Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

Mkuu mambo ya siasa siku zote ni historia, tumeuona Amina Chifupa(RIP), akitishiwa kwa kutaka uenyekiti wa vijana, the next thing we know amekufa kwa sababu isiyoeleeweka, sasa leo ulitegemea nini viongozi wetu wawe wajinga kuupanda tena mkenge wa Chenge?

Mkuu ukweli ni kwamba viongozi wetu ni sisi wenyewe, juzi tumesikia mtoto anakula kichwa cha mtu, ndivyo tulivyo amesema mkulu wangu Nyani, mimi siamini uchawi lakini gari langu nalifunga na funguo, maana sina noma kwenda Bagamoyo, maana nasikia huko kwenye uongozi wa juu ni lazima ifahamike kua na wewe huwa unaenda kwa hiyo kabla ya kwenda ni kutangaza kuwa unaenda, na kuzunguka tu pale Bagamoyo mjini na kurudi inatosha,

Viongozi wetu na sisi wananchi wote ni washirkina period!

Mkuu hapo nilikobold umenivunja mbavu mkuu.

Ila komandoo,haya madataz yako ni kama ile machine ya hiroshima maanake najua hata akina Chiligati wana-doubt kazi zao za propaganda maanake hadi sasa mkulu umetupatia madesa ya nguvu.Akionekana kwenye Tv sa hivi akifanya spinning ataishia kuonekana Ze comedy,halikadhalika Salva Rweyemamu
 
Watu waliliona kabla muungwana hajapata madaraka kuwa ataweka nchi katika auto pilot wakataadfhalisha hali mbaya na mparanganyiko ndani ya ccm, tusubiri tuone uteuzi wa 2010 itakuwaje maana najua kuna watu wengi wanaonekana kama wana moyo wa kimapinduzi wataachwa na utakuwa mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
Nakuaambia Muungwana atakapotoka katika urais CCM kwisha.Waliobakia sasa hivi sijui nani atakaesimama na kusema yeye ni safi? Pengine akina Anne Kilango,Mwakyembe na Rose Migiro.Bernard membe na Jk lao moja tu.

Wakati huo opposition kuna akina Dr Slaa,mashujaa wa taifa
 
Ag,

Mimi naomba nitofautiane na wengi, nadhani taifa letu linapitia kipindi kizuri sana kwenye uhai wake... kwa hakika hiki ndio kipindi cha kimapinduzi kweli... yaani ya kifikra, kiitikadi na kidemokrasia... hii ili itokee lazima equilbrium ile disturb kidogo... na hili ndilo lililotokea..

Si muda mrefu tulikua tunakasirikia CCM kutoambiana ukweli, sasa hivi demokrasia ndani ya CCM inakuwa sana... na kwa kweli kama watu wako imara kuamua hata katibu mkuu aondolewe... hii ni demokrasia ya hali ya juu...

Mimi nadhani CCM inajiweka mahali pazuri kuliko tunavyodhani wengi wetu.

Na kwa kweli wana mwenyekiti mpenda demokrasia.... kama Mh. Ben Mkapa angekuwa anaruhusu mijadala wazi kwenye uenyekiti wake haya tunayoyaona leo tusingeyaona... sasa tusubiri next CC meeting kitu kitakachojiri

Mwisho: Come 2010 mutaona jinsi wafanya biashara wengi... watakavyoamua kutogombea... tusubirini pia mtakavyoona Dar es Salaam kutavyoanza kuwa na wabunge wa kweli... wala sio bora wabunge kama ilivyo sasa!

'Demokrasia' tunayoiona CCM sio genuine,ni ya kulazimishwa.Yote yalianza na Tume ya Mwakyembe.Baada ya hapo ndio ujasiri ukajipenyeza.Mi namiini kabisa kuwa kuna wabunge ambao kweli waliweka maslahi ya wananchi wa majimbo yao mbele na kuna wale ambao wana hasira kwa kukosa mshiko wakati wa kampeni baada ya kugundua kuwa kila mbunge wa CCM angeweza kupata msaada mkubwa wa kipesa toka kwenye chama kulingana na pesa walizochota kwenye coffers za serikali.Lakini pesa zilienda to the chosen few
Ukweli ni kwamba ni mwelekeo mzuri,ingawa mazingira yake ni ya matata.
Siasa za kulindana finally zimefika ukingoni,kwa sababu within, wenyewe wamegundua kuwa kuna wale wenye nacho na wale wasiokuwa nacho.Wenye nacho wamesambaratishwa,therefore wale wasiokuwa nacho sasa wanaweza kunyoosha,bila ya kunyooshewa kidole, kusimama na kusema...
 
