Kutoka Dodoma!

Kutoka Dodoma!

FMES,

..suala hili likiachwa limalizwe ndani ya Chama/CCM ukweli hautajulikana.

..kama kuna "kideo" kinachomuonyesha Chenge akinyunyiza hivyo vitu basi mjadala huu utasonga mbele vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa hivi.

..mimi nilifikiri mimi na wewe tuko upande mmoja, kwamba tunataka UKWELI usioruhusu mabishano ktk suala hili. ukweli huo ni "KIDEO" kinachomuonyesha Chenge na Ofisa wa Bunge.

..suala hili ni zito na wananchi tunahitaji ushahidi kamili na usiopingika/usio na mashaka ili kuchukua hatua zinazostahili.

..nimeuliza ni wabunge wepi wengine ambao viti vyao vilimwagiwa "vitu"? kwanini hao hawajulikani? ningependa kujua hali zao zinaendelea vipi tangu hiyo jumatatu? i thought that is a fair and reasonable question.

NB:

..hakuna mahali ambapo nimehoji nia yako hapa JamboForums. mimi wakati wote naangalia facts siangalii nia/motives.

..hivi Spika ndiye mwenye camera/tapes? kwanini magazeti hayamhoji yule mwenye access na cameras? kwani habari hii mtu wa kwanza kuitoa si ni cameraman?
 
Mkuu Mtanzania,

.........2. I do not care what, Chenge to me is a thug na wenziwe wote, ni wahuni tena ni vibaka wasiokuwa na class kabisa kama bin-adam wengine wote, ...............!

3. Taifa letu linakuwaje na viongozi wapuuzi kama Chenge? Tunakuwaje na viongozi wajinga wajinga kama Lowassa? ..............................I mean it a shame huyu alenda Europe kukagua hizo machine, alienda Malasyia na Kolimba, lakini walipotaka kwenda Houston kukagua ofisi na machine za Richimond kama sheria za serikali na jamhuri yetu inavyosema, na kutaka Msabaha kwa makusudi mazima ya ufisadi akawakataza kwenda huko huku akiwashambulia kuwa wanapenda sana safari ili wale hela za wananchi huku hakuna cha maana wanachokifanya, akitamba kwamba yeye anaijua sana Richmond ni kampuni safi hawahitaji kwenda huko, sasa najiuliza kwa nini hakuwazuia kwenda ile miji mingine? Na kwa nini aliwazuia kwenda Houston ambako ndio makao makuu ya Richmond? Na ilikuwaje Hosea akawasafisha kundi zima la Richimonduli!

.......................dawa ni kuwakamata na kuwalazimisha wao na familia zao walipie risasi za kuwatwanga mbele ya public, tena ikiwezekana pale Sanamu Monument, yes piga risasi tu, kwa sababu look what they are doing to us now? ...............................

Yaani hapa FMES ukanifurahisha zaidi uliposema

..........Halafu kumbuka kuwa akiwa Mwanasheria mkuu ameshiriki kwenye kuwafunga wananchi wangapi wasiokuwa na makosa kisheria, ingekuwa nchi za majuu sasa hivi kungekuwa na kesi kibao na lawsuits against serikali yetu kwa sababu ya Chenge, kwamba hana intelligent judgement au uwezo wa kutosha kufikiri kama binadam kamili, kwa hiyo wote alioshiriki kuwafunga kisheria wanahitaki kuachiwa, na mikataba yote iliyosainiwa china yake akiwa Mwanasheria mkuu itenguliwe mara moja!

Binafsi, sioni siasa ya chama hapa, ninachooona ni taifa kwanza hapa kuna wabunge am,bao wamepania na wako intact, ..........

FMES........maneno mazito sana hayo mwanawane.........heshima mbele
 
Kwa kweli we still have long way to go,kama mambo yenyewe yanaendeshwa hivi.Lakini tunasema one day yes..
 
aidha kuhusu wahusika sijui kama wameshachukuliwa hatua au bado wako mitaani wakitafuta jengine jipya ,tukumbuke tu hawa wengine walisikika kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa watafanya juu chini na wao kuondoka na watu ,hili wa kulaumiwa ni Mh.Kikwete na hata haya yanayotokea Bungeni Mh.Kikwete anahusika moja kwa moja kwa kuwaachia wahuni hawa kutembea kifua mbele na sasa wanakuja maungoni hata hawaoni haya maana si kweli kuwa mhusika hatambui kama kuna security camera zinafanya kazi lakini kiburi ndicho kilichompa nguvu na kudharau Serikali nzima , kwamba hata zikimchukua hawatakuwa na cha kumfanya zaidi ya makelele ya siku mbili tatu ,mtu huyu alitakiwa akamatwe mara tu baada ya kumaliza ushirikina wake na kupata usimgizi katika vituo vya Polisi pale Dodoma.
Je mlioko Dodoma huyu mtu ametiwa nguvuni au hakuna wa kumkamata maana si ajabu ukaambiwa hakuna ushahidi.

