Kusaidia Ndugu/familia ni wajibu au lazima?

Kwa upande wa familia yangu
Nawajibika kwa mama,baba,Bibi,wadogo zangu na wale waliochangia maendeleo yangu tu

Kwa upande wa familia ya mume wangu nawajibika kwa baba yake,mama yake na waliochangia kufika alipo Basi

Kama hata kwenye story za mafanikio yake haupo arooo sahau
 
Huu niutamaduni wetu watanzania na baadhi ya mataifa mfano wahindi na waarabu.

Sera nzuri ya kijamaa shida ni moja au mbili
1 jinsi tunavyo wasaidia ndugu zetu
Jamii ya watanzania husaidia ndugu zao kwa mtindi wa kukidhi haja ya anaye hitaji mfano mdogo wake ambaye anaweza kujishuhulisha anaumwa au amepata ajal wakati mwingine ametia mimba basi atatoa pesa ya kutatua tatizo lile tu hivyo anajikuta kila likitokea anabeba msalaba.

Tofauti na wenzetu wahindi au waarab nipo hapa Zanzibar naona mfano wao hujitahidi kumtafutia mtu cha kufanya watampa ndugu mtaji au kumwanzishia kitu alichosema anataka kujishughulisha nacho na baada ya hapo watajivua kwa ndugu huyu ikitokea kapoteza kile walicho mpa ajiendeleze ni msiba wake

Hata mimi sio muumin na tabia hii ndio maana nimejifungia Zanzibar staki kusikia la muadhin wala mnadi swala mpaka nitakapo ona naweza kumuezeaha mtu.
Ukweli ni kwamba inarejesha nyuma hivyo tukitaka kujivua tuwawezeshe kupata njia ya kuingiza kipato sio kutatua shida zao
 
Nimeona sehem nyingi, familia nyingi na hata mmoja wa polisi aliyefariki kwa tukio la Juzi inaonesha kua alikua tegemeo la familia nzima mpaka mtoto wa kaka yake.

Hoja yangu ni moja.
Hii ni tamaduni au ni vipi!?

Unamaliza shule, unapata kazi baada ya hapo unatakiwa kusaidia familia nzima na ndugu wa pembeni(kitanzania)

Mtazamo wangu:
hii ni moja ya kurudishana nyuma kimaendeleo

Nilidhani ni vema iwe kutazama future ya yako kwanza na kuhudumia/kusaidia wengine isiwe ni wajibu/lazima bali iwe HIYARI kulingana na uwezo wa mtu.
Kusaidia ni LAZIMA.
Subiri ugongwe na daladala ndio utaelewa.
 
mimi husaidia ndugu kwenye issue za ugonjwa akifika hatua ya kulazwa,nikipata taarifa wanachangia kidogo gharama. Nawauliza bill ni kiasi gani,wanatumia robo yake kama costs hazizidi laki 5!

Muda mwingine unapigiwa simu umchangie ada ya mtoto! Swali linamrudia na mimi ninasomesha nahitaji kuchangiwa?
 
Familia zetu za Kitanazania nyingi ni maskini ! Kwa hiyo kama unao uwezo wa kusaidia hasa upande wa elimu usisite kufanya hivyo ili kuongeza wasomi watika ukoo wenu. Mungu akusaidie ili uweze kulitambia hilo.
Mungu ameshanisaidia na kunionesha kua yote hayo ni sababu ya umasikini.

Najua ni ngumu kubadili hii kwenye vichwa vya watanzania.

Ndugu ni mzigo na ni sababu ya umasikini tukiendekeza hii tabia.
 
Kusaidia ni LAZIMA.
Subiri ugongwe na daladala ndio utaelewa.
Mpaka hapa umeshadhihirisha imani ya uoga na ya kimasikini.

Kuweka fikra bila ndugu basi hakuna linalowezekana tayari ni umasikini.

Ajali zipo.
Kwani wote waliopata ajali, walisaidiwa na ndugu!?

Usipobadili fikra utaishi kimaskini mpaka uzao wako.
 
Mungu ameshanisaidia na kunionesha kua yote hayo ni sababu ya umasikini.

Najua ni ngumu kubadili hii kwenye vichwa vya watanzania.

Ndugu ni mzigo na ni sababu ya umasikini tukiendekeza hii tabia.
Uzuri wa msaada ni kwamba hulazimishwi lakini kuwasaidia ndugu au watu baki kama uwezo upo ni jambo muhimu sana na baraka kwako.
 
hii kitu ngumu sana ndugu zangu...tunapaswa kuwasaidia hakika...ila ukicheza hao ndio watakuangusha.....nlishawasomesha shemeji zangu duh...mie sikufika univ....hakika nliwalipia kwa kuunga unga.....walichokuja kuniambia....ila nimewasamehe kabisa...eti " kama baba etu angekuwepo angeweza kutosomesha...tukipata kazi tutakurudishia" na wamepigika na digrii zao...wacha...mmoja fundi simu posta,,,,mwingine keshatunguliwa 2 na baba tofauti......mie nadunda tuuu....adabu imewakaa....
ulikuwa una moyo kusomesha shemeji mimi siwezi na sitakuja kufanya
 
Back
Top Bottom