Mama Malecela amepigwa bit , ngoja tuone kama atarudia aloyatamka huko nyuma kwa ujasiri wa awali.

Tuiangalie CCM vizuri na si kwa wepesi. Hawako wepesi kiasi tunachoaminishana hapa wazee
 
Mkuu mambo ya siasa siku zote ni historia, tumeuona Amina Chifupa(RIP), akitishiwa kwa kutaka uenyekiti wa vijana, the next thing we know amekufa kwa sababu isiyoeleeweka, sasa leo ulitegemea nini viongozi wetu wawe wajinga kuupanda tena mkenge wa Chenge?

Mkuu ukweli ni kwamba viongozi wetu ni sisi wenyewe, juzi tumesikia mtoto anakula kichwa cha mtu, ndivyo tulivyo amesema mkulu wangu Nyani, mimi siamini uchawi lakini gari langu nalifunga na funguo, maana sina noma kwenda Bagamoyo, maana nasikia huko kwenye uongozi wa juu ni lazima ifahamike kua na wewe huwa unaenda kwa hiyo kabla ya kwenda ni kutangaza kuwa unaenda, na kuzunguka tu pale Bagamoyo mjini na kurudi inatosha,

Viongozi wetu na sisi wananchi wote ni washirkina period!

Hapana, Mkuu! Tunaendekeza tabia hii. Mtoto kumchinja mwenzie na kubeba kichwa chake ni ishara ya matatizo ya akili na sio u sangoma. Dalili za jamii kuendekeza usangoma ni kumkamata mama yake ati naye anashirikiana kula watu! Chifupa aliugua akafaraki. Hakuna kigeni. Isipokuwa kwa vile alitishia kushirikiana na dola kuwafichua wauza unga, tumekimbilia kuona mkono wa mtu.

Kwenye hii sakata ya Chenge nayo vile vile. Huyo Chenge kama kweli ni mlozi, alikuwa na haja gani ya kuongozana na afisa wa bunge? Au tunataka kusema kuwa tunguli zilikuwa nzito kiasi ya yeye mwenyewe kushindwa kubeba! Kama ni kumuonyesha wanapokaa victim watarajiwa, kweli Mheshimiwa mbunge mwenye nia mbaya alishindwa kusubiri wakati wa kikao na kunukuu sehemu walimoketi walengwa wake? Halafu tunaambiwa kuwa huyo huyo, msomi wa Harvard alienda kufanya uchafu huu akijua kuwa kamera zimezimwa! Hata mimi nisiyefika huko Harvard najua kuwa security cameras zimewekwa kunasa vitendo vinavyotendeka wakati wenyewe hawapo! Kwa vile tunapenda conspiracy theory hakuna maelezo tutakayokubali yasiyohusisha uMafia (ineptitude one at that) au ulozi. Hatujiulizi ni dawa au kemikali gani unayoweza kupakaa kwenye kiti ikaja mdhuru mtu masaa 12 baadae? Hata warusi na wabulgaria ilibidi wawakaribie walengwa ili ku'administer' sumu zao. Hapana, Mkuu, siwezi kuwazuia kujadili lakini mimi hamja ni'convince' kuhusu hoja yenu.
 
Fundi Mchundo,

..kama hizo "video" zinazomwonyesha Chenge akifanya hayo aliyokuwa akifanya zingesambazwa mitaani tusingekuwa tunauliza maswali yote haya.

..mambo yangekuwa mswano kwelikweli manaake wananchi tungewatolea macho polisi, CCM, na serikali nzima kuona watachukua hatua gani.

..natumaini waliotuletea hizi "dataz" watakuwa wamejifunza kutokana na "tukio" hili.
 
Mkuu Kasheshe,

Najua siku zote una tatizo na malecela, lakini subiri kimbunga kinakuja mafisadi hawawezi shinda nguvu ya wananchi, wamemchokoza mama, sasa kimbunga kinakuja wallahi atalia mtu, fasten your belt mkuu tena ninatabiri kuwa by the end of this week huenda akalia mtu huko bungeni watch......!
 