Uhaini mtupu!
 
".....Muongo na Mulozi ni watu wa kuchomwa......" by Franco Luambo Makiadi & OK-Jazz

Mkuu heshima mbele, marekebisho kidogo, si unajua zamani nilikuwa DJ yaani mzee wa mic na kukwaruza santuri, hii ngoma originally ilipigwa na Sam Mangwana, with a guest star Franco Makiadi.
 
Habari ambazo tumezipata kutoka kwenye TBC1; ambazo Katibu Mwenezi wa CCM ameonyeswa amezielezea ni kwamba... hilo jambop limejadiliwa kwenye kikao cha NEC. hata hivyo Katibu huyo mwenezi amesema... wanasubiria vyombo vya usalama viseme what happened... maana ndivyo vyenye authority!

Na maelezo ni kwamba huyo Mbunge ambaye sasa anatoka viti vya mbele vile vya mawaziri... na sasa anatakiwa kupatiwa kiti kingine kule back bencha alikuwa akipitishwa na wahudumu wa ofisi za bunge kuonyeshwa kwenye kikao hiki akae kiti gani...

Kwa maana hiyo basi ni jambo la kawaida kutafuta kiti... unalazimika kupitia kwenye safu mbalimbali na kuangalia kiti au sehemu ambayo ni muafaka kwako..

Kwa hili inaonyesha dataz za JF zimefungwa 3-0

Yani hapa sina mbavu. Na hivi ndivyo watakavyowapiga changa la macho watanzania. Interesting I see...! Na vipi mkuu kuhusu suala la Hosea kuonewa na kwamba ana kesi kubwa zaidi ya 5 amempa muungwana na muungwana hajazichukulia hatua yoyote kitu kinachomkatisha tamaa... Ataendelea na nafasi yake kama kawaida? 'Ataonewa sana na kudhalilishwa sana'?
 
Umesiliba vizuri nilitaka kumjibu,palipo na maslahi ya taifa unazi na ushabiki woote uwekwe nyuma.sasa hivi nchi hii inakoelea tutakuja kuzipiga kama majirani zetu tusipokuwa macho

Mkuu Yox2,

Heshima mbele bro, yaani sina la kuongeza, ila ubarikiwe kwa kuwa kama wakulu wangu Chuck D, na Mamen Flav Flavor, yaaani kwa kujua what time is!

Hizi sio saa za mchezo mkuu, yanayojiri Dodoma sasa hivi ni a total unofficial Civil War, ambayo imekosa silaha tu na kutangazwa rasmi, sasa watu wasifanye uhuni hapa au mchezo wa kuigiza, this is for real wandugu kwamba mafisadi wanataka the whole thing, halafu heshimu pia the effort za kutoa hizi dataz kwa sababu magazeti yetu yote bongo ninasema kwa jina la Mungu kuwa hawana hizi, na nimewaambia kuwa hizi wakae pembeni tu au waje wachote hapa tu, lakini sizitoi popote kwingine isipokuwa JF tu!

Ahsante Mkuu Yo Yo kwa ufafanuzi!
 
Kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, kama ni kweli Chenge alikuwa anatafuta kiti cha kukaa, na matokeo yake ni haya, basi mzee wa visenti bahati zote zimeanza kumkataa.

Inawezekana kabisa kilichosemwa ndio ukweli lakini matatizo ya nchi kama za kwetu ambazo ukweli daima hufichwa, inakuwa ngumu sana kwa sisi wananchi kuamini kinachosemwa.

Ilitakiwa polisi ndio watoe statement hiyo na wala sio msemaji wa CCM. Lakini naye Chenge kwa spika na naibu spika nako kuna seats za kukaa wabunge?

Watanzania tumezidi uoga yaani kusikia kuna uchawi, watu wanaharisha, wengine wanapata stroke, wengine wanakataa kuingia bungeni. Mimi naamini hapa suala ni hiyo bahati mbaya ya Chenge au uchawi. Ingelikuwa sumu wala hili jambo lisingeishia hapo na kufikia sasa ukumbi ungelikuwa umefungwa.
 
Heshima bro, binadamu mwenye akili sana hata akisikia jirani tu ameumwa na nyoka basi yeye hata ujani ukilia hutoka bomba sana, halafu akiskia mwenziwe ananyolewa basi yeye hutayarisha maji,

Sasa baada ya kumuona kwa macho yao viongozi kama Amina Chifupa na Balali, wewe unasema viongozi waliobaki waendelee kuwa wajinga?
 
Habari ambazo tumezipata kutoka kwenye TBC1; ambazo Katibu Mwenezi wa CCM ameonyeswa amezielezea ni kwamba... hilo jambop limejadiliwa kwenye kikao cha NEC. hata hivyo Katibu huyo mwenezi amesema... wanasubiria vyombo vya usalama viseme what happened... maana ndivyo vyenye authority!

Na maelezo ni kwamba huyo Mbunge ambaye sasa anatoka viti vya mbele vile vya mawaziri... na sasa anatakiwa kupatiwa kiti kingine kule back bencha alikuwa akipitishwa na wahudumu wa ofisi za bunge kuonyeshwa kwenye kikao hiki akae kiti gani...

Kwa maana hiyo basi ni jambo la kawaida kutafuta kiti... unalazimika kupitia kwenye safu mbalimbali na kuangalia kiti au sehemu ambayo ni muafaka kwako..

Kwa hili inaonyesha dataz za JF zimefungwa 3-0

JF 3 - Kasheshe/Mafisadi 0
 
Mie jamani naomba kujua huyo chiligati sijui nani sijamwelewa
Hivi wabunge viti bungeni wanajitafutia wao wenyewe nafasi ipo wapi wakae au wanawekewa na watumishi wa bunge?
2. Kama wanajitafutia wenyewe sasa hayo majina kwenye viti yalitoka wapi?kiasi jamaa awe anaangalia jina lake?
3. Na kama kulikuwa na majina kumbe iliwezekana kabisa kuoneshwa kiti chake wakati ule ule rasmi wa kuingia bungeni
4. Kwa mtizamo reasonable kabisa hata mie nikienda pale bungeni leo sitatafuta kiti najua nitaoneshwa tu na makarani wa bunge sembuse mtu aliyekuwa waziri na inajulikana kabisa anarudi kuwa back bencher?
5. Kwa taarifa zilizopo ule ukumbi wa bunge una idadi ya viti kubwa kuliko wabunge waliopo,je kulikuwa na haja ya kutafuta kiti mapema?
6. kwani bunge wakati linaanza ile siku ya kwanza alikaa wapi?mpaka atafute kwa kukaa awamu ya pili ambako kungesomwa bajeti?au hata kama alikuwepo kwanini atafute kiti siku ambayo sio official kwa wabunge kuingia kwenye debate hall?
7. Kwa spika ama naibu spika nako ni back bencher?mbona alishawapta hata mawaziri au alitaka kuongoza bunge siku hiyo?
Maswali haya na mengine mengi yanazua circumstantial evidence kuwa huenda basi amehusika,na kwa wale waliosoma sheria ya ushahidi najua wamo wana sheria humu,kuna vitu kama res gestae kwenye ushahidi na pia section 3-20 ya sheria ya ushahidiTanzania ambapo kuna mambo ya ushahidi wa kusikia au kudhani yanaruhusiwa ili mradi yawe supported na other set of facts(yaani corroborated) hivi hamuoni kama chenge anatia shaka?
 
Last edited:
Quote:- Kasheshe

Habari ambazo tumezipata kutoka kwenye TBC1; ambazo Katibu Mwenezi wa CCM ameonyeswa amezielezea ni kwamba... hilo jambop limejadiliwa kwenye kikao cha NEC. hata hivyo Katibu huyo mwenezi amesema... wanasubiria vyombo vya usalama viseme what happened... maana ndivyo vyenye authority!

Na maelezo ni kwamba huyo Mbunge ambaye sasa anatoka viti vya mbele vile vya mawaziri... na sasa anatakiwa kupatiwa kiti kingine kule back bencha alikuwa akipitishwa na wahudumu wa ofisi za bunge kuonyeshwa kwenye kikao hiki akae kiti gani...

Kwa maana hiyo basi ni jambo la kawaida kutafuta kiti... unalazimika kupitia kwenye safu mbalimbali na kuangalia kiti au sehemu ambayo ni muafaka kwako..

Kwa hili inaonyesha dataz za JF zimefungwa 3-0

Posted Date::6/13/2008
Mbunge anaswa akifanya tambiko bungeni Dodoma
*Alisindikizwa na kigogo wa Bunge
*Spika akiri kupokea taarifa hizo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

MBUNGE na Afisa mmoja Mwandamizi wa Bunge wamekutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kishirikina. Taarifa zilizopatikana mwanzoni mwa wiki hii na kuthibitishwa na ofisi za Bunge, inadaiwa mbunge huyo alifanya tambiko hilo Jumatatu, kabla ya mkutano wa Bunge la Bajeti kuanza Jumanne wiki hii. Shuhuda aliieleza Mwananchi kwamba, mbunge huyo aliingia kwenye ukumbi huo akiwa ameongozana na katibu mmoja wa bunge (jina tunalo) na kuanza kupita kila kiti cha mbunge na hatimaye aliishia kiti cha Spika.

Aliongeza kuwa, watu hao wakiwa wamefuatana walikuwa wakipita kila kiti huku mbunge huyo akinyunyiza vitu vinavyohisiwa kuwa dawa za kienyeji katika viti vya wabunge. "Alipofika kwenye kiti cha Spika, alisimama muda mrefu akiwa ananyunyizia vitu fulani, lakini sikujua ni nini na wao waliamini kamera zote zilikuwa zimefungwa," alidai shuhuda huyo. Shuhuda huyo alidai kuwa, mbunge huyo na mtumishi wa bunge walifanya shughuli yao bila kufahamu iwapo walikuwa wakionekana, bila kujua kuwa kulikuwa kuna watu wanafanya majaribio ya kunasa sauti na picha za ukumbini.

"Walianza kwa kusimama nje kwa muda mrefu wakiwa na wabunge wengine, baada ya wabunge kuondoka, mbunge huyo alibaki na katibu na kuingia ukumbini na kuanza kufanya kazi zao," alidai. Alipoulizwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, iwapo ana taarifa hizo jana, alisema amezipata na kueleza kushangazwa kwake iwapo bado kuna watu wanaoamini mambo ya ushirikina.
"Taarifa ninazo ila siamini, isipokuwa inashangaza kuona kama bado kuna watu wanaamini mambo hayo kwenye dunia ya leo," alisema Sitta. Sitta alisema baada ya kupata taarifa hizo, Katibu wa Bunge ameanzisha uchunguzi wa suala hilo. Hata hivyo alisema ushirikina hauwezi kusimama badala ya ukweli na haki.

Naona kuna watu tayari wameshaanza spin, ina maana moja tu kuwa tayari tumewashika pabaya, sasa mimi ninaomba kusema hivi nyinyi maa-agent wa serikali na serikali kwa ujumla, ni hizi spin zenu za kutaka kubadili ukweli ndio mantupa motisha wa kutafuta dataz kabla hamjazi-spin,

Look at this ishu, ukweli uko wazi kabisaa kwa kipofu Mkulu wangu Gavana wa New York, kuona, lakini here comes jamaa na spin kuwa eti mbunge alikuwa nahama kutoka viti vya mbele na nyuma, sasa mbona hawakusema kwa nini Mwakyembe ameenda kuangaliwa afya yake ambayo hapa ni clear kuwa imedhuliwa na huyo mbunge kuhama kiti cha mbele na nyuma? Hivi mnafikiri ni nani hapa asiyejua umbali wa kutoka kiti cha bunge na cha Chenge, kuanzia cha zamani mpaka cha sasa? Nani asiyejua kuwa kiti cha Mwakyembe kiko umbali wa akribu mile moja kutoka kiti kipya cha Chenge, sasa alipitiaje kwa Mwakyembe?

Sasa ni huu jinga ujinga wenu ndio unatufanya tuzitafute dataz na ku-strike ahead kabla hamja-spin, hapa ni clear kuwa tumewashika pabaya, wakuu naomba kuuliza hivi, mnafikri ninsingesema jana kuwa Mwakyembe ameenda Dar kwa uchunguzi zaidi wa kiafya, hivi kuna chombo hata kimoja cha serikali kingesema in public? Hivi mnajua kuwa siku hizi CCM na serikali kabla hawajajibu tuhuma yoyote serious huja hapa kwanza kuona kuna nini on the ishu ndio wanasema? Chiligati alikuwa wapi toka juzi kusema hili? Kasheshe ulikuwa wapi tangu juzi kuyasema haya ya Chenge kuhama kiti cha mbele na nyuma?

Tutaendelea tu kuwaeleimisha wananchi hapa JF, hatutarudi nyuma wala kudanganywa hata siku moja, JF mbele tena sasa ndio tutazidisha dataz tena kiroho mbaya! Kwenye hili la Chenge mmeshikwa pabaya, sasa kubalini sio kutaka ku-spin bila sababu wala hoja! Unajua mkiiwa wa kweli tunaweza kuwapa heshima kidogo lakini mkitaka hizi za spin subriri muone yaani you ain't seen anything yet, promise!
 
