja chache

1. Vituo vya kupitia kura vimewekwa mbali mno,mtu anatembea hadi 13kms kufuata kupiga kura.
2. Wengine unakuta familia nzima hawajui kusoma na kuandika hivyo anaona tabu kutafuta msaada wa kusaidiwa kupiga kura
3. Wapo wengi waliotoa malalamiko ya kupoteza shahada zao na hawakupata msaada.
4. Wapo waliuza shahada zao sababu ya fedha ndogo
5. Siku ile ya kupiga kura kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na shughuli nyingine kama vile minada hivyo wengine wala na bora wajitafutie chochote kuliko kwenda kupiga kura.
6. Si wote waliojiandikisha lengo lao lilikuwa ni kupiga kura,wengi walijiandikisha kwa lengo la kuwa na kitambulisho kitakachowasadia katika shughuli zao nyingine,hivyo kupiga kura kwao ni subsidiary kwakuwa hajui faida wala hasara za kupiga kura.

Mheshimiwa kama mtu anataka mabadiliko yuko tayari hata kupoteza maisha yake sembuse kutembea kilomita 13 kupiga kura. Lakini thread yako kwa ujumla inaleta maswali probably Chadema hamjui hali halisi ya vijijini. Chenge nae akijivua gamba mtaenda kufanya uchaguzi jimboni kwake na mtakuta hali ni ile ile kama mliyoikuta Igunga. Watembeleeni wanavijiji huko vijijini muone jinsi wanavyoishi.
 
wanasiasa bana! unaonaje ukitupatia kwanza data za igunga kabla na baada ya rostam azizi ili tuende sambamba maana unaponda as if rostam azizi ndo mwanzilishi wa igunga na hajafanya chochote katika umri wao wote. si vibaya pia ukitupatia data katika hayo uliyoorodhesha hapo juu hasa katika jimbo lako kabla na baada ya ubunge wako maana usije ukawa unatafuta umaarufu kwa kazi ambazo wamefanya watangulizi wako. kupiga kelele tu bungeni bila vitendo haitusaidii sisi wapiga kura sababu hatukuwatuma kwenda kupiga kelele tu huko. maana unaweza ukawa ukipigia kelele vitu ambavyo ki uhalisia haviwezekani kwa kutaka wanachi wako wakusikie ukiongea
 
Sasa kama hayo ni kweli kabisa, kulikoni wana Igunga kuichagua CCM tena? Au kura zimechakachuliwa? Si waougomee basi uamuzi wa NEC?
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

Kama sikosei wananchi wa Igunga walimpenda kwa sababu alitoa CHAKULA! haya unayosema ukienda Igunga watakushushua mpaka uchanganyikiwe!
 
Hizo picha za Igunga ni sawa tu na maeneo mengine ya wilaya kama Ngara, Misenyi, Chato na Karagwe mkoani Kagera. Tanzania nzima hatuchekani jamani. Ukitoa makao makuu ya mikoa, wilaya zetu ni choka mbaya. Naweza kusema Igunga hakuna shule yenye jengo moja tu lenye chumba kimoja tena la nyasi linalotumika kwa wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba lakini hapa mkoani Kagera ninaifahamu shule ya namna hiyo kama unataka picha niPM.
 
Bibie,hilo la sita ulloandika hapo ndilo linameza habari nyingine zote.. Kama watu wamejiandikisha kupiga kura ili wapate vitambulisho vya mambo mengine ina maana wamechoka na upigaji kura kwa sababu hawana imani na siasa zetu na sii kwamba hawajui faida na hasara zake - wanajua hakuna FAIDA! Huu ndio ukweli, haya maswala la gulio na kadhalika hayawezi kuwa na maana kwao kama wanajua kutakuwepo na mabadiliko wakiwachagua wabunge wao iwe CCM au Chadema tena kwa kumsimamisha mbunge ambaye maisha yake ni hohehahe kama wao. Akili zao zinawatuma kwamba wanamjengea maisha bora mtu huyo mbunge na sii wao (Of which it's true)..Yale yale ya kutoaminiana.