Mkuu unajua mimi huwa sipendi kuzunguka mbuyu, Data za uchawi zilitolewa kwanza hapa JF, na Enigma na mimi nikaziunga mkono kuwa ni za kweli 100%,

Baadaye mimi nikasema kuwa Mwakyembe ameathirika na huo uchawi sasa anenda Dar kuchekiwa hali yake kiafya, kesho yake Spika wa bunge letu akathibitisha kuwepo kwa video, kikao cha nec kikajaribu kuyeyusha, jana Spika amewapa wanaohusika masaa 72 kumpa matokeo,

video hata ikiwepo, haiwezi kuwekwa mitaani hayo mawazo ni ulofa wa akili kuwa nayo, kama sio uwezo mdogo wa kufikiri, mjifunze kujadili ishus bila ubinafsi, kwa kufikiria kuwa ndani ya hii forum kuna wananchi wengine pia sio wewe tu mtu mmoja mwenye kubadili majina kila kona ya hii forum, huo ni ubinafsi tena ni u-selfish ambao hauwezi kutusaidia kama taifa,

Unapojadili topic hapa JF jaribu kuwaheshimu na wengine, na ukishindwa ishu kubali ili watu wasonge mbele na ishus zingine, kama tusingewawahi kina Chiligati wasingesema kabisa kuwa kuna hiyo ishu period, watu wengine mnaonekana kuwa hapa sio mahali penu wakuu, kwa sababu siwezi kuamini kuwa kuna m-Tanzania mwenye akili timamu anyeweza kuamini kuwa CCM wanaweza kuruhusu video yenye kuonyesha Change akiweka something kuonyehswa to the public!

Man just grow up and stop being a crying baby, magazeti yote yaliyosema kuhusu hii ishu hayawezi kuwa yanamilikwa na sisi tulioanza kuuweka huu ujinga hadharani!

Ahsante Mkuu
 
Mkuu Kasheshe,

Najua siku zote una tatizo na malecela, lakini subiri kimbunga kinakuja mafisadi hawawezi shinda nguvu ya wananchi, wamemchokoza mama, sasa kimbunga kinakuja wallahi atalia mtu, fasten your belt mkuu tena ninatabiri kuwa by the end of this week huenda akalia mtu huko bungeni watch......!

They are rattling the snake,wataumwa! From there guys watakua serious na kujua kweli Tanzania ina watu wenye kiu ya haki.

Tingatinga hapa nae atakua anawashika pabaya hadi atakapomfikia Muungwana mwenyewe.Maanake wale walikua wanamhujumu kipindi kile cha election karibia wote yamewakuta.Bado akina Muungwana na wenine wachache
 
Kama watanzania wenzetu wamesharogwa...Sisi tulioko Nje ya nchi BADO!

Ndugu zangu wazalendo tuwe makini kwani pesa ni nyingi walizoiba,umafia wanaujua na CCM wanalicheza TAIFA NA WATU WAKE...
Haya mambo ya KIKWETE NA LOWASSA KAMA MAFIA WAKUU WAKISAIDIWA NA MAGAIDI WENZAO WENYE RANK ZA JUU NDANI YA CHAMA TAWALA...WANATUCHEZA AKILI AMA KUTUFANYA MISUKULE...

Lowassa si alishasema mbele ya kikao chao cha KIMAFIA kuwa alimshauri TOP Mafioso KUWA RICHMOND NI UTAPELI?
Kwanini Kikwete hakusimamisha mkataba wa RICHMOND licha ya kwamba alikuwa anajua?
Kwanini hakusimamisha malipo HEWA ya EPA ambayo kutokana na wingi wake ni LAZIMA ALIKUWA NA TAARIFA?
KWANINI BALLALI HAKUWAHI KUTAJWA KAMA MTUHUMIWA LICHA YA KWAMBA ALIHUSIKA DIRECTLY NA HUKU AKIJIGAMBA NI PESA ZA IKULU?
Wapi hao wasaidizi wao ambao walisaini documents wakampelekea na yeye kusaini na kuwarudishia huku kukiwa na udhibitisho wa saini na barua kuwa serikali ilitaka pesa hizo ziltolewe KIMAFIA? Kina DEP,DDDD,DF, Director of Supervisions...HAWA MAFIA WANAWAACHA MAFIOSO MAFISADI WENZAO KWENYE KAZI ILI WAWAUWE WATU,KUWATISHA NA KUHARIBU USHAIDI!
JOHNSON MWANYIKA ambaye ni kinara wa UMAFIA wa RICHMOND NDIYE ALIYEWEKWA KUWACHUNGUZA WALIOHUSIKA NA EPA...Wanafikiri sisi ni wajinga kiasi hicho?
Wakamweka Zitto ndani ya KAPU LA UFISADI na sasa shombo EVERYWHERE!
JE TUTAFIKA?
 
