Kutoka kwenye familia tuliyosomeshwa kwa gharama kubwa kumeniathiri kiuchumi, Kupeleka watoto kayumba ni aibu, Napambana kukwepa aibu

Chekechea na Primary nimesoma english medium private.

Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.

Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.

Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ?

Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?

Natoa mfano mwepesi hata kama umesoma kayumba lakini ulipambaniwa ule milo mitatu, ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane watoto wale milo mitatu, ukikutana na mzazi aliekulia maisha ya milo miwili nae analisha watoto mara mbili, akikupa ushauri kwamba ulishe watoto mara mbili ni ngumu kumuelewa hata kama watoto wake wana nguvu na afya kuzidi wako.

Ndivyo ilivyo kwa upande wangu, nilipambaniwa ili maisha yangu ya shule yawe mepesi ni ngumu mimi kuwapeleka watoto Kayumba, pia hata wazazi watanichukuliaje ? wamenipambania nisome kwa raha kisha waje kuona wajukuu wanaenda kayumba ?

Kwa sasa nina watoto watatu nawapambania wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
  • First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
  • wa pili yupo Primary day ada laki 9.
  • Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
  • Sina mpango wa kuongeza mtoto wa ziada labda uchumi ukae sawa

Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno, Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni

  • Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
  • Chakula kizuri shuleni
  • Mazingira tulivu
  • Usafiri shuleni hadi nyumbani
  • kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
  • Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
  • Hakuna kujazana darasani
  • kujifunza computer utotoni
  • Library
  • masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
  • watoto wengi hutokea familia zinazojali malezi na maadili.
  • wanafunzi wengi hufika elimu ya juu (shule ya msingi 80% niliosoma nao tuna degree, kuna msukumo unaupata usiachwe sana na wenzako kielimu)
  • n.k.

Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.

Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za usafiri, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga
Pole sana kaka kwa unayopitia kwa wakati huu na nikutoe hofu almost waajiriwa wengi wanapitia hapo na wapo ambao umewazidi maana umefikia hatua unatembelea IST yako mwenyewe.

Ushauri wangu kwako
1. Ni hatari sana kiuchumi kwako na familia kama unasomesha watoto private school kwa sababu tu wew ulipitishwa huko au unaogopa watakuonaje watu waliokuzunguka.

Uhatari huu utauona katika viashiria viwili
i. Unakopa ili kulipa ada
ii. Unaairisha moja ya mipango yako ili kulipa ada.

Nivema uweke tathimini za kiuchumi na kama upo kwenye moja ya kundi hapo juu nivema kufanya uamzi wa busara juu ya uchumi wako, binafsi sioni shida katika shule za Umma maana wengi tumesoma huko na ziko vizuri japo kuna changamoto ambazo ni za kawaida.

2. Nakushauri pia soma vitabu hivi viwili vitakusaidia sana katika ufumbuzi wa changamoto yako

i. Usichokijua kuhusu Malezi Kimeandikwa na mwanasaikolojia Mtanzania Deogratius Sukambi

Kitabu hiki katika sura yake ya pili (mtego wa upendo) kitakusaidia sana kuepuka kuingia katika mtego wa kudhania kuwa ukiwapelek huko private school ndio utakuwa umewapatia kilichobora
Sura yake ya Sita (Vifungo hisia) itakuwezesha kuepuk na hisia ulizonazo kuwa ulipopitishwa ndipo unabid na wew upitishe wengine

Lakini kwa ujumla wake kitabu kitakusaidia sana katika kujua wajibu upi n sahihi kwa mzazi kwa watoto wake na watoto pia kwa wazazi

ii. Millionare next door by Dr Thomas J Stanley & Dr William Danko

Kitabu hiki katika sura yake ya pili (Frugal Frugal Frugal) itakusaidia namna ya familia yako binafsi inaweza kuishi chini ya kipato chako ili kuweza kuwekeza amount ya pesa nyingi hatakama mna kipato kidogo au kikubwa

Katika sura yake ya tano (Economic Outpatient Care) itakusaidia kujua namna private school zinawafany wazazi wengi kuishia kuwa maskini lakini pia kuzarisha vizazi vinavyokuja kuwa katika truck hii ya private school mentality. (wakiamini ndio shule bora)

Hapo utaona ametolea mfano wa Ndoa ya Marry and Lamar walivyokuwa na hiyo mentality na wakawa masikini

Kitabu hiki kwa ujumla kina lenga tafiti zilizofanywa nchini malekani na hawa Doctrate wawili kujibu swalinla kwa nini watumishi wengi richa ya kulipwa pesa nyingi bado wanakufa masikini au wanakuwa dependent leaving in paycheck na wakistafu hawanauwezo wa kumudu maisha yao. Kisome chote nikitabu kizuri

Asante
Regards
M. Miguel
 
Ndio maana tunasema muende shule nzuri "pwenti"ndio Nini🤔?
Duh shule nzuri uliyo soma imeshindwa kukuongoza kuelewa kwamba "pwenti" ni neno lisilo rasmi linalo tumiwa na vijana wa kitanzania kumaanisha " point" ?

