Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Kwa hili, Rostam Aziz hutasameheka

Mkuu sikatai kama binadamu habadiliki. Suala kubwa ni willingness ya binadamu kubadilika. Kama binadamu hana willingness ya kubadilika hata ukicreate mazingira ya kubadilika itakuwa ngumu kumbadilisha.

Plan B rahisi ya kumbadilisha ambaye hataki kubadirika hii hapa. INDERECTLY;
1.watengenezee tatizo(tatizo geni na ambalo halizoeleki). hilo tatizo litawafanya wa-react.
2. publicize hiyo reaction yao(kwa kutumia media). hapa conclusively watahitaji solution.
3. then baada ya hapo nenda kawape solutions.

YOU ARE DONE, LAZIMA WATAKUCHAGUA.
 
Naamini aliyoyaona kule Igunga hakutarajia mheshimiwa Regia. Kwa jimbo analotoka mtu tajiri kama Rostam.

Kwa ujumla hakuna mtu wa ccm mwenye huruma na mahitaji ya wananchi tatizo wala siyo rostam.

Mpaka hapo nchi hii itakapotoka ktk mikono ya waharamia hao waitwao ccm ndiyo tunaweza kupata maendeleo.
 
RA alichofanya ni kunufaisha mtu mmoja mmoja na kwa maslahi yake na si kwa jamii nzima, lakini PM alishamlinda kwa kauli yake kuwa wakiwajibiswa hawa nchi itayumba.
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

acha unafiki mbona hata hapa karatu kuna mafisadi wa chadema wameigeuza bodi ya maji ya KAVIWASU kuwa mradi wao binafsi m/kiti wa bodi diwani wa krt mjini(Jublete Gerson Mnyenye) na 'manager' wa bodi anayejulikana kwa jina maarufu la Ticha ni fisadi nyangumi tu kama mafisadi nyangumi wa ccm na m/keti wa halmashauri anauza viwanja vya wazi vya kijiji kila mara hivyo hayo unayoyaeleza yaeleze bila kuacha kutaja maeneo mengine ya chadema,Rostam ni fisadi kweli ila hata chadema wako wengi tu
 
Napenda kueleza kidogo kuhusu Igunga, mimi siyo Magamba wala swahiba wa Rostam ila penye ukweli nitasema. Nikiwa mmoja wa wanaIGUNGA, mzaliwa wa kijiji cha Ndembezi. Suala la elimu Rostamu amejitahidi sana, shule nyingi za msingi zimeanzishwa, na baadhi ya vijiji kuwa na shule mbili hadi tatu katika kijiji kimoja mfano Vijiji vya Ndembezi, Nkinga na Mwisi. Kwa sekondari, wakati Rostam anaingia kulikuwa na sekondari tatu wilayani, moja St.Peters Alban Ussongo ya misheni na mbili Nanga ss na Igunga ss za serikali, leo kuna zaidi ya Sekondari 15, zikiwemo za kata na binafsi 3. Ni kweli wananchi hasa wa jamii ya wafugaji hasa wasukuma na wataturu hawajui kusoma kutokana na kuendekeza mifugo zaidi. Suala la maji, nilipokuwa mdogo kulikuwa na mabomba lakini yalikufa, Rostamu kachimbisha visima vingi sana na mabwawa pia kuna vijiji vingine kuna miradi ya maji inaendelea na wananchi wanapata maji mfano Ndembezi. Suala la barabara karibu vijiji vyote vina barabara zinazopitika mwaka mzima, tatizo la uharibifu wa barabara ni kubwa kutokana na kutumiwa na mifugo. Kuhusu mawasiliano kata karibu zote zina mawasiliano ya simu hasa Airtel na Vodacom. Kuhusu kabila la kutembea uchi hakuna, wako jamii ya wafugaji wataturu wanafanana na wamasai mila zao, labda watoto wao chini ya miaka 10 ndio hukaa uchi. Suala la Tv siwezi kulisemea sana ila kuhusu umeme nadhani ni mojawapo ya wilaya zenye coverage kubwa, kuanzia Simbo, Nkinga, Ndembezi, Ziba, Iborogelo, Nyandekwa, Nanga, mpaka Igunga kuna Umeme. Rostamu alikuwa mbunge aliyetakiwa kuipigia kelele serikali kuleta maendeleo, mengi mazuri kafanya. Simpendi Rostamu kwa ufisadi wake lakini namkubali kwa yale aliyochangia Igunga. Nawasilisha
Mkuu wangu kusema kweli unaonyesha jinsi usivyoelewa maendeleo. yaani Igunga iliyokuwa na maji ya bomba leo yamekufa chini ya uongozi wake unakuja leo kumsifia kwa kuchimba visima? Je, tunaenda mbele ama tunarudi nyuma!...Halafu, kama wananchi wengi wanatembea zaidi ya kilomita 10 kwenda shule au zahanati hili swala halikugusi wewe isipokuwa kijiji cha Ndembezi ambacho wewe unatakiwa kumpa sifa diwani wako zaidi ikiwa sehemu nyinginezo hazina maendeleo. Tunachokitazama ni Rostam kafanya yapi JIMBONI kwake na kwa mapana ya wadhifa alokabidhiwa kwani kuwa na sekondari 15 bila walimu ni sawa na kuwa na yale mabomba ya maji yaliyokufa. Hizi shule mwisho wa siku zitakufa tu maanake wanafunzi hufuata WALIMU kupata elimu hawafuati majengo. Mifano ya picha imetolewa hapo nyuma na nakumbuka Mwanakijiji aliwahi kusema haya akimfunika nguo Rostam kumsetiri na aibu kubwa.

Yaani uloandika yote ni aibu tupu kusema watoto wa miaka 10 ndio hukaa uchi bila kueleza sababu ya hawa watoto kuwa uchi. halafu zaidi ya yote unasema barabara zinaharibiwa na mifugo, jamani ng'ombe wanu wanakula barabara?.. au akipita barabara yenye lami ama changarawe zilizoshindiliwa vizuri mifugo gani inaweza kuharibu barabara kiasi kwamba Regia afikirie hizi ni barabara zilizotokana na mifugo. Sote tumeishi vijijini na tunajua barabara za shamba na tumefuga mifugo vile vile tunajua tulisemalo. Picha zinajieleza zaidi ya maelezo yako.

Mkuu wangu unasikitisha sana kutooona jinsi Igunga ilivyobakia nyuma ktk maendeleo. Na pengine ndio upeo wako ktk kuyajua maendeleo, hivyo nitakusamehe.
 
Kwa kweli kuna wakati nai-hurumia Tanzania sana! at mtoa hoja ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... yaani "Mtunga sheria" na msimamizi wa sheria ya za bunge zitekelezwee... Tuna safari ndefu... tumewapa rungu watu wasio stahili... dada pole sana unaweka wazi uwezo wako... mno. unafikiria kwa kutumia moyo na sio akili... pole sana na pole sana Tanzania.
 
Asante sana Mkuu!ningeshangaa sana Kama usingniattack,ningeshangaa mno kama usingeandika haya!Baada ya kunishambulia anza sasa kujadili hoja iliyopo mezani Kama wenzako walivyofanya!
 
Nimeamua kuandika habari hii baada ya kujishauri tangu nikiwa Igunga!

Rostam Aziz amekuwa Mbunge wa Igunga tangu mwaka 1994 ambapo mpaka sasa ni takribani miaka 17 chini ya uongozi wake. Nilikuwa sijawahi kufika Igunga kabla hivyo sikuifahamu ilivyo.Siku Rostam anajiuzulu alieleza mafanikio mengi aliyoyafanya Igunga nikadhani Igunga hali ni shwari na watu wanamaendeleo mazuri,nilivyofika sikuamini nilichokiona. Rostam alitudanganya. Katika tembea yangu yote hapa nchini sijawahi kuona Wananchi wanashida kama wa Igunga.