Makala hii ya BUBU iliyotoka kwa MPAYUKAJI HOVYO INAMAKE SENSE KUWA SASA MAFIOSO WA CCM WAKO KAZINI KUJISAFISHA WAKIWATUMIA WAKUU WAO MAFIOSO MAFISADI WAKIONGOZWA NA DON KIKWETE KWA KUSAIDIWA NA KAPTEN MAKAMBA....

HIVI NANI ASIYEJUA KUWA SERA ZA CCM NI NZURI ILA IMETEKWA NA MAFIA?
NI UMAMUZI WAO KUSUKA AMA KUNYOA KWASABABU UMAFIA WAO TUMESHAUONA NA UFISADI WAO WA KISANII UPO UKINGONI?
Lowassa na Kikwete ni mafisadi wanaotaka kutuchezea akili....
NARUDIA TENA...HAWA WATU WALIENDA KWENYE KABURI La mwalimu huko musoma kuitambikia CCM kwasababu wao wanaaamini ni balaa za MWALIMU!
Wakagundua kuwa UCHAWI ndio nguzo muhimu ya kuendelea nayo kuwapumbaza wabongo!

NYIE WATANZANIA WENZETU NA WABUGE UJUMBE WANGU NI HUU....KAMA NYIE MMESHAROGWA..SISI BADO...IRUDISHENI SERIKALI KWA WANANCHI TUANZE UPYA...NA KAMA HAMUTAKI NI BORA MUGAWANYE NCHI KWASABABU SI WANANCHI WOTE WALIOROGEKA!
KILIMANJARO,ARUSHA NA KWINGINEKO BADO TUKO FITI NA CCM IKITAWALA NI BORA NCHI IGAWANYE KATI YA WAZALENDO NA MISUKULE ILI KILA MTU AUBEBE MSALABA WAKE!
WANANCHI WENGINE TUMESHACHOSHWA!

NEC imeamua kuwa chaka la mafisadi?

Nkwazi Nkuzi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

TAARIFA kwamba Waziri Mkuu mfukuzwa, Edward Lowassa, hakuwa na hatia bali alijiuzulu kuwajibika, ila hakuhusika katika kashfa ya Richmond, ni upuuzi wa mwaka.

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) iliyokutana hivi karibuni ilitoa tamko hili la kuchusha na kukera kama lilivyokaririwa na vyombo vya habari.

Inashangaza na kukatisha tamaa kama chama kinachojidai kupigania masilahi ya Mtanzania kikiimba wimbo wa maisha bora kinaweza kuja na upuuzi kama huu! .

Kama hakuhusika na kashfa ya Richmond ni kwanini alijiuzulu? Je, ina maana taarifa nzuri ya kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe ni upuuzi?

Je, kitendo cha NEC si kulidharau na kulitukana Bunge na kulionyesha kama taasisi inayosema uongo? Je, Bunge limechukuliaje shambulio na kashfa hii? Kama Lowassa hakuhusika na Richmond, alijiuzulu kwa kosa gani au kashfa gani? Huu ni uchovu wa kisiasa usio na mfano. Huu ni mwanzo wa kifo cha CCM!

Badala ya Kamati Kuu ya CCM kufanya kazi za umma ilifanya kazi ya kusafishana. Na hii si mara ya kwanza kwa CCM kufanya hivyo. Mwanzoni akina Lowassa na wenzake walitaka kuitumia Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) .
Nayo bila tahadhari wala kuona mbali ilijaribu kuwasafisha mafisadi hawa bila mafanikio hadi Bunge lilipoamua kuunda kamati iliyoweka historia ya kuwa Bunge la kwanza katika Afrika kumtimua mkuu wa shughuli za serikali bungeni, waziri mkuu.

CCM imekuwa ikipewa kila aina ya majina mabaya kutokana na maamuzi yake mabaya yaliyojikita kwenye kulindana na kubabaisha. Hivi ni Mtanzania gani awe hata mwanachama wa CCM damu asiyejua kuwa Lowassa alifukuzwa kazi na hakujiuzulu? Ni nani hajui kuwa kilichomfukuzisha Lowassa ni ufisadi wa nyuma ya Richmond? .