Kwa hiyo umeona umuhimu wa kitambulisho, kitambulisho kinaweza kubadilisha maisha yao ktk sehemu zinginezo na sii kupiga kura na ndiko ukweli ulikosimama. Acha Igunga, mimi nina hakika majority ya Watanzania wamejiandikisha kupiga kura kwa sababu hii wapate kitambulisho cha kupiga kura kama ID ya makazi na uraia wao na umuhimu wake wanaujua wao, lakini basi nyie Wabunge wetu mnapinga kutolewa kwa vitambulisho vya Kitaifa na kuviona havina maana wakati mahitaji yake ni makubwa sana kuliko maelezo kwa raia kina sisi tusokuwa na majina.

Kama nilivo sema,hakuna chama cha siasa kitafanya yaliyo tofauti na yale yanayo fanywa na ccm.
Kama ni ufisadi utakuja kwa kasi ya ajabu,...

Sisi tulio zaliwa enzi za utawala wa Mwinyi tunaamini kwamba bora kumchagua tajiri atakula
kidogo,...kuliko kumchagua maskini asie kuwa na chochote maana ataanza kujishibisha mwenyewe
ndio aanze kufikiria wananchi wake.

Kama walivo sema Igunga walijiandikisha zaidi ya 170 elf na wakajitokeza kama 53elf hivi.
Hao 120 elf ni wale wasio kuwa na imani na chama chochote cha siasa,na sio wanachama wa chama chochote
kile,.....so suluhisho hapo ni kuruhusu mgombea binafsi,labda angepata kura za hawa wote.

Vyama vya siasa ni vitega uchumi,...atakae bisha EITHER NI MNAFIKI AU HAJUI KWAMBA HUO NDIO UKWELI.
 
Mkuu Asante!CHADEMA ina njia mbalimbali za kuchangisha fedha kwaajili ya kusaidia operesheni za chama.Nitaanzaisha hapa sredi next tine nakuomba uongozi wa JF uweke sticky ili kila mmoja a pate fursa ya kujisomea na kuchangia kama atapenda.
Kuhusu huyo bibi aliyeenda kupiga kura akiwa hajui anamchagua nani au chama gani ni kweli yeye alipoulizwa alisema anataka kuchagua chama Cha Nyerere!

QUOTE=only83;2600065]We lovu you dada Regia lol!!!

Jamaa alikuwa hana huruma na watanzania,alitumia ubunge kama nafasi ya kupiga deal tu....Lakini upande wa pili dada Regia,chama chetu kimejipanga vp kukabiliana na mazingira ya namna hii....maana CCM ilitumia ujinga na umaskini huu kutushinda.Nasikia japo sija-prove hili kuna mama/bibi mmoja alienda kupiga kura kwenye kituo fulani akasema "Nataka kile chama cha kwa Nyerere" sasa kwa mazingira haya sidhani kama ni rahisi kupenyeza sera zetu kirahisi...Chama kimejipanga vp?

Lakini kuna mawazo ya kuchangia chama na mambo kama hayo kwa sisi wana-JF hili sijaona comments za kwenu kama makamanda wetu,mnaonaje? na wazo la kuanzisha kitu kama kuchangia kupitia M-PESA,TIGO-PESA nk...nilikuwa Arusha wiki moja iliyopita watu wanapenda sana kuchangia ukombozi wa taifa hili,kuna tajiri mmoja nilimsikia akisema,yeye atatoa gari lake 2015 au hata before 2015 kutembea Arusha nzima kuelezea ushenzi wa CCM na viongozi wake...Tupeni muongozo dada.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Chadema,Mungu mbariki dada Regia...
[/QUOTE]
 
Hizo picha za Igunga ni sawa tu na maeneo mengine ya wilaya kama Ngara, Misenyi, Chato na Karagwe mkoani Kagera. Tanzania nzima hatuchekani jamani. Ukitoa makao makuu ya mikoa, wilaya zetu ni choka mbaya. Naweza kusema Igunga hakuna shule yenye jengo moja tu lenye chumba kimoja tena la nyasi linalotumika kwa wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba lakini hapa mkoani Kagera ninaifahamu shule ya namna hiyo kama unataka picha niPM.

Wewe umetoa mfano wa mbali sana,...
mimi nawaambia kama wanachuo wa Mlimani (UDSM) wana kaachini
kwanini tushangae watoto wa chekechea kukalia tofali?

Tatizo wana siasa wetu wanajidai wao wa mjini sana,....
kuijua Igunga tu wametumia milioni 400,... mara wengine bilioni 3,...huu ulikua utalii + anasa sio siasa
hizi.....sasa unadhani hadi wanajua kila kona ya nchi watakua wametumia kiasi gani?

