William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,464
- Thread starter
- #601
Wakuu heshima mbele, kama tulivyoahidi kuwa tutahitimisha dataz za nec,
1. Kulikuwa na wazungumzaji wengi siku hiyo, kutoka makundi mawili yaisyokubaliana na kupendana kabisaa kama ilivyojionyesha kwenye mjadala huu wa siku ya mwisho, ingawa kati ya wote waliooongea, ni watatu ndio hoja zao ni worhty kuziweka hapa, nao ni muungwana, sendeka, na selukamba.
2. Sendeka, alianza kwa kumshambulia muungwana kwa nguvu sana kuwa anawalinda mafisadi, ndio maana wanakuwa na kichwa cha kuweza kwenda kwenye majimbo yao ya uchaguzi na kutengeneza sherehe zao kubwa za mapokezi na kulidhihaki taifa na hotuba zao chafu.
3. muuungwana alismama kujibu tena kwa hasira sana kuwa maneno ya sendeka hayana ukweli kwa sababu, kama sio yeye muungwana, el bado nagekuwa na madaraka mpaka leo, ".....ninasema kuwa siku nne kabla ya kwenda Dodoma kwenye kikao cha ile ripoti, edward alikuja kwangu na kuniomba kuwa nimpe nafasi ili ajieleze kuhusiana na ripoti, lakini nikamkatalia kata kata na kumtaka aende mbele ya wananchi kule bungeni akajieleze na kujitetea kwa sababu mimi siwezi kumsaidia....", " .....lakini kwa mshangao mkubwa akaniletea barua ya kujiuzulu, badala ya kujitetea bungeni......"
4. Ikaja zamu ya selukamba, aliyemshambulia sana sendeka kuwa ni kibaraka wa mama kilango, na kusema kuwa choko choko zote za kina sendeka na wenziwe zinaanzia kwa mama kilango, alismea kuwa "........kuna watu ambao hawaonekani kuelewa kuwa uchaguzi wa urais uliiisha zamani bado wanataka urais mpaka leo, hivi hawajui kuwa Tanzania tuna rais tayari?...."
selukamba aliwashangaza wajumbe wote kwa kauli nzito aliyoitoa kuwa anaomba kulindwa maana mama kilango (ambaye hakuhudhuria kiako siku hiyo), amemtishia sana kuwa anaweza kumpiga au kumfanyia ubaya.
5. sendeka alirudi tena na kumjibu selukamba kuwa ni kibaraka wa mafisadi na hasa el na akamuonya muungwana na njama kubwa wanaozizfanya za kutaka el awe rais mwaka 2010, "....tunajua kuwa mnajitayarisha kugombea urais mwaka 2010 sio siri sasa kama sio unafiki ni nini mwambieni tu rais yupo hapa?....", ilibidi muuungwana aingilie kati maana sasa wajumbe walikuwa karibu washkane mashati, alianza kwa kujaribu kumsafisha el lakini wajumbe wakaguna sana kwa mshangao, ndipo alipoanza kunawa mikono kama nilivyozileta jana.
6. Ishu ya Mkamba kuondolewa ukatibu ilisemwa wazi pamoja na juhudi zote za baadhi ya mafisadi kuitoa kwenye agenda na ilikubaliwa kuwa itapelekwa kwenye kikao cha karibuni cha cc kwa uamuzi wa mwisho. Na pia wanachama wote watakaobainika kuwa ni mafisadi watafukuzwa chama.
7. Mbunge wetu shujaa Mwakyembe bado hajarudi Dodoma, mpaka sasa hivi ninapoandika, akiendelea na uchunguzi wa madikatari bingwa DAr, naye Spika amewapa masaa 72 wale wote kuanzia polisi mpaka uwt waliokuwa wakichunguza ile soo ya bunge, kumpa matokeo mara moja. Sasa the showdown ya makundi haya mawili kati ya mafisadi na wengine inahamia bungeni, ambako the dataz ni kwamba kati ya siku mbili zajazo kutakuwa na mashambuliano ya kukata na shoka, kwenye mjadala wa bajeti.
Kwa haya wakuu naomba kusema ndio mwisho wa dataz kutoka kikao cha nec kilichoisha hivi karibuni, heshima mbele kwa wote waliochangia hii mada, na wale waliopitisha angalau macho yao tu, nia na madhumuni yetu ni moja tu nayo ni kuelimishana na kuhbarishana habari muhimu za taifa letu na kumuachia mwananchi aaamue mwenyewe cha kufanya, au kutokufanya. Ni muhimu kupeana za ndani kabla hazijafika kwenye media na kuwa spinned na kina Chiligati, maana sasa hata waki-spin tunawangalia kwa macho mawili maana we know the truth.
Ahsante Wakuu! tuendelee kukata ishus maana taifa liko njia panda!