Kuna siku CCM watakuja kutwambia kuwa Tanzania ni nchi iliyoendelea. Maana wanaweza kujipayukia lolote kana kwamba wanawaambia ‘mataahira’! Baya zaidi wanapodanganya wanajidanganya na wao pia!

Kama tamko la NEC halitatenguliwa, basi hakuna siri, aliyosema Mwalimu Nyerere yanatimia. Mwalimu aliwahi kuionya CCM juu ya kuvamiwa na wafanyabiashara. Wakati ule tulijua wafanyabiashara, tusijue ni mafisadi.

Je, Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete anapotuambia ana azima ya kupambana na ufisadi ilhali akikalia kiti kwenye kamati inayopitisha upuuzi na baraka kwa mafisadi, tumweleweje? .

Tunaambiwa kuwa hata waziri Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, hawakuwa na kosa! Mbona Msabaha aliiambia Kamati Teule ya Bunge kuwa Richmond ulikuwa mradi wa waziri mkuu wa wakati ule na Mwarabu wake? Kwa nini NEC wamesahau kuwa yaliyoandikwa huwa hayaozi (scripta manenta)?

Kama CCM itashikilia upuuzi huu ningeishauri tume teule ya Bunge na Bunge lenyewe kwenda mahakamani kupinga dharau hii na matusi kwake.

Kama Lowassa na wenzake hawakuwa na hatia wala kushiriki kwenye uchafu wa Richmond, basi NEC ituambie nani wako nyuma ya Richmond. Au ni yale yale kuwa Richmond inafutikwa chini ya busati kuepuka kumtaja mhusika wa kweli aliyeiidhinisha? Je, Watanzania nao kwa upande wao watakubali kugeuzwa mabwege kiasi hiki ilhali kila kitu kiliwekwa wazi mbele yao na kamati teule ya Bunge? Enyi Watanzania ‘wapumbavu’, nani aliwaroga hadi mkaaminishwa kuwa Lowassa na wenzake hawakuwa na hatia bali waliwajibika? Mbona Lowassa na wenzake waliwekwa ‘uchi’ mbele zenu mkajionea na kusikia kila kitu! Namna hii inatisha na si vibaya kusema: Sasa, rasmi CCM imeikabidhi nchi kwa mafisadi .

Tuliwahi kuonya kuwa CCM, kwa sasa ina ombwe la uongozi wenye akili timamu. Tulionya kuwa uchafu wa wakuu wa CCM utaiangamiza nchi. Kweli kama Lowassa hahusiki na Richmond, ni kwa nini ametupwa nje? Je, hii inaweza kuwa janja ya kumsafisha ili arudishwe kwa mlango wa nyuma? Je, uswahiba wake na Kikwete umeshinda hata haki? Je, akirudishwa, Watanzania watamkubali na kumpokea? Maana, kupitia wapambe na ‘waganga’ wake aliwahi kukaririwa bila hata chembe ya aibu akijilinganisha na mzee Ali Hassan Mwinyi aliporejea kwenye siasa na kuwa rais baada ya Wizara yake ya Mambo ya Ndani wakati ule kukumbwa na kashfa ya mauaji ya kina Nzegenuka .

Hivi karibuni Katibu Mwenezi wa CCM, John Chiligati, alikaririwa akipindisha maneno ya tume teule ya Bunge kuwa waziri mkuu wa zamani Lowassa, apime na kuamua la kufanya. Baada ya Lowassa kupima aliamua kujiuzulu. Je, huyu kama aliamua mwenyewe kujiuzulu kama tunavyoaminishwa, hii si ishara ya kukiri kuwa alifanya makosa? Kinachonichefua zaidi ni ile hatua ya NEC kuwamwagia sifa mafisadi shutumiwa waliojiuzulu kuwa walikiletea heshima chama hicho! Je, maana yake hii ni nini? Au ni yale kuwa Lowassa aliamua kuachia ngazi ili serikali yote isianguke? Kama Lowassa aliubeba msalaba wa serikali chafu inayonuka, basi iwe ni kwa faida ya walioko nyuma ya kashfa hizi na si kuwahadaa Watanzania kuwa Lowassa na wenzake hawakuwa na makosa .

