makoye2009
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,638
- 1,219
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!
Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.
Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;
1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo
2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama
3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20
4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.
5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.
6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.
7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.
8. Zipo Kata ambazo hazina mawasiliano ya simu
9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.
10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu
11. Na mengine mengi madogo madogo.
Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo
1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?
Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!
Nawasilisha!
Dada Regia Mtema,
Akhasante sana kwa taarifa hizi zenye kuisikitisha sana toka jimbo la Igunga. Napenda kuchangia mada hii kama ifuatavyo na hasa nikilenga kwenye maeneo yenye red colour:
Nianze kwa kusema kuwa to me this is unbelievable! Naona kama vile naota. Kwamba kuna hali mbaya namna hii kwa Wanaigunga, hali ambayo inaweza kukutoa machozi unapoisoma na hasa ukizingatia kuwa MWAKA HUU NI JUBILEI YA MIAKA 50 YA UHURU!
Wanaigunga hawahawa ndiyo waliolia na kuzimia wakti Rostam Aziz anatangaza kujiuzulu Ubunge na nyazifa nyingine ndani ya Chama cha Magamba. Kama kweli hali ndivo ilivo hawa wana Igunga walikuwa wanalilia nini na kuzimia kwa kihoro???Siamini hata kidogo. Yawezekana wale watu waliolia na kuzimia siku ya RA akitangaza kuachana na siasa UCHWARA ilikuwa ni MAIGIZO(Kwamba alitafuta watu akawalipa pesa ili wajifanye kulia na kuzimia). Huu ulikuwa mpango mkakati uliokuwa umaandaliwa barabara na RA mwenyewe!
Labda sasa nianze kuchambua dondoo moja baada ya nyingine kama zilivoainishwa na dada Regia:
- ELIMU:Juzi siku ya kupiga kura kuna watu WA IGUNGA WALIONEKANA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA BAADA YA KUSHINDWA KUPIGA KURA KWA VILE HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA. Ilibidi wapate msaada wa wasimamizi ili waweze kupiga kura.Huu ni ukweli ambao hata CCM wanajua hili.Kwamba Igunga iko nyuma kielimu kwa asilimia kubwa sana. Lakini bado CCM wameng'ang'ania jimbo hili kwa maksudi ili waendelee kuwanyanyasa watu wa Igunga. Kwamba CCM iko tayari kuwaona watu wa Igunga wakiwa WAJINGA ili iweze kuwatawala kiurahisi!!!Hii linafanywa maksudi na Serikali ya CCM! Mtu atajiuliza hapa kwanini CCM chini ya RA kwa miaka yote hii hawajaweza kujenga shule za kata vijijini kwa ajili ya Wanaigunga? Jibu liko wazi:SIASA UCHWARA
- MAJI: Swala la MAJI lilijitokeza kwenye harakati za kampeni na CCM wakatumia TATIZO LA MAJI kuwarubuni wana-Igunga kwa kufunga maji Igunga mjini na kuyaelekeza vijijini kama Rushwa. Kwa hiyo CCM wanageuza matatizo ya Wananchi na Wanaigunga KAMA MTAJI WA KISIASA.
- AFYA : Miaka 50 ya uhuru bado wanaigunga hawana Zahanati za uhakika.Zahanati zilizopo ni chakavu,hazina madaktari,hazina manesi,hazina madawa,n.k. CCM wametumia mabilioni ya pesa kulipata jimbo hili lenye WATU MASKINI.FUKARA,WAJINGA na WAGONJWA badala ya kuelekeza hayo mabilioni ili kuwakomboa wana-Igunga
- MIUNDO MBINU: CCM kwa miaka yote ya RA (17 years) plus na ya CCM/TANU miaka ya 1960s jumla miaka 50 hawajweza kuunganisha barabara za Igunga angalao kwa kiwango cha changarawe achilia mbali lami ambayo ni ndoto kwa wana-Igunga. Bado CCM wametumia mtaji wa ukosefu wa miundo mbinu kama barabara na madaraja kujipatia kura. Tumeona Waziri Magufuli akienda kuwatapeli Wana-igunga kwamba ATALIJENGA DARAJA LA MBUTU haraka iwezdekanavo. Huu ni uongo wa mchana kweupe. Where was Magufuli and his Party in 50 years to construct the same???SIASA UCHWARA!
- MAWASILIANO(TV na SIMU): Ni aibu kwa RA na CCM yake kwa kushindwa kuwapatia Mawasiliano ya uhakika wana Igunga.Rostam Azizi tunajua ana-share(HISA) kwenye Kampuni ya Simu za mikononi ianyoitwa VODACOM. RA alikuwa na uwezo wa kujenga hata BTS 10 kwa ajili ya wanaigunga pekee. RA alikuwa na uwezo wa kuwanunulia Wanakijiji wa kila kijiji au kata TV set moja na kuwawekea umeme wa Jua(Solar Power) ili waweze kufuatilia taarifa za habari na Bunge linapokuwa Dodoma kwa wakti wote! Lakini RA hakufanya hayo. Hii ni maksudi ili kutumia ujinga wa wanaigunga kuendelea kuwatawala. SIASA UCHWARA!
- VYOO : Miaka 50 ya Uhuru bado Wana-Igunga wanajisaidia porini kweli??? This is very shameful for CCM and all its organs. Je,hii wilaya Igunga haina Bwana Afya wa Wilaya?Je, RA alishindwa kwa miaka yote 17 aliyokaa pale ofisi ya Mbunge alishindwa kuwaelimisha wana-igunga juu ya umuhimu wa vyoo vya shimo?? SIASA UCHWARA!
- KUTEMBEA UCHI: If at all there are people in ths country still going NAKED this country is under a curse! Hawa watu watakuwa wanaishi Tanzania ipi tunayodai imejaa AMANI,UPENDO na MSHIKAMANO? Kweli RA FISADI mwenye pesa lukuki alikuwa hayaoni haya?? Kama anaweza kuwakodishia CCM helikopta 2 za kufanyia kampeni ALISHINDWA NINI KUWANUNULIA WATU HAWA HATA MITUMBA TU achilia mbali NGUO ZA GHARAMA pengine kutoka hata ulaya! Lakini RA hakufanya hivo. SIASA UCHWARA!
Naomba CHADEMA wajipange kutumia udhaifu huu wa CCM na RA kuanza kuleta mabadiliko kwa Wana Igunga. Anzisheni matawi ya CDM huko vijijini na muwatumie viongozi wenu wa mashina/matawi hasa kata mlizoshinda kuwaeleimisha Wana-Igunga umuhimu wa Shule/Elimu,usafi/vyoo, Tekohama/Habari/TV kwa kuwahamasisha wajinunulia solar panels na TV sets ili waweze kupata taarifa za habari. Ikiwezekana CDM kuwanunulia TV sets/Solar panels kama huduma kwa jamii. Naamini hili litaiweka CDM pazuri na hasa ukizingatia kuwa 2015 siyo mbali. Huu utakuwa mtaji saafi sana kwa CDM kwenye Uchaguzi Mkuu 2015.