Mambo yafuatayo nimeyagundua katika jimbo la Igunga;

1. Wananchi wengi wa Jimbo la Igunga hawajui kusoma na kuandika mpaka vijana wadogo

2. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 13 kufuata maji kwenye Makomero tena maji yenyewe sio safi wala salama

3. Wananchi wengi wa Igunga wanatembea hadi Kilomita 10 kufuata shule,wengine wanaenda hadi 20

4. Kwenye kata nilizopita hawaelewi wala kuzijua shule za awali.

5. Wananchi wengi wanatembea umbalimrefu kufuata Zahanati na hayo majengo yenyewe ya Zahanati unaweza kulia.

6. Hakuna barabara za kuunganisha kijiji kimoja na kingine,njia zilizopo ni mapitio ya ng'ombe.

7. Wananchi wengi hawana vyoo wala hawana mpango wa Kujenga vyoo,wao wajenga mabafu tu yanayotumika kuogea na kujisadia haja ndogo,haja kubwa utajua mwenyewe.

8. Zipo Kata ambazo hazing mawasiliano ya simu

9. Lipo Kabila mpaka leo wanatembea uchi kama kwa King Muswati.

10. Wapo wanaotembea karibu Kilomita 13 kufuata TV waone taarifa ya habari na mambo mengine. Hii ni Kata anayotoka Dr. Kafumu

11. Na mengine mengi madogo madogo.

Rostam alikuwa na uwezo wa kupunguza hayo niliyoyataja kwasababu zifuatazo

1. Alikuwa ni Mbunge hivyo alikuwa na fursa ya kupiga kelele ndani na nje ya Bunge na akasililizwa.
2. Alikuwa Mbunge mwenye ushawishi ndani ya chama chake hivyo angeweza kushawishi Mawaziri ili miradi iende Jimboni kwake.
3. Alikuwa Mbunge tajiri sana,kama aliweza kuipa CCM,Mabilioni ya shillingi,Kama aliweza kuhonga watu mbalimbali mamilioni ya shilingi alishindwaje kusaidia Jimboni kwake? aliishia kuwanunulia tu simu Mabalozi wa Nyumba Kumi ili wamfanyie Kampeni.
4. Alikuwa anafahamiana na wafadhili wengi tu wa Maendeleo wa ndani na nje ya nchi alishindwaje kuwashawishi wawekeze kwake?

Rostam aliyaweza haya yote lakini hakujali kwakuwa hakuwa na lengo la kuwatumikia Wananchi wa Igunga. Kwasababu hizo basi nashawishika kusema kuwa Rostam ni zaidi ya DUBWANA ni mtu anayeongoza kwa roho mbaya hapa nchini. Hana huruma hata kidogo, anajali maslahi yake tu.. Bora ulivyojiuzulu, ungejiuzulu na utanzania kabisa, ukaombe uraia wa nchi nyingine huko ughaibuni sio Afrika!

Nawasilisha!

Hapo ndio mnaonesha ukilaza wenu watu wa magwanda.

Hivi mlitegemea RA ayafanye yote hayo kama mbunge? tuoneshe wewe umefanya nini jimboni mwako halafu tufananishe aliyoyafanya Rostam jimboni mwake na kwingine zaidi ya jimboni mwake.

Unanshangaza sana, mtu mzima kwenda kuongea haya ya mtu badala ya mawazo endelevu. Mie nna uhakika mmewekeza siasa zenu katika kuongelea mtu au watu na ndio maana mkaangukia pua Igunga.
 
Mama/baba nisome vizuri utanielewa usilete jazba zako hapa.Soma taratibu uelewe na wala huna sababu ya kutukana hapa.Hakuna popte niliposema kuwa haya yote yangefanywa kwa asilimia zote na Rostam..Soma kwa pozi and you will get my concept!Nod umeamka nini?

regia huyo ni baba ..futa hio mama hapo juu
 
Mama/baba nisome vizuri utanielewa usilete jazba zako hapa.Soma taratibu uelewe na wala huna sababu ya kutukana hapa.Hakuna popte niliposema kuwa haya yote yangefanywa kwa asilimia zote na Rostam..Soma kwa pozi and you will get my concept!Nod umeamka nini?

Tafadhali sana, ni wapi nilipotukana na ni wapi nilipoonesha jazba?