Kama CCM ingekuwa ni ile ya Nyerere, Lowassa na wenzake walipaswa kufukuzwa kwenye chama hapo hapo na kuchukuliwa hatua za kisheria, badala ya kumwangiwa sifa za uongo na NEC. Kama kuna kitu kimefanywa na NEC kwa kuwatetea na kuwapongeza kina Lowassa, si kingine bali kuonyesha sura halisi ya Kikwete, wenzake na CCM.

Kinachoonekana hapa ni kwamba CCM sasa ni chama cha mafisadi. Kinachojibainisha hapa ni kwamba pesa iliyoibwa na hawa watu na washirika wao si chochote, isipokuwa ushindi kwa CCM! Je, CCM imewapongeza hawa mashujaa wake kutokana na kazi yao njema ya kulihujumu taifa ili CCM ishinde kupitia takrima? .

Kama si hivyo, sasa ni nini kilichoishawishi kamati kuu kufanya upuuzi wa mwaka? Je, wajumbe nao walihongwa kiasi cha kuja na usanii huu usioingia akilini?

CCM sasa inafikia ukingoni. Katika kikao hiki cha NEC, tunaarifiwa kuwa kulikuwa na mgawanyiko. Wana CCM safi walitaka mafisadi wasulubiwe huku wakubwa wao wakiwapinga. Je, wadogo walilazimishwa na wakubwa kuridhia upuuzi huu? Je, NEC imeamua kutoa taarifa yake na si ya wajumbe? Maana hatujaambiwa jinsi walivyofikia kutoa tamko hili hatari kwa nchi na hata kwa chama chenyewe

Je, wale wana CCM safi watakubali kuburuzwa na kuonekana wasaliti kwa taifa lao kwa kuogopa wakubwa wao? Je, tutegemee nini? Wapo watakaojitenga na CCM kuhakikisha haki inatendeka au nao watageuka wanafiki na wachumia tumbo kiasi cha kukubaliana na jinai hii? Hata kama CCM itazika tofauti zake kwa ujanja au nguvu, ukweli ni kwamba ina nyufa nyingi kiasi cha kushindikana kuzibwa. Na hili likiongezewa na kuwa na uongozi mgando usio na visheni wala udhu, siku za CCM zinaanza kuhesabika .

Kama imeweza kutekwa na kushindwa na kundi la wahalifu wachache, kweli kitaweza kupambana na changamoto za kuendesha taifa kubwa kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia, ambapo kashfa za wateule wake zinavujishwa kwenye mitandao kila uchao? Je, huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM? Nani anajua? Tuhitimishe: Taarifa ya Kamati Kuu ya CCM ni matusi na kejeli kwa Watanzania. Inapingana na anayotuaminisha kila uchao Rais Jayaka Kikwete na mwenyekiti wa CCM. Hakika chama hicho kimegeuka chaka la ufisadi .

Je, kwa CCM hii ya mafisadi tutaweza kuushinda ufisadi na kuwaletea Watanzania maisha bora? Kama CCM inataka kurejea kwenye uchaguzi ujao, basi badala ya kuwasafisha mafisadi, ije na hoja ya kuwabana warejeshe pesa yetu na kushitakiwa kwa ufisadi.

Isiharibu ushahidi utokanao na kuwajibika kwao. Na kama kuna ndoto ya kumrudisha kwenye ulingo wa siasa yeyote kati ya wale tuliokwisha kuwatimua, ijulikane ni ndoto ya mchana

KAMA CCM WALIMPUUZIA MWALIMU NA KUWAWEKA MAADUI WAKUBWA WA WATANZANIA AMBAO NI MAFIA WALIOKITEKA CHAMA KWA KUSAIDIANA NA MAFIOSO MKAPA ALIYEAMINIWA NA MWALIMU PAMOJA NA WANANCHI...THEN WAMELIWA?
MWALIMU ALIKATAA KABISA KIKWETE NA LOWASSA...MITAMBIKO NA MISAMAHA WAKATI YUKO KABURINI HAIFANYI KAZI TENA....RUDISHENI NCHI KWA WANANCHI LA SIVYO NCHI IGAWANYWE NA MISUKULE WAENDELEE NA MABOSI WAO WACHAWI NA SISI WAZALENDO TUENDELEE KUIJENGA NCHI KWA KUPITIA USHIRIKIANO NA WALE WANANCHI AMBAO UCHAWI BADO HAUJAWAPUMBAZA ILI TUPATE MAHALI PA KUANZIA KUIKOMBOA NCHI!
MKITEGEMEA KIKWETE AFANYE KITU NI SAWA NA KUTUMBUKIA CHOONI HUKU UKITEGEMEA MSAADA WA KUJA KUTOLEWA...Tatizo hapo ni kuwa ukishatumbukia chooni hata ukitolewa huko bado akili zako zitakuwa FYATU!
 
Mkuu Kasheshe,

Najua siku zote una tatizo na malecela, lakini subiri kimbunga kinakuja mafisadi hawawezi shinda nguvu ya wananchi, wamemchokoza mama, sasa kimbunga kinakuja wallahi atalia mtu, fasten your belt mkuu tena ninatabiri kuwa by the end of this week huenda akalia mtu huko bungeni watch......!

Mkuu Field Marshall ES,

Heshima mbele!

Sina hakika kama ulikuwa unani-address mimi, au umetumia jina langu tu kufikisha ujumbe!

Sijawahi hata siku moja kuwa upande tofauti na Mzee. JSM na wala Dada Mh. mama Anne K. Malecela...

Naomba kama waweza niwekea hiyo post... ingenisaidia nami kujifunza...
 
They are rattling the snake,wataumwa! From there guys watakua serious na kujua kweli Tanzania ina watu wenye kiu ya haki.

Tingatinga hapa nae atakua anawashika pabaya hadi atakapomfikia Muungwana mwenyewe.Maanake wale walikua wanamhujumu kipindi kile cha election karibia wote yamewakuta.Bado akina Muungwana na wenine wachache

JSM is bigger than that....sidhani kama ana issue na Muungwana! Kama ungelimjua he is humble and principled man! Hana haja ya kumfikia Muungwana....Amefanyiwa mangapi na 'hajarudisha'.....hao wanaofanya 'madude' hawana upeo mrefu....na huwa wanarudi pale pale...na yeye huja kuwakwamua....wengine huwaachia waozee huko!!
 
Field Marshal ES said:
video hata ikiwepo, haiwezi kuwekwa mitaani hayo mawazo ni ulofa wa akili kuwa nayo, kama sio uwezo mdogo wa kufikiri, mjifunze kujadili ishus bila ubinafsi, kwa kufikiria kuwa ndani ya hii forum kuna wananchi wengine pia sio wewe tu mtu mmoja mwenye kubadili majina kila kona ya hii forum, huo ni ubinafsi tena ni u-selfish ambao hauwezi kutusaidia kama taifa,

FMES,

..hii ishu inanikumbusha yule Waziri wa Liberia ambaye picha zake za ngono zilisambazwa kwenye magazeti na internet.

..kuna watu walim-comfront Waziri yule kuhusu "katabia" kake akabisha. baada ya hapo ndiyo picha zake zikamwagwa kwenye public domain.

..THERE IS NO MORE POWERFUL EVIDENCE THAN ONE THAT IS VISUAL. hicho ndicho kinachonifanya mimi niseme lets have the videos up and close the deal.

..kukubali ati CCM hawawezi kuruhusu hizo video ziwepo mtaani inamaanisha tumesalimu amri kwamba hatuwezi kuwaondoa madarakani.

NB:

..mengine uliyoyasema nadhani hayana nafasi hapa JamboForums.

..siamini kwamba kutofautiana kwetu ktk jinsi ya kuli-approach suala hili, kunahalalisha kuitana majina ya ajabu-ajabu.
 
Bunge Likivunjwa Na Serikali Kurudishwa Kwa Wananchi Tutajua Mengi Tu!
Top Mafioso Don Kikwete Akisaidiana Na Kapten Makamba Hawatakuwa Na Kazi Na Hapo Tutaanza Upya Na Ukweli Kujulikana!
Narudia Tena...la Sivyo Nchi Ipigwe Panga Na Misukule Waendelee Na Owners Wao Na Wazalendo Tujipange Kuirudisha Nchi Yote Mikononi Mwa Wananchi!
Mimi Niko Radhi Kuingia Msituni Walahi Vile!
 
Jmushi 1,

Mbona unakuwa unaongea vitu vingi kama huko ndotoni ? Vitu unavyozungumza havi-make sense kabisa umenikumbusha jamaa mmoja anaitwa Munishi ambaye alivamia BCS kipindi fulani tukamfukuza.
 
