Rais Samia amehutubia kwa njia ya Mtandao Mkutano Mkuu wa (9) wa Asasi ya Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji (EITI) nchini Senegal

Jun 4, 2022
68
184
Katika hotuba hiyo Mhe. Rais amesisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza vigezo vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Rasilimali madini, mafuta na gesi asilia kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wananchi; kupambana na rushwa katika sekta ya madini, mafuta na gesi asilia; na kuwezesha Sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya nchi.

Mhe. Rais alieleza kuwa katika utekelezaji wa Vigezo vya uwazi na uwajibikaji vya Asasi ya Kimataifa ya EITI, Tanzania imetunga Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika sekta ya madini, mafuta na gesi asilia ya Mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake za mwaka 2019 ambazo zinasimamiwa na Taasisi ya TEITI. Amesisitiza kuwa Sheria na Kanuni zinazosimamia sekta ya madini, mafuta na gesi asilia zimeweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta hizo hapa nchini.

Aidha, alieleza kuwa hadi sasa Tanzania imeweka wazi ripoti kumi na mbili (12) za ulinganishi wa malipo ya kampuni za madini, mafuta na gesi asilia na mapato ya serikali. Pia, Mhe. Rais amesisitiza kuwa Tanzania inajivunia kuwa ni moja ya nchi inayotekeleza vigezo vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji duniani kwa kuwa vinaendana na Sera ya nchi katika usimamizi wa Uwazi na uwajibikaji. Amesisitiza pia, suala la uwazi na uwajibikaji linasimamiwa kuhahakikisha kuwa manufaa ya usawa yatapatikana kati ya Mwekezaji na Serikali ya Tanzania sekta ya madini, mafuta na gesi asilia.

Mhe. Rais alimalizia kwa kusema kuwa “Nawakaribisha wawekezaji wote duniani kuwekeza nchini”

Lengo la Mkutano huo ni kuunganisha nchi wanachama wa EITI duniani kwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio katika utekelezaji wa vigezo vya kimataifa vya EITI. Aidha, Mkutano huu ni fursa ya kutoa mapendekezo yatakayowezesha kuboresha shughuli za uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali madini, mafuta na gesi asilia duniani.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa(Mb), Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga; Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Bw. Dunstan Kitandula, Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Bi. Jesca Kishoa, Mwenyekiti wa kamati ya TEITI Bw. Ludovick Utouh, Mjumbe wa kamati ya TEITI Bw. Adam Anthony na Kaimu katibu Mtendaji wa TEITI Bi. Mariam Mgaya.
 
Hakugusia japo kidogo kuhusu mkataba wa milele kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kampuni ya DP ya Waarabu wa Dubai?
 
Back
Top Bottom