Mnalipa mamilioni ili kukariri sio? 😁😁😁
 
Hamna Cha vijana Wala cha Nini wewe sema tu umeandika mbiombio hamfundishwi kuhariri maandiko yenu kabla hamjayapeleka public!hebu hamisha watoto Hizo shule wasije rithi hili tatizo🤔
 
Chekechea na Primary nimesoma english medium private.

Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.

Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.

Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ?

Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?

Natoa mfano mwepesi hata kama umesoma kayumba lakini ulipambaniwa ule milo mitatu, ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane watoto wale milo mitatu, ukikutana na mzazi aliekulia maisha ya milo miwili nae analisha watoto mara mbili, akikupa ushauri kwamba ulishe watoto mara mbili ni ngumu kumuelewa hata kama watoto wake wana nguvu na afya kuzidi wako.

Ndivyo ilivyo kwa upande wangu, nilipambaniwa ili maisha yangu ya shule yawe mepesi ni ngumu mimi kuwapeleka watoto Kayumba, pia hata wazazi watanichukuliaje ? wamenipambania nisome kwa raha kisha waje kuona wajukuu wanaenda kayumba ?

Kwa sasa nina watoto watatu nawapambania wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
  • First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
  • wa pili yupo Primary day ada laki 9.
  • Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
  • Sina mpango wa kuongeza mtoto wa ziada labda uchumi ukae sawa

Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno, Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni

  • Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
  • Chakula kizuri shuleni
  • Mazingira tulivu
  • Usafiri shuleni hadi nyumbani
  • kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
  • Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
  • Hakuna kujazana darasani
  • kujifunza computer utotoni
  • Library
  • masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
  • watoto wengi hutokea familia zinazojali malezi na maadili.
  • wanafunzi wengi hufika elimu ya juu (shule ya msingi 80% niliosoma nao tuna degree, kuna msukumo unaupata usiachwe sana na wenzako kielimu)
  • n.k.

Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.

Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za usafiri, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga
Tuondolee maisha ya maigizo wewe
 
Hamna Cha vijana Wala cha Nini wewe sema tu umeandika mbiombio hamfundishwi kuhariri maandiko yenu kabla hamjayapeleka public!hebu hamisha watoto Hizo shule wasije rithi hili tatizo🤔
Duh inaonekana wewe mtoto wa geti kweli kweli yani hujawahi kabisa kusikia neno " pwenti" maisha yako yote?

Vipi na kuhusu neno " Piwa" kumaanisha " Pure"?

Anyways hayo ndo madhara ya kukariri darasa.

Umezidiwa maarifa mpaka na mababu zetu.

Wazungu walipo kuja Tz waliwaambia babu zetu kwamba nguo ya kuvaa juu inaitwa " Shirt" ( sheet!)

Babu zetu wakawaambia acheni ujinga nyinyi, mbona mwahangaika kutumia nguvu nyingi sana kuelezea simple term kama hiyo? Kwanini msiseme tu " Shati" mbwa nyinyi, ( sheet) ndio mboga gani tena?

Hawakusikia wazungu wakaja tena na neno ( Cupboard)

Babu zetu wakawaambia hivi nyie mna shida gani nyie mabwege?

Cupboard ndio nini tena?

Kwanini msiseme tu " Kabati"

Sasa wewe ndio wale waswahili walio kariri uzungu.

Narudia tena kwa mara nyingine " pwenti" inamaanisha " point" acha kukariri
 
English medium zina faida kwenye hilo hakuna ubishi

Ushawahi sikia binti wa english medium kapewa mimba na boda?

Pambania.
nishaona mzee tena nimesoma nae class moja advance akiwa analea Mtoto kwao.alinipa stories ilikuwa kivumbi kwao nusura mama yake na yeye wote wafukuzwe Nyumbani mana baba yake alimind vibaya sana
 
Kupeleka mtoto Private ni zaidi ya kufaulu kwenye mitihani, Hata vijijini kwenye shule wanazokaa chini wapo vipanga wanaofaulu zaidi.