Hapo watakua wameifahamu nchi,hawajaanza kupanga "michakato" ya kuokoa hali ya nchi (hela zingine)
Hawajaanza utekelezaji ambao hauta kamilika (Hapo watakuwa wamezeeka na wame tajirika sana) na wata staafu siasa
bila kufanya lolote.
 
Mkuu Asante!CHADEMA ina njia mbalimbali za kuchangisha fedha kwaajili ya kusaidia operesheni za chama.Nitaanzaisha hapa sredi next tine nakuomba uongozi wa JF uweke sticky ili kila mmoja a pate fursa ya kujisomea na kuchangia kama atapenda.
Kuhusu huyo bibi aliyeenda kupiga kura akiwa hajui anamchagua nani au chama gani ni kweli yeye alipoulizwa alisema anataka kuchagua chama Cha Nyerere!

QUOTE=only83;2600065]

We lovu you dada Regia lol!!!

Jamaa alikuwa hana huruma na watanzania,alitumia ubunge kama nafasi ya kupiga deal tu....Lakini upande wa pili dada Regia,chama chetu kimejipanga vp kukabiliana na mazingira ya namna hii....maana CCM ilitumia ujinga na umaskini huu kutushinda.Nasikia japo sija-prove hili kuna mama/bibi mmoja alienda kupiga kura kwenye kituo fulani akasema "Nataka kile chama cha kwa Nyerere" sasa kwa mazingira haya sidhani kama ni rahisi kupenyeza sera zetu kirahisi...Chama kimejipanga vp?

Lakini kuna mawazo ya kuchangia chama na mambo kama hayo kwa sisi wana-JF hili sijaona comments za kwenu kama makamanda wetu,mnaonaje? na wazo la kuanzisha kitu kama kuchangia kupitia M-PESA,TIGO-PESA nk...nilikuwa Arusha wiki moja iliyopita watu wanapenda sana kuchangia ukombozi wa taifa hili,kuna tajiri mmoja nilimsikia akisema,yeye atatoa gari lake 2015 au hata before 2015 kutembea Arusha nzima kuelezea ushenzi wa CCM na viongozi wake...Tupeni muongozo dada.

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Chadema,Mungu mbariki dada Regia...
[/QUOTE]

Thanx for your concern dadaa...plz this should be taken seriously sister tuna uchungu sana na Taifa hili...umaskini wetu tukiuweka kwa pamoja ni utajiri tosha kuliko hata wa Rostam na chama chake....
 
Huyu jamaa hata ukimlaumu haisaidii sana,
Kwanza amepitia chaguzi za 1994, 1995, 2000,2005 & 2010 na wananchi wamempa kura,
Hapa bana wa kuwalaumu ni wana-Igunga wenyewe.
Hawa jamaa utafikiri walilishwa limbwata na huyu tapeli,
Cha ajabu anawawekea mtu na bado wanamchagua.
Hawa wana Igunga hawasaidiki kabisa,
Mungu aliamua kuwasaidia kuwakomboa but inawezekana wameshazoea shida wakaamua warudishe matatizo,
Hakuna haja ya kuwasemea na shauri zao wenyewe na huyo dalali wao,
Wacha awadalalie hata kidogo walichonacho!!
Hapana, wanaigunga zaidi ya 25,000 wameupigia kura upinzani. Hiyo ni dalili tosha kwamba wanataka mabadiliko. Angalieni nguvu kubwa iliyotumiwa na chama tawala nayo pia ni dalili wazi kwamba wanaigunga wanataka mabadiliko.
 
Kweli watanzania we have a long way to go, kwa hali hii bado wanawachagua hao wasiowajali. EEe Mungu tuamshe kwenye lindi hili la upofu na usingizi.
 
Dada Regia kama hayo mambo umeyaona Igunga tu na huamini kama yapo sehemu zingine basi inaonekana hujaizungukia Tanzania, Jaribu kupita mikoa yote japo wilaya mbili tu kwa kila mkoa na na tarafa mbili kwa kila wilaya utakayofika, na upitie kata mbili kwa kila tarafa utakayofika na mwisho kabisa vijiji viwili kwa kila kata halafu baadaye uje useme kama Igunga ina tofauti na sehemu zingine.
Wakati mwingine uwe unaisoma thread na kuielewa ndipo ujibu au utoe mchango wako.
 
Wabunge kuweni makini, kama tutawapima kwa mtindo huu mbona wote hamtarudi Bungenin2015!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom