Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

wajemeni shida hizo ziko kila mahali hata kule karatu. Rostam alikuwa mbunge tu, kazi ya kuondoa kero hizo ni ya serikali.... aghh!

There are too many piss artist that have infiltrated JF RECECTLY and their main job is to divert readers from real issues to their garbagge dumps.Too many readers are falling into their traps. WATCH OUT !!!!!!!!
 
Tatizo lako unaongea sana vita visivyotekelezeka..CHADEMA sio NGO wala Charity Organization kwamba ifanye vitu hivyo.Kwa vijipesa inayopata Kama ruzuku itafanya wapi na kuacha wapi?unataka ianze kuwagawa wapiga kura kwa wale ambao watakuwa hawajasaidiwa na waliosaidiwa?hebu fikiri mara mbili na unipe mifano ya chama gani duniani kinayafanya haya na kikawa salama.

Na hapo unajisuta mwenyewe kwa uliyoyaanika kuhusu ambayo hajayafanya Rostam Igunga, ulifikiri yeye ni NGO au Charity organization?

Hapo ndio unaponifurahisha, "mkuki kwa nguruwe, kwa binaadam mchungu".
 
Tumekuwa na Mwalimu kwa miaka zaidi ya 20 akiwa Rais wa Nchi hii. Mkoa anaotoka kuna barabara moja tu ya lami inayotoka Mwanza- Musoma- Sirari. Kauwanja ka ndege ni ka vumbi na tope kako pale Musoma. Butiama haina chochote cha uhakika. Hili la Mbunge au kiongozi yeyote wa kisiasa kuwaletea maendeleo watu wake nimeliona Kilimanjaro tu.
 
03_11_ghz840karatu.jpg
Hapa ni Karatu, Dr Slaa, hutasameheka
zito.JPG
Hapa ni Kigoma Vijijini Zitto Kabwe hutasameheka
kirombero.jpg
Hapa ni Kirombero Regia hutasameheka
IMG_2841iringa.JPG
Hapa ni Iringa mjini mchungaji Peter Msingwa hutasameheka
 
Halafu mbona unamsifia sana huyo Rostam?
Au ndio yaleyale ya aisifuye mvua,....?
Nina uhakika ukitoka hapa unachofanya ni ku-print tu haya majibishano na kumpelekea huyo jamaa yako, the jioni akaunti benki imenona.
Haiwezekani mtu mzima ukabaki kumtetea mtu tu hivihivi bila kua na ushahidi wa maana!!

Na haiwezekani mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akaja hapa kutoka jimbo walilobwagwa kuja kutuletea habari Rostam hajafanya hivi Rostam hajafanya vile, nnashaka kama ni Mbunge kweli huyu au kabandika tu picha na anatumia ID ya kujipachika, uelewa wa Mbunge mahiri unatakiwa uwe mpana zaidi ya kuongelea mtu ambae hajafanya, labda ni mbunge kwweli lakini wa kupewa na si wa kuchaguliwa na wananchi, hivi kama kachaguliwa kwa kura alikuwa anawaambia nini wananchi kuwa "convince" mpaka wamchaguwe? ngoja nitembelee website ya magwanda nikapate kukidhi kiu yangu.
 
