Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,895
HUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.
Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).
Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.
Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.
Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.
Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.
Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.
Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.
Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.
Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.
Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.
Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.
Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.
Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI
Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.
Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.
Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.
Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam