Mrejesho: Faida nilizopata baada ya kuwatoa watoto wangu shule ya English Medium na kuwarejesha kayumba

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Dec 7, 2018
718
1,643
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa JF wenye title" Tunaowatoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Soma: Tunaowatoa watoto wetu shule za kiingereza njooni hapa tufarijiane

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakaonipa "faida" nitakazozipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapofika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sitokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanaosoma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu; yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko waliosoma shule za kiingereza.

2. Brother wangu wa mtaani ambaye na yeye kawarudisha watoto wake kayumba. (Huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary). Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa…(anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu)

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza "shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini (ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake). Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.

1. Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa Tsh. laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo Kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni wewe ukiwa na hela yoyote hata laki tano niite kwa laki tano hiyo hiyo nitafanya kitu. Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kinondoni shamba au Hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anaowajengea nyumba anasema “huyu anauza mchicha, huyu mama lishe etc”. Nikawa inspired.

2. Kuhusu somo la kiingereza nimenunua vitabu na CDs ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
 
Baba yangu mdogo amefungwa jela baada ya kuwa tapeli na madeni mengi kisa anasomesha English Medium uwezo mdogo.

Kuliko Umsomeshe mtoto Nursery unalipa 1M primary unalipa 1.2M, Sec unalipa 2M then Chuo unampeleka kwa Asante Nyerere University akimaliza huko anakuja Mitaani kutembeza Bahasha na akipata Kazi analipwa Laki Saba.

Fikiria kama hizi ni akili au matope?

Peleka Expensive schools kama una hela ila usiingie madeni bure.

Hata hao wanaopeleka feza na st Thomas wengi sio pesa zao. Ni hizi hizi unazosikia wameiba na kuficha kwenye majumba.

Tafuta pesa wekeza kwenye assets wapeleke shule nzuri moderate kama wewe kipato chako kama changu.
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunao watoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.

Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunao watoa watoto wetu shule za English Medium na

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.

Mpeleke mwanao kayumba kama huna hela, ila usimpeleke huko ili ujenge.
 
Baba yangu mdogo amefungwa jela baada ya kuwa tapeli na madeni mengi kisa anasomesha English Medium uwezo mdogo.

Kuliko Umsomeshe mtoto Nursery unalipa 1M primary unalipa 1.2M, Sec unalipa 2M then Chuo unampeleka kwa Asante Nyerere University akimaliza huko anakuja Mitaani kutembeza Bahasha na akipata Kazi analipwa Laki Saba.

Fikiria kama hizi ni akili au matope?

Peleka Expensive schools kama una hela ila usiingie madeni bure.

Hata hao wanaopeleka feza na st Thomas wengi sio pesa zao. Ni hizi hizi unazosikia wamwiba na kuficha kwenye majumba.

Tafuta pesa wekeza kwenye assets wapeleke shule nzuri moderate kama weww kipato chako kama changu.
Naunga mkono hoja asilimia mia.
 
Upo sahihi mkuu mi pia watoto wangu nimewatoa English Medium nimewaleta kayumba ambayo ipo jirani na ninapoishi.

Imenisaidia kupunguza gharama unnecessary na kuniondolea stress ambazo hazina kichwa wala miguu.

Halafu sisi wazazi ndo tunaona fahari watoto wetu kusoma English Medium ila watoto wala hata hawaoni tofauti
 
Miezi michache iliyopita nilianzisha Uzi hapa jf wenye title" Tunao watoa watoto wetu shule za English Medium na kuwarejesha kayumba njooni tufarijiane hapa"

Lengo la Uzi lilikuwa kupata watu watakao nipa " faida" nitakazo zipata kwa kuwarejesha watoto wangu Kayumba plus maneno ya kunifariji ambayo yatasaidia kujustify uamuzi wangu.

Sababu ya kuwarejesha kayumba wanangu ni kuyumba kiuchumi. Nilipata maoni mengi mazuri. Miongoni mwa maoni niliyopata hapa JF ni pamoja na:

1. Itanisaidia kuokoa pesa ambayo ninaweza ku invest katika maeneo mengine muhimu kama vile kuwanunulia viwanja na kuwajengea nyumba watoto wangu so that wanapo fika level ya chuo at least kila mtu awe na nyumba yake moja.

2. Sintokuwa na stress za ada plus mbaya kuliko zote( ile stress maalumu ambayo mzazi unaipata wakati mtoto wako amerudishwa nyumbani ada, wakati wenzake plus jirani zako wanao soma kayumba wanaenda shule.

Nje ya JF nilipata ushauri kutoka kwa

1. Binti yangu ( yeye yupo form three shule ya kayumba pia. Nilimsomesha English Medium kuanzia la kwanza. Anasema daddy kuna watoto wamesoma shule za kiswahili lakini wapo vizuri sana darasani kuliko walio soma shule za kiingereza.

3. Brother wangu wa mtaani ambae na yeye kawarudisha watoto wake kayumba.. (huyu kasomesha hadi chuo but still bado ana watoto wa primary. Alikuwaga kichaa wa shule za English medium.

Anasema mdogo wangu mtoto wako umsomeshe kayumba au English Medium mwisho wa siku wote watakufa watazikwa" anataja jina la makaburi ya mtaani kwetu"

Akaongeza: Tofauti ya kayumba na English Medium ni lugha tu lakini mwisho wa siku wote wanaandaliwa kuajiriwa..

Kingine siku hizi watoto wanaharibika sana so hakuna guarantee mtoto wako atakuja kuwa nani hapo baadae.

Akaongeza " shule nyingi za English Medium zinawafanya wanafunzi hasa watoto wa kiume kuwa watoto walaini laini ( ana experience na watoto wake mwenyewe na rafiki zake)

Halafu haziwafundishi watoto kuhusu uhalisia wa maisha zaidi ya kuwakaririsha masomo so bora umpeleke kayumba akapambane na kukomaa huko.

MIEZI MIWILI BAADA YA KUFANYA UAMUZI.
Nimenunua kiwanja nje ya mji ( ilala rural/ mvuti) kwa sh.laki tisa na mwezi ujao Insha'allah nitapiga msingi( fundi wangu yupo kinondoni ambae alinijengea nyumba yangu ya kwanza utaratibu wake wa kazi huwaga ni" wewe ukiwa na hela yoyote hata laki TANO niite kwa lako TANO hiyo hiyo nitafanya kitu . Next time ukipata laki tatu niite. Hadi nyumba yako itakamilika. Huyu ndo alinifanya nikajenga nyumba yangu ya kwanza. Tukiwa Kino garden au hananasif tunaangalia ndondo anapokea simu za watu anao wajengea nyumba anasema ' huyu anauza mchicha' huyu mama lishe, etc. Nikawa inspired.

Kuhusu somo la kiingereza: nimenunua vitabu na cds ambayo madogo watakuwa wanajifunza wakiwa home plus tuition ya nguvu ya kiingereza.

Mungu akinipa uhai nitafanya vitu vikubwa sana kwenye familia yangu.

Kama uwezo wako mdogo, unaishi nyumba ya kupanga uswahilini, uchumi wako umeyumba, sikushauri uhangaike na English medium.

Mpeleke mwanao kayumba wewe upambane kutafuta hela.
Kumbe Dar es salaam kuna viwanja vya laki tisa?.

Tunakunywa bia kila siku tukijua viwanja ni mamilioni
 
Hongera sana.

Mtoto akilelewa vizuri na akapata mahitaji ya lazima kwa binadamu basic needs kwa wakati na mental health nzuri, usimamizi wa kimasomo mzuri, Hata akisoma kayumba lazima afanye vizuri

Chuo kikuu cha dsm, ama Udsm best students wao kwenye graduations kila mwaka ni waliosoma kayumba primary.
 
Upo sahihi mkuu mi pia watoto wangu nimewatoa English Medium nimewaleta kayumba ambayo ipo jirani na ninapoishi.

Imenisaidia kupunguza gharama unnecessary na kuniondolea stress ambazo hazina kichwa wala miguu.

Halafu sisi wazazi ndo tunaona fahari watoto wetu kusoma English Medium ila watoto wala hata hawaoni tofauti
Hongera sana mkuu
 
Back
Top Bottom