Nachukua fursa hii,kuwashukuru WanaIgunga(Ingawa wengi hawana uwezo wa kuwa kwenye computer kama mimi na wewe)Nawashukuru wote waliotutia moyo,nawashukuru hata wale ambao hawakututia moyo,Nawashukuru sana
Uchaguzi Igunga umeisha,mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu mchakato mzima,kuna mengi sana yalitokea na mimi nimeyashuhudia.Kwanza nikiri kuwa ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika Igunga,kimsingi nilitarijia Igunga yenye neema,na maisha bora,lakini nilikumbana na UFUKARA wa kutisha,na maeneo mengine hata Kiswahili hawajui kwani vijana wadogo sana wa umri chini ya miaka 25 hawajaenda shule,amezaliwa hapo hapo kijijini,amekulia hapo kijijini,na hajui maisha mengine zaidi ya maisha ya shida hapo kijijini.Wanawake wanatembea hadi kilometa 15 kufuata maji ambayo kimsingi si safi wala salama.
Lakini katika lindi kubwa la umaskini wa Igunga,bado serikali ya CCM imatumia mabilioni ya pesa kurudisha jimbo la IGUNGA,ni wazi siasa za Igunga zilikuwa za nguvu kupita kiasi,kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa letu tumeshuhudia uvunjivu,mkubwa wa sheria na katiba.Mimi ni mmojawapo wa waadhirika wakubwa wa siasa za visasi,na matumizi makubwa ya nguvu,nilitekwa na vijana wa green guard,na kunitupa porini,baada ya purukushani kubwa,nikaripoti polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,na mwisho wakanigeuzia kibao et mimi ndio niliwateka,(Aibu kwa jeshi letu la polisi,historia itawahukumu)
Nimeshuhudia dini ikiingilia siasa,na kuwataka waumini wao kutokichagua chama fulani,huu ni moto uliopandikizwa kwa makusudi kabisa,yaani chama tawala kimeishiwa hoja,hata kufikia mahali pa kuwatumia viongozi wa DINI,ili tu kujihakikishia uhalali wa kubaki madarakani,na bila aibu viongozi wetu wastaafu,na wazee wa heshima kwenye hili taifa wakakaa kimya,hakuna hata mmoja aliyekemea tabia hii(Historia itahihukumu ccm kwa kkupandikiza chuki ya dini kwenye taifa letu,aibu kubwa kwa ccm)
.Nimeshuhudia wanawake wakinyanyaswa na polisi eti tu ni wafuasi wa CHADEMA,hakuna hata mmoja aliyekemea,DC aliyevunja sheria yeye kwa kuwa tu ni DC na ni kada wa ccm,akaonekana amedhalilishwa.Nimeshuhudia vijana wengi wakibambikiziwa kesi,kwa kuwa tu ni wafuasi wa CHADEMA,ninapoandika sasa kuna vijana watano walishika gari ya mwenyekiti wa ccm wilaya ya Igunga akigawa hela rushwa,wakaripoti polisi,na baada ya polisi kukagua gari hiyo wakakuta begi lina zaidi ya 21milion,vijana wale wazalendo wakawekwa chini ya ulinzi,eti ni wanyanganyi wanotumia silaha,na bila utu wala heshima kwa binadamu wenzao,polisi wakawapelea Nzega siku ya Ijumaa,hadi Jumatatu walipopelekwa mahakamani na kusomewa shitaka la unyanganyi wa kutumia silaha,Vijana wale walisekwa ndani kwa siku tatu bila chakula wala maji,,u wapi utu wa na usawa wa binadamu?tunaelekea wapi kama taifa?na misingi gani ya taifa tunajenga?
Uchaguzi wa Igunga umekuwa na mengi ya kujifunza,kwa serikali ya ccm,wametumia rasilimali zetu,kwa ajili ya Igunga tu,ni aibu kwa ccm na viongozi wake,lakini kubwa na ambalo sharti wajifunze ni kuwa ,inapofika mahali Chama dola,chenye serikali,rasilimali pesa,rasilimali watu,uongozi kuanzia balozi wa nyumba kumi,kulalamikia CHAMA CHA UPINZANI,eti kinagawa hela,eti kimeingiza makomandoo,na Mungiki,ni wazi kuwa CCM kimepoteza mwelekeo na sasa kinaelekea kwenye anguko kuu.
Ni faraja iliyoje kuona kuwa sasa ukombozi wa pili wa taifa letu u karibu kuliko mategemeo ya wengi,kuna wengine wataona ni maneno ya kujifariji baada ya kushindwa Igunga.Lakini huu ndio ukweli na ccm ni mashahidi katika hili,wanajua nguvu kubwa kiasi gani walitumia kulikomboa Igunga,na bila msaada wa vyombo vya dola wasingeweza.
Uchaguzi umeisha,kuna majeruhi wengi,na ambao kesho ndio wapamabanaji wa ukweli,Jambo moja la msingi ni kwamba hakuna wingi wa silaha,risasi,mabomu,wala vifaa vya kisasa vya kijeshi vinavyoweza kuzuia umma unaotaka mabadiliko,umma uliochoka,umma unaolilia ukombozi,na kwa kadri serikali inavyozidi kuminya uhuru na demokrasia ndivyo umma unavyozidi kuamka na kupigania uhuru wao.Daima tutasonga mbele
 

There are too many piss artist that have infiltrated JF RECECTLY and their main job is to divert readers from real issues to their garbagge dumps.Too many readers are falling into their traps. WATCH OUT !!!!!!!!

"Often we fault in others what we see in ourselves."
 
ni stori ya kusikitisha kwakweli, mwisho wa ccm ukaribu mno.
 
Kwleli amesema mengi
Tuungane naye kwenye thread yake moja kwa moja
Yamenigusa ndo maana nimeandika kidogo tu
Kila la heri
 
Mkuu,nashukuru sana kwa uchambuzi mzuri na wa kina..Hii ndio Tz yenye kila aina ya Neema mwenyezi MUNGU ametujalia.Cha kushangaza kina FaizaFoxy hawayaoni haya kabisa.

Dada Regia,

Thank you for your appreciation.
Hivi dada unafikiri hawayaoni haya? Wanayaona na they know what they're doing for the benefit of the Magamba Party!

Jamani CDM tukaze buti hasa huko vijijini ili mwaka 2015 tuingie Ikulu kwa kufuata nyayo za Michael Satta a.k.a King Cobra,Rais mpya wa Zambia toka chama cha Upinzani cha Democrtatic Party. Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere(RIP) aliwahi kusema,''PLAY YOUR PARTY,IT CAN BE DONE''.

God bless CDM, God bless Tanzania,God bless Africa.
 
"When a true genius appears in this world, you may know him by this sign, that the dunces are all in confederacy against him." --Jonathan Swift

Now I know Rostam Aziz is a genius.
 
Iko siku Mungu ataiweka huru Tanzania na haya yote yataisha
 
ni vyema mapambano haya yakaanza na kila mmoja wetu pale alipo
 
Mkuu Nanyaro Nashukuru kwa taarifa nzuri ya hali ilivyokuwa kule igunga, sasa mimi tena naungana na muuliza swali hapo juu, tunaomba kufahamu chama kinawasaidia vipi hao vijana na wengine wote walioingia katika matatizo kwa kupigania haki, sote tunafahamu kwamba vitisho na mabavu ya ccm siku moja yatazikwa lakini kwa sasa naomba hao vijana wapatiwe msaada husika.
 
acha kutoa povu chundu wewe, eti ccm imetumia mabilioni,, kuna chama kimetumia mkojo? acheni kutupoteze MUDa

Mwenzio kaandika kwa staha nawe pinga kwa staha ukiona uko mtupu kichwani na moyoni ficha upumbavu wako kwa kuka kimya si lazima uandike kila post.Umasikini mkubwa wa Watanzania hausemeki na yeye kasema hapo tunajua sote Nchi ilivyo .Matumizi mabaya ya mali ya Umma na madaraka hata UN wamesema CCM wanatumi vibaya polisi ikiwa ni pamoja nakuua .Now unarusha matusi .Ruka post kama huna hoja wenzio hatuandiki kila post tukiona hatuna cha kusema .Ficha upumbavu tafadhli usitumie masaburi kila mahali hii ni JF.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom