Kutoka Dodoma!

Naamini Chenge kama Mbunge ana wajibu wa kuwaelimisha wananchi si wa Bariadi pekee bali nchi nzima kwa kitendo alichokifanya humo ndani ya Bunge baada ya masaa ya kawaida. Au huenda akawa anahitaji kazi nyingine ya kuwa MSAFISHAJI na MUANDAAJI wa ukumbi wa Bunge. Wananchi wana haki ya kujua nini kilinyunyizwa kwenye hivyo viti.
 
Mh. Sitta naye alitakiwa ku-come forward aeleze kama kuna kanuni za bunge zilikuwa zinamruhusu Chenge kufanya alichokifanya, au kama alikuwa na idhini ya kuandaa ukumbi kabla ya kikao kilichokuwa kinafuata. Je huyo afisa wa Bunge naye alikuwa anaangalia wapi wakati kunanyunyizwa kitu kwenye sehemu hizo zilizotajwa.
 
Hollo,
Amka ndugu yangu. Evidence zipo. Si umesikia kamera zilikuwa zinayoyoma?
Haya camera zimeyoyoma hizo movie zipo wapi?wekeni hapa tujue kama ni kweli!la sivyo ni kubuild castles in the air
 
kufichuka kwa siri za mafisadi si jambo rahisi, tumshukuru Mungu mwenyezi ameamua kusikiliza maombi ya wamchao ili kulisafisha taifa. Sasa ni nafasi yetu, kuweka wazi, kukemea na kukataa kabisa kutumiwa na madfisadi. SHUKRANI kwa watoa data, asante sana.

Aibu... aibu... Mungu ibariki Tanzania
 
Watu wanaweza kuchukulia hii issue lightly lakini hapa kuna kaharufu fulani fulani kabaya. Sijui na TAKUKURU watakuwa na nafasi gani katika hii issue. Hainiingi hata chembe huyo ofisa wa bunge kuendelea kumuangalia Chenge akimwaga huo ujinga wake kwenye viti vya waheshimiwa bila ya kusema lolote. Kuna ka-harufu kwa rushwa hapo. Vinginevyo huyo Ofisa atoe maelezo ni vipi haruhusu huo ujinga ufanyike tena kwa SELECTED SEATS. Na kama ilikuwa halali kwa nini hawakufanya kwa Bunge zima? Labda Sitta atueleze kama kulikuwa na hiyo tenda bila kutangazwa hadharani, kwi kwi kwi.
 
hata thomaso ni hadi alipoona alama za misumari!kuwepo kwa data siyo hoja!data zinaweza zikawepo na zikawa wrong vilevile

Hollo, ni bora utulie pembeni ndugu yangu uangalie upepo unakovuma - kuwa devil's advocate hakukataliwi, ila adha ya 'kula matapishi' yako mwenyewe huwa ni kero na ngumu kuvumilia!! Baadae
 
Kwa wale wanaoamini imani za dini wanajua kwamba shetani akishakukutumia huwa lazima ifike mahala akuumbue. Sasa hivi naona shetani ameamua kuwaumbua ndugu zetu wa CCM. Tuendako watasambaratishana kama mchwa waliokosa kichuguu. Uzuri ni kwamba yote haya yakitokea Taifa litapona.

Yaani hadi leo kuna wana CCM bado wanafanya siasa kwa uchawi, yaani mtu alikuwa mwanasheria mkuu, mwenyekiti wa maadili wa chama tawala anajaribu kujijenga kisiasa kwa njia za uchawi! Sasa tusubiri kama wana CCM wa Bariadi watamwandalia sherehe tena kwa kukamatwa akiloga. Aibu!
 
Wananchi wa Bariadi hawajawahi kumwandalia sherehe Chenge. Yeye ndiye amekuwa akiaandaa hizo sherehe kama wafanyavyo wabunge wa CCM kwani hiyo ndiyo huitwa takrima !
 
JE ?NEC imekwisha ?mbona JK alikuwa mpirani?
Naona kuwa sidhani kama kikao kimekuja na lolote la maana ama jipya.
 
Something is going to happen soon here in Dodoma stay tuned.


ANDREA!mwana wa chenge! nimekukosea nini mimi taifa lako? nimekusomesha hadi ndani na nje, nikakupa kiti cha enzi uweze kuwahukumu wenye haki na wakosefu, ukaamua kujilimbikizia mali za yatima na wajane! nimekukosea nini mimi taifa lako?

nikakupa wadhifa mkubwa kuwatetea hawa maskini wangu, ukaamua kuchukua chakula chao ukajilisha mwenyewe na kingine ukawatupia mbwa, nimekokosea nini mimi taifa lako?

ukaamua kuasi na kuuma mkono wako wa kulia! ukaamua kuungana na beel-zebul, ukaniasi mimi niliyekulisha ukanawiri.

tazama sasa nimekuacha! beel zebul ameamua kukuumbua, tazama sasa nimekuacha, nimekuacha uabike!

beel-zebul=shetani mkuu
 
Waungwana,

Kipi kilichomfanya Mkapa aone umuhimu wa 'kurudi tena kwenye siasa' na hatimaye kuhudhuria kikao cha NEC? Kama mtakumbuka aliwahi kutwambia Watanzania kwamba yeye ameshastaafu siasa hivyo tumsimsumbue na mambo ya siasa.

Huyu jamaa alidhani ameshajiset kimaisha kwa ufisadi mkubwa alioufanya alipokuwa Rais na mkataba aliousaini kati ya 'kampuni yake' ya KCP na TANESCO wa shilingi bilioni 326 ambao unamwingizia kwa siku shilingi 146 millioni. Hivyo akajua siasa hana haja nazo tena maana atakuwa busy na 'mabiashara' yake ndani na nje ya nchi.

Kufuatia pressure kubwa kutoka kwa waandishi, Watanzania na hata baadhi ndani ya CCM ameanza kuwa na wasi wasi mkubwa kwamba chochote kinaweza kutokea na yeye kufikishwa mahakamani na pia kufilisiwa kutokana na ufisadi huo.

Je, Mkapa 'kuonekana tena katika anga za kisiasa' kutamsaidia katika juhudi zake za kuwazuga vigogo wa CCM na Watanzania kwa ujumla dhidi ya ufisadi mkubwa alioufanya akiwa Rais?
 
Fine!

Kama substance zilizotumika ku_infect viti vya wabunge etc ndani ya nyumba ya bunge... Ni SCIENTIFIC...Tupeni report zozote za toxicologist..au Chemists...waliotinga hapo bungeni ..for sampling!

Kama sio sangoma thing....tunategeme sana kupata fununu ..za analisis za chemicaly zilizotumika zikifanyika....either kwenye hospitals au maabara acredited..kama za chuo kikuu..au mkemia mkuu..!
 
kuna uhakika gani kuwa ni uchawi?hizi ni blah blah
Of course, naomba kuwasisitiza wana JF kufikiria mbali zaidi. Hakuna uchawi, kuna kitu inatumiwa na inaua taratibu na mwisho mlengwa anakuwa ndio hivyo tena.

Tatizo kubwa ni kuwa sidhani kama kuna wataalam wa kuigundua hii kitu ikitokea imetumiwa na watumiaji wa kitu hii kutekeleza azma zao naamini wanajulikana japo yawezekana wanalindwa. Ni watu hatari kwa taifa letu na wa kuepukwa kwa nguvu zote. Wale wanaodhani hilo halipo Bongo basi niwahakikishie LIPO na tena wanajitahidi kuhakikisha watu mnaamini kuwa ni uchawi tu na ikiwezekana kukatokea lolote msahaulishwe na walengwa wawe wanaishia taratibu tu.

Beware!
 
Sawa uchawi upo maana hata biblia inakiri hivyo. Lakini kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti tunavunja nguvu ya matunguli au kila aina ya madawa ya uovu ili kuendeleza mtandao wa ufisadi. Tunaamini Mungu yupo upande wetu na mwisho tuta rise tukiwa washindi.
 
Back
Top Bottom