Ni suala la kumrahishia maisha mtoto, kuhusu kufaulu hilo ni jambo lingine.

soma uzi mzima.
Nadhani hapa wazazi wengi tunalenga katika kuwaandaa vijana wetu kuwa raia wa dunia(global citizens) ili kutumia uwanda mpana wa dunia kujikwamua kiuchumi. Ni kazi ngumu mtoto aliyesoma shule za umma kuanzia chekechea hadi chuo kikuu kuweza ku interact na dunia kama mwenzake wa private school.

Jambo la kuzingatia ni uwezo wako wa kiuchumi maana haina faida kuingia kwenye madeni yaliyokuzidi kimo ili kumpeleka mtoto private school.
 
Hizi pepsi za sasa za take away zina ladha gani?? Mbona mbaya hivi..

Ni kweli mkuu pambana..
 
Chekechea na Primary nimesoma english medium private.

Sekondari Form 1 hadi 6 nimesoma Boarding private, Msosi Pilau kila J5 na J2, Ugali ni nadra sana.

Chuo kikuu sikupata mkopo ila si haba sikuwahi kupata changamoto za kiuchumi.

Rasmi na mimi nikawa baba, nikaanza kuwaza watoto waje kusoma KAYUMBA wakati mimi sijasoma huko ?

Hali yangu ni tofauti na waliowahi kusoma kayumba wao hata wakiwa matajiri wanaweza kusomesha watoto kayumba kwa uhuru, wana uzoefu na hizo shule kwahiyo wanaweza kuwasaidia watoto mawazo na ushauri, sasa mimi sijasoma kayumba wala siyajui mazingira yapoje nitamshauri nini mtoto ?

Natoa mfano mwepesi hata kama umesoma kayumba lakini ulipambaniwa ule milo mitatu, ni kwamba na wewe ukiwa mzazi kuna msukumo unakuingia upambane watoto wale milo mitatu, ukikutana na mzazi aliekulia maisha ya milo miwili nae analisha watoto mara mbili, akikupa ushauri kwamba ulishe watoto mara mbili ni ngumu kumuelewa hata kama watoto wake wana nguvu na afya kuzidi wako.

Ndivyo ilivyo kwa upande wangu, nilipambaniwa ili maisha yangu ya shule yawe mepesi ni ngumu mimi kuwapeleka watoto Kayumba, pia hata wazazi watanichukuliaje ? wamenipambania nisome kwa raha kisha waje kuona wajukuu wanaenda kayumba ?

Kwa sasa nina watoto watatu nawapambania wasije pitia maisha ambayo mimi sikupitia,
  • First yupo form 1 boarding, ada milioni 2 na nusu kwa mwaka
  • wa pili yupo Primary day ada laki 9.
  • Huyu mwengine nae soon anaanza shule hio ya laki 9
  • Sina mpango wa kuongeza mtoto wa ziada labda uchumi ukae sawa

Suala la kufaulu wapo wanafunzi wanaokalia ndoo wanapasua vibaya mno, Kusomesha private kumelenga zaidi kumrahishia mtoto maisha ya shuleni

  • Vyoo visafi kila siku vinasafishwa
  • Chakula kizuri shuleni
  • Mazingira tulivu
  • Usafiri shuleni hadi nyumbani
  • kutumia kiingereza kwenye masomo tangu shule ya msingi
  • Kila mwanafunzi ana kiti na dawati lake
  • Hakuna kujazana darasani
  • kujifunza computer utotoni
  • Library
  • masomo ya kupika, kushona, kuchora, n.k.
  • watoto wengi hutokea familia zinazojali malezi na maadili.
  • wanafunzi wengi hufika elimu ya juu (shule ya msingi 80% niliosoma nao tuna degree, kuna msukumo unaupata usiachwe sana na wenzako kielimu)
  • n.k.

Ninajua zipo shule za bei rahisi mfano kuna shule za serikali za englsh medium, shule za sekondari za jumuia ya wazazi, n.k. kwa research yangu zimetofautiana kidogo na Kayumba.

Kwa sasa nina miaka 36 kiuchumi bado najibana sana hasa kwasababu bado najenga ili nihamie kwangu, imenibidi nitembelea IST ili kupunguza gharama za usafiri, Simu yangu ina miaka mitatu sijabadili, wife nae nashukuru anajua tunayopitia nae kapunguza vizinga
Huyo wa mwisho muanzishe government kuliko kumpeleka private kisha yakakushinda na kuamua kumpeleka government
.

Ni heri aanze huko huko.
 
Darasa moja wanafunzi 100.
Zaidi ya 100, kuna baadhi ya shule darasa moja utakuta wanafunzi mia nne ,dawati la kukaa wanafunzi watatu wanajibana wanakaa watano wengine wanakaa chini ndio maana wengi wao huwa ni wachafu sana
 
Back
Top Bottom