Nyinyi hamna zaidi ya kuongelea watu> au hamjui namna ya kutumia weakness za mwanasiasa mmoja mkazifanya ni mradi kwenu? Rostam hayuko tena Igunga, hivi kama chama cha siasa ni juzi tu ndio mmeyajuwa yote hayo? au jina la Rostam ndio msingi wenu wa kisiasa?

Mnanshangaza na mnanisikitisha sana kwa siasa zenu maji taka. Rostam hayuko, nyie sasa fanyeni au mpaka mmpate ubunge wa jimbo fulani ndio mnawatumikia wananchi kama chama cha siasa?

Tafadhali, funguweni mawazo japo kidogo.

"Great minds talks about ideas, average minds talks about events, poor minds talks about peoples"
 
Kwa kweli kuna wakati nai-hurumia Tanzania sana! at mtoa hoja ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... yaani "Mtunga sheria" na msimamizi wa sheria ya za bunge zitekelezwee... Tuna safari ndefu... tumewapa rungu watu wasio stahili... dada pole sana unaweka wazi uwezo wako... mno. unafikiria kwa kutumia moyo na sio akili... pole sana na pole sana Tanzania.

Hapa utamuonea Regia bure, kimsingi nyanja ya siasa hapa nchini na Afrika kwa ujumla imejaa watu wa aina hii.

Lakini atleast hivi hivi kibongobongo hii inasaidia kuongeza kipato cha kaya zinazohusika na kwa extended family zilizopo hii inashuka kwa kundi kubwa sana la wananchi, japo pia inaongeza mzigo usio wa lazima kwa walipa kodi wengine wasiohusika.
 
Wakuu kusema kwamba hii ni hali halisi Tanzania nzima kiasi fulani si kweli, tukianza mfano na hiyo architecture ya flat roofing ni ya kipekee, pia inanishangaza watoto wa kijijini kukaa chini darasani. Guys just some 20, 30 years ago watoto wa kijijini walitengeneza baiskeli za miti, gravity pumping stations na kusafirisha maji kwa mianzi, kofia za mikeka. U name it. Sasa leo hii watoto wa kijijini wanakaa chini darasani? It would be interesting kama kwenye club za pombe nako wanakaa chini.

Kusema ule ukweli kuna something very wrong in our society. Jamiii yetu imekuwa reduced kutoka kujitegemea na kuwa watu wa kusubiri hand outs. Maneno kama aahh! yule bwana pamoja na kukaa ulaya hana msaada, au una mia ya karibu, unatuachaje... they are not uncommon. Miaka michahche tu iliyopita usingekuta mtu kule kijijini akienda club ya pombe bila hela eti akitegemea kupiga mizinga. Lakini leo unakutana na vijana watanashati tena jijini wako bar wanasubiri fadhila.

Kuhusu Rostam, it's just a special case. Wakuu ni wapi mliona mbunge au kiongozi wa umma analiliwa mpaka watu kuzimia eti kisa kajiuzulu? The talk around humu JF kutoka kwa akina JK, Mkapa, CCM, Nape, bila aibu hata Kafumu mwenyewe was Rostam amefanya mambo makubwa!!!!!! Ndiyo maana wengine tulipoona picha za huko tukaanzisha mpaka thread ( https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...liyofanywa-na-rostam-ni-yepi.html#post2526520 ) kwamba at least tuonyeshwe hayo makubwa ya huko Igunga.Lengo hasa ilikuwa ni kuwaonyesha watanzania maeneo mengine ambako wabunge wao hawatuhumiwi ufisadi lakini kuna hatua tangible zimepigwa.

The so called "makubwa" ya Rostam yalitumika hata kuneutralize tuhuma za ufisadi dhidi yake. Sasa imethibitika ni uongo tena mchana kweupeeeeeeeee! The guy is just a scam, fraud and heartless.
 
Kusema vilaza sio sio tusi,sio jazba?anyway tuayache hayo..Rudi kwenye Mada niliyoianzisha kama huiwezi basi achana nayo au la hayo yakwako unayoyasema sasa anzisha serdi yake tutayajadili ,kwa hapa tunajadili Uongozi wa Rostam na Igunga kwa kipindi Cha miaka 17.

Tafadhali sana, ni wapi nilipotukana na ni wapi nilipoonesha jazba?

