Kutoka kwenye familia tuliyosomeshwa kwa gharama kubwa kumeniathiri kiuchumi, Kupeleka watoto kayumba ni aibu, Napambana kukwepa aibu

Mtoto kama ana akili hata akisoma kayumba anafaulu vizuri tu. Kama kilaza hata ukimpeleka English Medium bado atakuwa na ufaulu hafifu.
Kupeleka mtoto Private ni zaidi ya kufaulu kwenye mitihani, Hata vijijini kwenye shule wanazokaa chini wapo vipanga wanaofaulu zaidi.

Ni suala la kumrahishia maisha mtoto, kuhusu kufaulu hilo ni jambo lingine.

soma uzi mzima.
 
Kila la kheri, Ila nafikiri uandae tuu saikolojia yako kuwa wanaosomesha watoto serekalini sio wote ni masikini au kuaomesha watoto kayumba sio fedheha.
Kama umewahi kusoma kayumba hata ukija kuwa tajiri ni kawaida kusomesha mtoto kayumba, uzoefu wako wa hizo shule unaweza kumsaidia mtoto kwenye kumpa ushauri mtoto, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?
 
Chekechea na Primary nimesoma english medium private

Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.

Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.

Nilipokuwa baba uchumi haukuwa vizuri ila nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA ??? Kwa maisha niliyopambaniwa niyaishi kupanda magari ya njano, watoto waanze kutembe na vidumu??

Ndipo nilipoanza mapambano ya ziada kuwaandalia watoto future, yote hii ni kukwepa aibu.

Nina watoto watatu napambana mno watoto wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,

Hivi hata wazazi watanichukuliaje aisee ?? Baba ulisomeshwa kwa raha watoto usomeshe kayumba ??

Shule nilizosoma zilirahishia maisha yangu ya shuleni,

  • Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
  • Chakula kizuri shuleni
  • Mazingira tulivu
  • Usafiri shuleni hadi nyumbani
  • kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
  • Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
  • Hakuna kujazana darasani
  • kujifunza computer utotoni
  • Library
  • masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
  • Marafiki wengi hutokea familia zinazojali malezi
  • n.k.

Hadi sasa napambana sana japo kipato si kikubwa.

Mtoto moja yupo form 1 ada milioni 2 na nusu kwa mwaka

Moja yupo Primary ada laki 9 day.

Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9

Sina mpango wa kuongeza mtoto wa tatu labda uchumi ukae sawa

Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.

Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za mafuta, wife ana passo, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga
Dogo umezaa mapema sana,anyway pambana na hali yako.
Sisi wenzako 36 tuna watoto 2 hawajaanza shule serious za mahela makubwa makubwa. Tunatumia muda huu kujenga. Wakishaanza kuwa serious, ujenzi hakuna ni kusomesha tu.
Wakimaliza kusoma ni mwendo wa bata na mama yao, labda na mtoto mmoja wa mwisho.
 
Mkuu kama umepitia Kayumba naweza kutamani niwe wewe maana hata nikipeleka mtoto huko hakuna cha kujutia.

Ishu inakuja wewe baba ulisomeshwa shule za private english medium, Kusomesha watoto Kayumba roho itauma
Kwahiyo unasomesha English Schools kwa presha/hofu tu ila sio matakwa yako, kwa maana ungekuwa uko huru wanao wangesoma Kayumba?
 
Chekechea na Primary nimesoma english medium private.

Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.

Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.

Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ? Kwa jinsi wazazi walivyonipambania maisha ya shule yawe mepesi kweli watoto wangu waanze kwenda kayumba ?

Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba, wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?

Hivi hata wazazi watanichukuliaje ? wamepambana nisome kwa raha kisha wajukuu wao niwasomeshe kayumba ??

Nina watoto watatu napambana mno watoto wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,

Hadi sasa napambana sana japo kipato si kikubwa.

  • First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
  • wa pili yupo Primary day ada laki 9.
  • Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
  • Sina mpango wa kuongeza mtoto wa tatu labda uchumi ukae sawa

Nimelenga hasa kuwarahisisha maisha watoto, kuhusu kufaulu hizo ni bidii zao na uwezo wao (hata kayumba kuna vipanga)

  • Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
  • Chakula kizuri shuleni
  • Mazingira tulivu
  • Usafiri shuleni hadi nyumbani
  • kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
  • Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
  • Hakuna kujazana darasani
  • kujifunza computer utotoni
  • Library
  • masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
  • Marafiki wengi hutokea familia zinazojali malezi
  • n.k.

Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.

Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za mafuta, wife ana passo, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga
Its all about mindset, watoto wata adopt. It you mwenye ego and pride. Drop them na utaona ni kawaida mkuu. Haya ni maisha yanabadilika mno kwa kasi
 
Dogo umezaa mapema sana,anyway pambana na hali yako.
Sisi wenzako 36 tuna watoto 2 hawajaanza shule serious za mahela makubwa makubwa. Tunatumia muda huu kujenga. Wakishaanza kuwa serious, ujenzi hakuna ni kusomesha tu.
Wakimaliza kusoma ni mwendo wa bata na mama yao, labda na mtoto mmoja wa mwisho.
36 una mtoto hajaanza shule ni kwamba wa kwanza umempata ukiwa na miaka takribani 33

muda wote hadi 32 ni kwamba hakuna mwanamke alienasa mimba yako ?

ungejitahidi at least uwe na mtoto ambae ukifika 50 yeye nae kaanza harakati za kukutaftia wajukuu :) :)
 
Back
Top Bottom