Mateso ajira mpya kupata hela ya kujikimu

Mateso ajira mpya kupata hela ya kujikimu

mwinuka2023

Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
26
Reaction score
56
Wakuu kwema

Kama kichwa Cha mada kilivyo jieleza hapo naomba niwasogee hapa jinsi mambo yalivyo kwa Hawa wenzetu wa ajira mpya.

Nimekuwa nilifatilia mjadala sehem mbalimbali za wenzetu wa ajira mpya wengi wakilalamika kutopewa hela ya kujikimu ambayo ni haki yao.

Mwanzo nilidhani labda serikali Haina pesa ila Leo nimeshutushwa baada ya kupitia group Moja la walimu kuona wakiongelea habari ya Rushwa.

Iko hivo fedha zipo Halmashauri ila watumishi wa Halmashauri hawataki kutoa tu fedha kwa wahusika Ili kutengeneza mazingira ya Rushwa hivo basi baadhi Yao wanalazimika kutoa laki Moja kama hongo Ili upate pesa ya kujikimu 960000/= na ukitoa laki Moja Leo kesho tu hela inangia kwenye account yako.

Na hii ni kwa Halmashauri nyingi tu hapa nchini na usipotoa ujue kupata haki yako ni ngumu na unaweza usipate kabisa na ukionekana kiherehere wa kuifatilia na kuhoji mambo basi utakuwa na wakati mgumu sana hata hiyo kazi utaona ya uchungu, wenye mambo mepesi ni wale tu wanaotangulia Kurahisisha mambo (hongo).

Maswali ninayojiuliza TAKUKURU hawaoni haya mambo au idara zao za uchunguzi Huwa zinafanyaje kazi Hadi kushindwa kunusa harufi ya Rushwa kwenye mambo kama haya.

Kupata haki yako ni Hadi utoe rushwa vipi mwingine ambae Hana hiyo Laki Moja anaishije kuna andiko nimesoma hapa jamaa analala chini kwenye baridi Kali hela ya kula Hana huyu mtu anafundishaje watoto wetu au kama ni muuguzi anahudumiaje wagonjwa kwa kutoa huduma Bora.
 
Back
Top Bottom