..THERE IS NO MORE POWERFUL EVIDENCE THAN ONE THAT IS VISUAL. hicho ndicho kinachonifanya mimi niseme lets have the videos up and close the deal.
..kukubali ati CCM hawawezi kuruhusu hizo video ziwepo mtaani inamaanisha tumesalimu amri kwamba hatuwezi kuwaondoa madarakani.

Mkuu ninachosema ni kwamba wewe ni mtu mzima na una akili timamu, ninataka kuamini kuwa ni m-Tanzania kama mimi, sasa siasa huwa inaongelewa na history behind it, sasa naomba uniambie ni lini Tanzania tumewahi kuonyeshwa kiongozi wa juu akifanya ufisadi katika video? Je tulionyeshwa video ya mzee wa vijisenti, alipokwenda kuweka hela New Jersey USA? Sasa ina maana hana hizo hela huko kwa sababu hatujaona video au visual evidence? Lakini unafikiri kuwa hazipo?

Ni wapi tumeonyeshwa visual evidence ya lowassa na Richimonduli? Sasa ina maana kwamba hahusiki kwa sababu hakuna visual evidence? Spika wa bunge amesema wazi kuwa kuna video camera sita, tano zilikuwa zimezimwa lakini moja ikawachukua watu wawili, mmoja ni ofisa wa bunge, mwingine ni mbunge, Chiligati amesema wazi baada ya kubanwa sana kuwa mwingine kwenye camera ni waziri mmoja wa zamani,

sasa with all this evidence wewe bado unalilia visual evidence tuuuu, sasa hii ina raise some questions kwamba exactly unachotaka ni nini hasa kama sio ubinafsi? Kona zote za bongo sasa wananchi wanaongelea iwapo alichokiweka mle kwenye viti ni uchawi au sio lakini hii ya kuwa alikwenda kweli wananchi walishaaipita siku nyingi mkuu, wakati mwingine kama huna uhakika na ishus ni vyema basi kusoma alama za nyakati bro!
 
video hata ikiwepo, haiwezi kuwekwa mitaani hayo mawazo ni ulofa wa akili kuwa nayo, kama sio uwezo mdogo wa kufikiri, mjifunze kujadili ishus bila ubinafsi, kwa kufikiria kuwa ndani ya hii forum kuna wananchi wengine pia sio wewe tu mtu mmoja mwenye kubadili majina kila kona ya hii forum, huo ni ubinafsi tena ni u-selfish ambao hauwezi kutusaidia kama taifa,

Unapojadili topic hapa JF jaribu kuwaheshimu na wengine, na ukishindwa ishu kubali ili watu wasonge mbele na ishus zingine, kama tusingewawahi kina Chiligati wasingesema kabisa kuwa kuna hiyo ishu period, watu wengine mnaonekana kuwa hapa sio mahali penu wakuu, kwa sababu siwezi kuamini kuwa kuna m-Tanzania mwenye akili timamu anyeweza kuamini kuwa CCM wanaweza kuruhusu video yenye kuonyesha Change akiweka something kuonyehswa to the public!

Mkuu! Kebehi ya nini? Kuna tatizo gani kuweka video katika public domain kama haihatarishi usalama wa nchi? Hapa tunazungumzia video ya chumba kinachoonyeshwa kila siku kwenye luninga kwa hiyo hilo suala la usalama halipo. Kuendekeza usiri ndiyo mara nyingi unatuletea matatizo na si vinginevyo. Tatizo lako ni kuwa unataka kutuaminisha wote kuwa video inaonyesha kuwa Chenge anaweka kitu wakati hakuna ushahidi isipokuwa hearsay! Mbona wakina Anna Abdallah wamesema kuwa alikuwa akionyeshwa sehemu ya kukaa? Au mwenzetu unataka kutuambia kuwa ulishuhudia hicho kitendo cha Chenge? Au uliiona video? Hapa tunabadilishana mawazo na kila mtu ana haki ya kuwa na ya kwake kama ilivyo kwako. Usitegemee hata siku moja kuwa wote tutadandia band- wagon ati kwa sababu Mkuu umeleta dataz. Wewe (na sehemu kubwa ya jamii) unaamini kuwa Chenge alikuwa anafanya usangoma, na ni haki yako kabisa. Mimi siamini (pengine niko peke yangu), na ni haki yangu kabisa. Tusitumie lugha za kutishana, kukebehiana kwa vile mtu mnatofautiana mawazo. Tujadiliane kiungwana na kama kuna kutofautiana mawazo, tukubaliane bali tuendelee kuheshimiana.
 
Back
Top Bottom