Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi, niko hapa jijini Arusha, kuwaletea live, kinachoendelea, kwenye mkutano wa kimataifa wa ITAC
ITAC is a brainchild of WAJIBU designed for people to meet and discuss trends on transparency and accountability, sharing best practices, successes and challenges in order to promote an interdisciplinary learning in hastening the transformation process by promoting the culture of transparency and accountability in our societies.
The conference theme is “Transformation to a culture of total transparency and accountability”.
The conference is held from 18th – 19th November, 2021 at the Gran Melia Hotel in Arusha, Tanzania.
Kwa kuanzia, msikilize Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akiuzungumzia mkutano huu.
Bila Kuwepo Uwazi Serikalini, Hakuna Uwajibikaji!- Ludovick Utouh, Aaandaa Kongamano la Kimataifa la Uwazi na Uwajibikaji Afrika.
Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Wajibu, Ludovick Utouh, amesema bila ya kuwepo kwa uwazi katika utendaji wa serikali, uwajibikaji hautakuwepo, ili uwajibikaji uwepo, ni lazima kwanza utanguliwe na uwazi, baada ya kuwepo kwa uwazi kwa kila mtu kujua kila kinachofanyika, watendaji watajikuta wanalazimika kuwajibika maana kila kitu kitakuwa kiko wazi.
Utouh ameyasema hayo, jijini Dodoma, katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, wakati akilitambulisha kongamano la kimataifa la kujadili umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika kusukuma mbele maendeleo, sio tuu ya nchi ya Tanzania, bali maendeleo ya bara lote zima la Afrika.
Bwana Utouh, amesema Kongamano hilo la siku mbili, linafanyikia jijini Arusha, litaanza kesho Alhamisi, tarehe 18 November, 2021 na kumalizika Ijumaa, tarehe 19, November, 2021 ambapo mada mbalimbali kuhusu umuhimu wa uwazi na uwajibikaji, zitawasilishwa na wataalamu wabobevu wa kimataifa kutoka Tanzania, Afrika na Kimataifa.
Bwana Utouh amesema, kongamano hilo lina umuhimu wa kipekee, kwasababu bila kuwa na uwazi katika utendaji kazi serikalini, utendaji unakuwa haupo, na kusisitiza, hoja za uhitaji wa serikali kutenda kazi kwa uwazi, ni takwa la kikatiba, na lipo kwenye katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Mkutano huu unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 500 kutoka sehemu mbalimbali.
Mgeni rasmi alipaswa kuwa Makamo wa Rais, ila for now, ametuma mwakilishi
Mkutano umeanza, mwakilishi wa mgeni rasmi amewasili, nitaendelea kuwapatia kinachoendelea hapa.
Karibu.
Paskali