Mkutano wa mazingira wa ITAC 2023 kufanyika Arusha, kushirikisha Nchi sita

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkutano wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (International Transparency and Accountability Conference - ITAC) unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 na 29, 2023 wenye lengo la kutoa elimu na kuibuka utatuzi wa changamoto za mazingira unatarajiwa kushirikisha Wadau 300 kutoka Nchi sita.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Gran Melia, Jijini Arusha, Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh amesema Mkutano huo wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (ITAC) utakuwa wa tatu tangu WAJIBU ilivyoanza kuaanda mikutano ya aina hii Mwaka 2021.
9b4a80ce-5e2a-4ab4-856c-85553d9b2ac9.jpeg

Amesema "Strengthening Accountability for Climate Action, yaani Kuimarisha Uwajibikaji kwa Mabadiliko ya Tabianchi ndio maudhui ya Mkutano wa ITAC.”

Ametaja mada mbalimbali zitawasilishwa na watoa mada wa ndani na nje ya nchi;

* Sayansi ya Mabadiliko ya Tabianchi;

* Vihatarishi vya kifedha katika Mabadiliko ya tabianchi (Climate change and fiscal risks)

* Ushiriki wa sekta binafsi katika ufadhili wa kifedha wa mabadiliko ya tablanchi na taratibu za uwajibikaji wa fedha za sekta binafsi (Private sector engagement in climate change financing and the accountability mechanisms for private finance).

* Mbinu Bunifu kwa ajili ya kukabiliana na kuendana na mabadiliko ya tabianchi (Innovative Mechanism for climate change Mitigation and adaptation).
c20a54c2-0824-4730-b8e9-b261c355bbc2.jpeg

Ameongeza kuwa mkutano utahusisha Taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo, Wanadiplomasia, Wanaazaki, Wabobezi wa masuala ya uwazi na uwajibikaji, wabobezi wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi, wanataaluma na Wanahabari wa ndani na nje ya nchi, kukiwa na ushiriki wa moja kwa moja na wa njia ya mtandao

Ameeleza kuwa uwepo wa Watoa mada wa kimataifa utangeza ladha ya Kimataifa kwa kupata uzoefu wao kutoka katika Nchi Sita ambazo ni Tanzania, Afrika ya Kusini, Kenya, Zimbabwe, Nigeria pamoja na Zambia na watoa mada kutoka katika nchi hizo wameshathibitisha ushiriki wao katika Mkutano huu mkubwa wa Kimataifa wa Uwajibikaji (ITAC 2023).

Aidha, amesisitiza kuwa Mkutano huo unatarajiwa kuleta uelewa mzuri juu ya changamoto na fursa zinazohusiana na uwajibikaji wa kifedha wa umma katika kugharamia hatua ya mabadiliko ya tabianchi, na kubainisha mikakati ya kuimarisha mifumo ya uwajibikaji wa kifedha.

“Washiriki watapata fursa ya kubadilishana ujuzi na uzoefu, usimamizi mzuri zaidi wa fedha zinazohusika na mabadilko ya tabianchi, kutambua vihatarishi (risk) vilivyopo na namna ya kushughulikiwa na kupanga wakati wa ushiriki wa pamoja kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi hayana mipaka,” amesema na kuongeza:
0bbdc9ef-aa73-46a3-a10f-31c77f058d9b.jpeg

“WAJIBU inatoa rai kwa wadau wote wa uwazi na uwajibikaji kutoka ndani na nje ya nchi kuweza kushiriki Mkutano huu wa Kimataifa wa ITAC 2023 ambao ni fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo ya nini kifanyike ili kukuza na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwenye usimamizi wa fedha na rasilimali nyingi zinazohitajika kwenye kugharamia kudhibiti hali ya mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo ya nchi za Bara la Afrika.

“Aidha, watu wenye fani za Masuala ya Mazingira, uhasibu, uchumi, sheria, utafiti, waandishi wa Habari, wana geologia na maendeleo ya jamii, mkutano huu ni muhimu sana kwao kwa kuwa mada zitakazojadiliwa zinahusu moja kwa moja utendaji wa kazi zao.”

Amesema wanashauri Wadau kujiandikisha kushiriki kwenye Mkutano huu kupitia tovuti ya www.wajibu.or.tz ambapo mwisho wa uandikishaji utakuwa tarehe 18/09/2023.

Amesema Washiriki wanaotokea nchini watakaohudhuria ukumbini - (physical) na watakaoshiriki kwa njia ya mtandao (online) watachangia Tsh 25,000.

Washiriki wanaotokea nje ya nchi - (non-Residents) watakaohudhuria ukumbini - (physical) na watakaoshiriki kwa njia ya mtandao (online) watachangia Dola za Marekani 15.

Mzee Utouh amehitimisha kwa kusema “Akaunti ya washiriki waliopo nchini (Local Account) watapitia NMB ambapo jina la akaunti ni WAJIBU Institute of Public Accountability, akaunti Namba 20110018487 na mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni Septemba 25, 2023.”
 
Back
Top Bottom