Nyinyi hamna zaidi ya kuongelea watu> au hamjui namna ya kutumia weakness za mwanasiasa mmoja mkazifanya ni mradi kwenu? Rostam hayuko tena Igunga, hivi kama chama cha siasa ni juzi tu ndio mmeyajuwa yote hayo? au jina la Rostam ndio msingi wenu wa kisiasa?

Mnanshangaza na mnanisikitisha sana kwa siasa zenu maji taka. Rostam hayuko, nyie sasa fanyeni au mpaka mmpate ubunge wa jimbo fulani ndio mnawatumikia wananchi kama chama cha siasa?

Tafadhali, funguweni mawazo japo kidogo.

"Great minds talks about ideas, average minds talks about events, poor minds talks about peoples"
 
Hapa utamuonea Regia bure, kimsingi nyanja ya siasa hapa nchini na Afrika kwa ujumla imejaa watu wa aina hii.

Lakini atleast hivi hivi kibongobongo hii zinasaidia kuongeza kipato cha kaya zinazohusika na kwa extended family zilizopo hii inashuka kwa kundi kubwa sana la wananchi, japo pia inaongeza mzigo usio wa lazima kwa walipa kodi wengine wasiohusika.
Karibu na wewe ulingoni kwenye hii fursa kama unavyosema
 
Kwa kweli kuna wakati nai-hurumia Tanzania sana! at mtoa hoja ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... yaani "Mtunga sheria" na msimamizi wa sheria ya za bunge zitekelezwee... Tuna safari ndefu... tumewapa rungu watu wasio stahili... dada pole sana unaweka wazi uwezo wako... mno. unafikiria kwa kutumia moyo na sio akili... pole sana na pole sana Tanzania.

Hao ndio wabunge wetu na watunga sheria. Ukistaajabu ya Musa kuna na ya Firauni.
 
Hapo ndio mnaonesha ukilaza wenu watu wa magwanda.

Hivi mlitegemea RA ayafanye yote hayo kama mbunge? tuoneshe wewe umefanya nini jimboni mwako halafu tufananishe aliyoyafanya Rostam jimboni mwake na kwingine zaidi ya jimboni mwake.

Unanshangaza sana, mtu mzima kwenda kuongea haya ya mtu badala ya mawazo endelevu. Mie nna uhakika mmewekeza siasa zenu katika kuongelea mtu au watu na ndio maana mkaangukia pua Igunga.

Wewe ni mmoja wao ulikuwa ukishabikia makubwa ya Rostam Igunga. Ushahidi uko humu humu JF, you have been challenged for more than a month kuleta angalau kubwa moja ukayeyuka, kimyaaaaaaaaaaa!!!! Kumbuka RA is a king maker, ni jinamizi haongelewi eti kwa kumuonea wivu kama mlivyozoea kuita wanaohoji ujambazi.
 
Kusema vilaza sio sio tusi,sio jazba?anyway tuayache hayo..Rudi kwenye Mada niliyoianzisha kama huiwezi basi achana nayo au la hayo yakwako unayoyasema sasa anzisha serdi yake tutayajadili ,kwa hapa tunajadili Uongozi wa Rostam na Igunga kwa kipindi Cha miaka 17.

Ukilaza kijana sio tusi wala jazba, ni ukweli. Hivi unakuja kama mbunge kuongelea mtu aliyekwisha achia ngazi?

Turudi kwenye mada ipi ya kuongelea mtu? unanchekesha! hebu kuwa kama mbunge wa ukweli na uongelee kuwa nimekuta mapungufu haya na haya na haya na sasa nafanyia kazi haya na haya na haya. Achana na kuwekeza kichawi kwenye vichwa vya watu.
 
Hao ndio wabunge wetu na watunga sheria. Ukistaajabu ya Musa kuna na ya Firauni.

Na bado Kama haya mnastaajabu basi miaka mitano ijayo mtaona na kusikia mengi ndani na nje ya Bunge......

Kama wewe mwenyewe hujishangai mwanaume kujivalisha hijabu na kujipachika majina ya kike,utawezeja kuchambua hoja bila kuwa na bias hasa pale penye ukweli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom