Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
845
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazina mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo:

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.

2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.

3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.

4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga.

Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
 
ezra1504

Member
Nov 2, 2010
55
12
Kwani nani asiyejua kwamba huyu jamaa alikuwa CCM kwa maslahi yake binafsi na si wananchi?

Kwa utajiri alio nao na shughuli zake za biashara, huwezi kupata ht muda wa kupumzika km una manage shughuli zako zote, kwa nini yeye ajifiche nyuma ya kivuli cha chama na ubunge? Wapo matajiri wengi wakubwa km yeye ila hawapo kabisa ktk mambo haya kwani ht muda wa kusimamia biashara zao hawana, e.g. Bakhresa, Manji, Sabodo, Mengi, Mfuruki, etc.

Amemaliza shida zake na hapa anajianaadaa kutokomea!
 
Bushloiaz

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
636
575
Dada Regia umesema kweli,kama mtu umefika igunga hali inasikitisha sana,hao wanaotembea uchi ni wataturu na wanalalia ngozi,nilishawahi kushuhudia mama mjamzito anaumwa amebebwa kwenye tela linalokokotwa na ng'ombe pale simbo.Kiufupi hali ya igunga ni mbaya na zaidi inachangiwa na ukosefu wa elimu
 
Hardwood

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,020
1,021
ROSTAM ni IRANIAN IN DIASPORA!!! Yuko kwa ajili ya maslahi yake binafsi na nchi yake ya IRAN! Binafsi nawahurumia sana WASUKUMA na WANYAMWEZI wa IGUNGA sababu 17 years PARLIAMENTARY TENURE ya ROSTAM imemtajirisha mno yeye binafsi huku akiwaacha wananchi wa IGUNGA wakiwa katika hali mbaya sana.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Kunna aina ya watu wanapenda watu wanatumia vitu na kuna aina watu wanapenda vitu wanatumia vitu hivyo dada unaweza kujua huyu ni aina gani ya mtu
 
echonza

Senior Member
Jun 25, 2009
163
15
Wawakilishi wengi wa wananchi, hasa hao wafanyabiashara walio wengi ndani ya chama tawala ndiyo tabia na kimsingi upinzani umekuwa uliyasema hayo sana.

Nakumbuka Mhe. Zitto akiwa anahutubia wananchi, alitoa historia kubwa kuhusu rasilimali Taifa lilizonazo na akamalizia kwa kusema, haisezekani kwa utajiri huo tukawa tu na maendeleo haya ya leo (yaani ni asilimia mbili tu ya hatua iliyopigwa, ikimanisha nchi imepoteza asilimia 98 ya kuleta maendeleo nchini ndani ya miaka hiyo takribani 50 tangu uhuru). Inashangaza sana hata wao CCM kuwasikia wakiimba wimbo wa maendeleo yamepatikana kwa kiwango kikubwa sana na ilihali ukiuliza utaambiwa viashiria ni majengo ya dhahanati, shule na barabara zisizopitika wakati wa masika na mara nyingine hata tu wakati wa kiaangazi hakuna barabara kabisa.

Kama Serikali ya CCM itaendelea kupima maendeleo kwa viashiria vyao hivyo, hata kama ni miaka 50 mingine ijayo, akina Regia Mtema wengine wataandika matatizo ya kufanana na yale tena pasipo shaka. Nawashauri na kuwaomba chama tawala wakubali kushindwa uongozi na waachie kwa hiari madaraka ifikapo 2015, maana kama itatokea watatolewa kwa hasira za wananchi kupitia masanduku ya kura, basi aibu itakuwa mara kumu zaidi kuliko wangeachia ngazi.

Yaani ukienda vijijini hadi inasikitisha kupita kiwango, maana watu wenyewe wanaoishi huko hata hawajitambui, na ndiyo maana kwao hakuna tatizo kutokuwa na choo, ni bora jua lizame tu ili kesho ifike. Kweli ndiyo maana ya maendeleo hiyo?
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Regia,

Mwenyezi Mungu hawezi kukujalia yote mawili. Kupenda MALI na kupenda WATU na MAENDELEO yao. Rostam anafahamika kwa mapenzi yake kwa MALI. Na mali zenyewe kwa TANZANIA ni lazima UIBE, UFISADI au UDHULUMU watu.

Mwalimu aliliona hili zamani akawaweka kando wenye mali kwenye siasa na UONGOZI wa NCHI yetu. Alipoondoka madarakani tukampuuza. Tukatupilia mbali maadili haya na miiko mingi mingine ya uongozi. Dunia yote ya wastaarabu wenye mali sio viongozi. Jichunguzeni CHADEMA kama tatizo hili mnalo.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,331
Matatizo kama hayo yapo karibia Tanzania nzima kwa aina tofauti tofauti tena hata mijini kuna watu hawana uhakika wa milo miwili kwa siku...

Angalizo: Hakikisheni sehemu ambazo nyie ni wabunge au mna majimbo mnapunguza matatizo ya watu ili na nyie tusije kuacha kuwasamehe, au mkakosa la kuonyesha ikifika 2015
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,466
1,164
Wakuu salaam! Ni matumaini yangu kuwa wote tuko salama.

Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!
Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona.Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20
4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.
5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.
6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.
7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.
8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu
9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.
10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine.Hii ni Kata anayotoka Dr Kafumu
11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1.Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga.Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini,Hana huruma hata kidogo,anajali maslahi yake tu..Bora ulivyojiuzulu,ungejiuzulu na utanzania kabisa,ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

Mkuu kuna thread niliianzisha kuhusu jambo hilo hii hapa, maana nilishtushwa kweli na picha za huko nilizoziona. Unajua sikuzote tulikwa tunaaminishwa kwamba Igunga ni kama paradise. Kiasi kwamba naamini kuna watanzania walikuwa na hamu na wao wapate fisadi kutoka sehemu zao afanye makubwa kama ya rostam hahaha ahahaha ahahahah!!!!!!!!!!! Huyu jamaa ni tapeli la kimataifa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/174772-igunga-makubwa-yaliyofanywa-na-rostam-ni-yepi.html#post25265201.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

Na kama kwenye makubwa ndiyo kuko namna hii basi kazi tunayo!!!!
 
JosM

JF-Expert Member
Oct 11, 2008
676
13
Dah! hii habari imenishtua sana, pia siwezi kushangaa kwani siyo Igunga peke yake ukitembelea baadhi ya majimbo kadhaa utakutana na hali kama hii... Hii hali haikupaswa kuwa sehemu ambayo tajiri mkubwa na kifisadi wa kimataifa Rostam anatoka, nilitegemea wananchi wa huko wangekuwa na maendeleo kwa kiasi flani hivi....

Kwenye hii dunia ya sasa ukiwa hauna elimu ni taabu sana, sasa sipati picha hao vijana na watoto wasiyo jua kusoma wala kuandika hatima yao itakuwa je? Hizi lawama pia serikali inahusika moja kwa moja, maana kwa kushindwa kuwapa wananchi wake haki zao muhimu kama elimu na Afya...

Hii mdio miaka 50 ya uhuru tunajivunia? hakika tumepiga hatua kubwa kwa kufanya wananchi wake mbumbumbu..... Ili tatizo alitoisha kama wananchi wenyewe hatuta amka na kuwapigania wenzitu ambao wanakandamizwa kwa kuto kujua haki zao.

DSC_0491.jpg
 
NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,668
362
wajemeni shida hizo ziko kila mahali hata kule karatu. Rostam alikuwa mbunge tu, kazi ya kuondoa kero hizo ni ya serikali.... aghh!

Kaka huko Karatu ulikosema umefika au unakisia? Hata kama umefika hebu pa-study upya alafu linganisha na hicho anachoandika Regia, au nenda mwenyewe Igunga jaribu kulinganisha hali.....