Haya ukweli umeshafahamika!MUNGU ni mkubwa!Jamani watanzania tufanyeni kazi na tuache mambo ya uzushi yasiyo na evidence hiki ni kipindi cha sayansi na tekinologia bwana,la sivyo hatutaenda mbele!maneno mengi hayatatufikisha popote!
Habari ndo hiyo!
Hollo
 
Na maelezo ni kwamba huyo Mbunge ambaye sasa anatoka viti vya mbele vile vya mawaziri... na sasa anatakiwa kupatiwa kiti kingine kule back bencha alikuwa akipitishwa na wahudumu wa ofisi za bunge kuonyeshwa kwenye kikao hiki akae kiti gani...
wanasubiria vyombo vya usalama viseme what happened... maana ndivyo vyenye authority!

Haya ukweli umeshafahamika!MUNGU ni mkubwa!Jamani watanzania tufanyeni kazi na tuache mambo ya uzushi yasiyo na evidence hiki ni kipindi cha sayansi na tekinologia bwana,la sivyo hatutaenda mbele!maneno mengi hayatatufikisha popote!
Habari ndo hiyo!

Masikini ya Mungu, tizama wanavyojichanganya wenyewe, mara wamejadili, mara mbunge alikuwa anhama, mara wanasubiri taarifa ya polisi ya uchunguzi, wallahi ameshikwa mtu pabaya hapa!
 
We hollo mbona unatutia kichefuchefu sana wewe! yaani unajitahidi kutukatisha tamaa lakini hutatuweza. We rudi kwenu Bariadi na na kwambia hutapokelewa tena kama ulivyopata zile heshima za kujinunulia. Jimbo lile si lako tena safari hii, jimbo lako ni Harvard na ndugu yako Sumayi. Ole wako!!!
 
Haya ukweli umeshafahamika!MUNGU ni mkubwa!Jamani watanzania tufanyeni kazi na tuache mambo ya uzushi yasiyo na evidence hiki ni kipindi cha sayansi na tekinologia bwana,la sivyo hatutaenda mbele!maneno mengi hayatatufikisha popote!
Habari ndo hiyo!
Hollo

Mkuu hollo heshima mbele,
Ukweli upi wakati maswali haya hatujajibiwa?

Hivi wabunge viti bungeni wanajitafutia wao wenyewe nafasi ipo wapi wakae au wanawekewa na watumishi wa bunge?
2. Kama wanajitafutia wenyewe sasa hayo majina kwenye viti yalitoka wapi?kiasi jamaa awe anaangalia jina lake?
3. Na kama kulikuwa na majina kumbe iliwezekana kabisa kuoneshwa kiti chake wakati ule ule rasmi wa kuingia bungeni
4. Kwa mtizamo reasonable kabisa hata mie nikienda pale bungeni leo sitatafuta kiti najua nitaoneshwa tu na makarani wa bunge sembuse mtu aliyekuwa waziri na inajulikana kabisa anarudi kuwa back bencher?
5. Kwa taarifa zilizopo ule ukumbi wa bunge una idadi ya viti kubwa kuliko wabunge waliopo,je kulikuwa na haja ya kutafuta kiti mapema?
6. kwani bunge wakati linaanza ile siku ya kwanza alikaa wapi?mpaka atafute kwa kukaa awamu ya pili ambako kungesomwa bajeti?au hata kama alikuwepo kwanini atafute kiti siku ambayo sio official kwa wabunge kuingia kwenye debate hall?
7. Kwa spika ama naibu spika nako ni back bencher?mbona alishawapta hata mawaziri au alitaka kuongoza bunge siku hiyo?
Maswali haya na mengine mengi yanazua circumstantial evidence kuwa huenda basi amehusika,na kwa wale waliosoma sheria ya ushahidi najua wamo wana sheria humu,kuna vitu kama res gestae kwenye ushahidi na pia section 3-20 ya sheria ya ushahidiTanzania ambapo kuna mambo ya ushahidi wa kusikia au kudhani yanaruhusiwa ili mradi yawe supported na other set of facts(yaani corroborated) hivi hamuoni kama chenge anatia shaka?
 
Masikini ya Mungu, tizama wanavyojichanganya wenyewe, mara wamejadili, mara mbunge alikuwa anhama, mara wanasubiri taarifa ya polisi ya uchunguzi, wallahi ameshikwa mtu pabaya hapa!
Kashikwaje pabaya!mmeshaambiwa kilikuwa kinatafutwa kiti!Hapa dawa ni kuachana na haya mambo na kuendelea kuchapa kazi!haya wewe evidence zako zipo wapi?zaidi ya maneno?
 
Back
Top Bottom