Pia huko sawa kumuweka mbunge pembeni na maendeleo ya jimbo lake na kusema ni kazi ya serikali...hapa kuna makosa kama sio mapungufu ya kitafsiri. Ukisoma vizuri post ya Regia ameonesha wazi ni namna gani Rosti Hamu kama mbunge angeweza kuhakikisha maendeleo ya jimbo lake (tena hata zaidi ya Karatu kwa wapinzani au majimbo mengine ya CCM) ikiwamo kutumia "influence" yake kwa chama na serikali kutaka miradi isogee jimboni mwake

Ni rahisi tu kusema "THE MAN WAS AFTER HIMSELF" na wala hakuwa na hesabu akilini mwake za wana Igunga na maendeleo yao
 
Shenkalwa

JF-Expert Member
May 3, 2011
580
132
No comment. Kwani nani asiyejua kwamba huyu jamaa alikuwa CCM kwa maslahi yake binafsi na si wananchi? Kwa utajiri alio nao na shughuli zake za biashara, huwezi kupata ht muda wa kupumzika km una manage shughuli zako zote, kwa nini yeye ajifiche nyuma ya kivuli cha chama na ubunge? Wapo matajiri wengi wakubwa km yeye ila hawapo kabisa ktk mambo haya kwani ht muda wa kusimamia biashara zao hawana, e.g. Bakhresa, Manji, Sabodo, Mengi, Mfuruki, etc. Amemaliza shida zake na hapa anajianaadaa kutokomea!

Na zaidi ya hayo, utajiri wake umetokana na njia za wizi tu yeye na mwenzake jidew. EPA, MEREMETA, KAGODA, Nakadhalika, nakadhalika. Msidanganyike sasa hivi hakuna uchaguzi ambao magamba wanashinda kwa halali. Hakuna.
Kinachotumika hapo ni usalama wa taifa. Hawa ndiyo wanaoiumiza nchi hii kwa kuwawezesha hilo genge la magamba kuendelea kuimaliza nchi hii. Yanayofanyika kwenye chaguzi ikiwa ni pamoja na uchaguzi mkuuu uliopita wanayajua na wanashiriki kuyafanya kwa kuwafurahisha mabwana zao lakini iko siku watayakiri hayo kwa midomo yao. Wanashiriki biashara chafu ya kuwafanya watanganyika wawe maskini wa kutupwa miaka nenda miaka rudi. Watu wanahangaika, hospitali hazina madawa, shule hazina madawati/waalimu na waalimu wenyewe wanalia na kusaga meno, wafanyakazi inabidi waishi kwa wizi wizi tu bidhaa zote muhimu zinapanda bei kila kukicha. Maisha yamekuwa magumu kwa kila mlala hoi lakini wakubwa wanapasua anga kila siku. Familia zao zinaishi kama ziko peponi, wanabadilisha magari ya kifahari na kujenga majumba ya kifahari kwa kutumia rasilimali za nchi hii. Wanashindana kwa kuwa na majumba ya kifahari katika nchi za nje na mengine mengi. Nasema usalama wa taifa wana mchango mkubwa katika kufanikisha haya maovu kwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi. Mtakuja kuyakiri haya siku moja kwa midomo yenu. Ndiyo. Hata sasa yanawasumbua katika dhamira zenu. Hamna amani kwa ajili ya kusutwa mioyoni mwenu. Iko siku itakuja mtayasema wenyewe kwamba hadharani kuwa mlifanya hiki na kile. Kama hamtayasema hapa duniani mtayasema mbele za Mungu.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,395
Nilikaa Igunga miaka ya nyuma kidogo. Hii ni wilaya ya wafugaji na mifugo. Watu ambao kwa Tanzania yetu wamekuwa wakithamini mifugo yao kuliko kitu chochote. Ufugaji wenyewe sio wa tija zaidi ya kuoa wake wengi na hivyo kuzaa watoto wengi basi. Ndio ufahari wenyewe. Vijiji vingi vya Igunga vilikuwa na waarabu wengi na maduka yao. Ndio akina Rostam pale Mwisi. Hawa hawakujali mambo ya elimu zaidi ya dini yao ya kiislamu. Rostam kwa hulka yake aliwatumia wanaIgunga kwa kutatua angalau kwa muda tu shida zao ndogondogo kama hela ya kula, karo, visima vichache vya maji,.....
 
TEMPOLALE

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
302
107
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!
Penye red, naogopa asije akasema uthibitishe
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,598
14,328
wajemeni shida hizo ziko kila mahali hata kule karatu. Rostam alikuwa mbunge tu, kazi ya kuondoa kero hizo ni ya serikali.... aghh!
Mkuu, ndio maana dada yetu ameweka sababu hizi, zinaweza kuwa tofauti na mbunge wa eneo lingine:
...
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

84 Reactions
Reply
Top Bottom