Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Mkuu huu msimamo wako ndo wangu. Wananchi wengi wanajipa stress kwasababu ya kuigana. Nyumba na gari ni kitu kinawarudisha nyuma vijana wengi. Binafsi bado sina nyumba wala gari ila niliamua kuwekeza kwenye biashara ili kuwa na kipato cha uhakika. Hii kujenga nyumba ili tu ionekane una nyumba hata kama ni ya kiwango cha chini ni jambo ambalo nimelikataa. Au mwanaume kama mimi kununua Passo, Vitz, IST au Starlet ili nionekane nina gari ni upuuzi mwingine nilioukataa. Nasisitiza tu kuwa kijana fanya unachofanya kwa bidii na maarifa ukitanguliwa na uaminifu basi mafanikio yatakuja kihalali bila stress. Usimwige mtu. Run your own race.
Maisha ni malengo. Kamwe usishindane wala kujilinganisha na mwingine. Our struggles are different.

Kwa kijana wa kawaida wa Kitanzania (ambao ndo tuko wengi), ambaye ametoka kijijini akabahatika kuingia University, its is obvious atamaliza degree ya kwanza at the age of 25-27. Baada ya hapo aanze kutafuta address mjini. By the time anaanza kupata sense of stability he is already 30! Na mishahara ya serikali yetu (hata Private sector), you can see that struggle is real. coupled na extended families mambo yanakuwa magumu zaidi.

Hapo linganisha na yule ambaye ni mjasiriamali. Alimaliza form four/six akaingia uraiani. Wengine walifanikiwa. wengine hawajafanikiwa. Wengine unayatamani mafanikio yao. Wengine wanatamani ya kwako. Ilimradi kila mtu anauelewa wake nini maana ya mafanikio.

Ushauri kwa wadogo zetu. Msishindane na wengine. Maisha hayana specific plan. Na mjue kabisa usione vyaelea vimeundwa/tafutwa. Kikubwa muwe na bidii/juhudi na muwe waaminifu katika majukumu yenu. Uaminifu ni silaha.

Ukiona mtu anaendesha gari. Don't panic! ukiona ana nyumba nzuri don't panic! be inspired. Mimi nimenunua gari 10 years after University. Kuna kipindi mpaka jamaa zangu wakawa wananicheka (by then nilikuwa hata naazima IST ya wife). But I knew what I wanted. At the end of the day nimenunua gari ambayo najua ni jasho langu. Its a beautiful car which I dreamed all along! Chuma cha Mjerumani. and that gives me inner satisfaction. Sijaanza kujenga nyumba yangu (nimeshawajengea wazazi though). Lakini some of my friends wamejenga mpaka maghorofa. Nawatembelea, we drink together and we are close as ever.

But I know when time comes, God allowing, I will build house (in a nice place ;-) and friends and foes alike will admire it. Huu utaratibu wa kujenga simply kwa sababu fulani amejenga "anakaa kwake" niliukataa. Au kwenda kununua kiwanja ni the middle of nowhere....kusudi tuu niwe na nyumba...nilikataa..(bora kurudi kujenga kijijini kwetu). Honestly kuna nyumba nyingine unaziangalia mpaka unasema Lord Have Mercy kwa huu ujenzi.......lakini unakuta yote yanafanyika kwa sababu watu wanaishi kwa kufuata pressure za wengine............! I reject this notion..I have got one life to live.

I determine my own pace of movement. Sitaki pressure za walimwengu. At the end of the day sishindani na mtu. Maisha niliyonayo ni haya tuu. I simply want to be happy and fulfilled.
 
Vyote ninavyo...nyumba nilijenga at 28 na gari ati 29 now after kujenga migombani ndo nimenunua kwingine na msingi wa nyumba ya pili tayari at my 31! Pambana yote yanawezekana mangi!!
WE KWELI MANGI!
safiiii!
 
Naona kila mtu under 30 alikua na mafanikio sana, kwa wale wa Dar mbona daladala na mwendokasi zinajaa sana.

Basi wacha twende sawa.

Nikiwa na miaka 13 tu nliweza kununua kiwanja kikubwa na kujenga nyumba mbili, moja nlikua napangisha nyingine naishi mwenywe.

Sasa hvi nina miaka 19 lakini namiliki nyumba za kifahari 9, magari 20, mengine nimewapa wadogo zangu waendee shule.

Jamiiforums
Where everyone is rich.
 
ngoja mimi nisiongee neno maana wengine wanaweza yaita matusi
Ila wengi wenu hapa ni waongo, hamna nyumba wala gari.
tofautisha usafiri na gari
Tofautisha NYUMBA na nyumba
wengi wetu (wetu) wana usafiri tu na nyumba
hakuna mwenye NYUMBA
 
Maisha hayana bahati kla mtu kazaliwa na bahati
Nimetumia muda mwingi kudadavua ulichoandika sijakuelewa... Wapi nimeandika maisha yana bahati????? Duuuuuuuh????? Uzee huu macho hayaoni vizuri nadhani.......
 
Nenda Mereran ukajionee wapo wa chini ya miaka 20 wanamiliki magar na nyumban zaidi moja.
 
do!bia 1=tofali 2!ina maana chumba kimoja cha tofali 450=bia 225!kumbe mwaka 1 badala ya bia =vyumba 2!

Kingine usitumie nguvu wala kuiga mtu kwenye kujenga.

Fanya kwa uwezo wako. Kidogo kidogo unainua upande mmoja mmoja.

Ukishajenga ya kwanza ya pili na ya tatu zitafuatia.
 
Nilichogundua bhana maisha hayana formula ili ufanikiwe,unaweza ukawa mpambanaji lkn bado ukagonga 30 Huna hata gheto,unaweza ukawa na under 30 na vitu vyote hivyo ukawa tayari umeshamiliki,so haya mambo ni kumshirikisha sana Mungu na kupambana bila kukata tamaa,na bahati vilevile zinachangia kwakweli
 
Nilivyoanza ujasiriamali miaka kadhaa nyuma wakati bado nikiwa mdogo sana, vitu ambavyo vilinimotivate vilikuwa ni Gari kali, kuishi Mbezi Beach, kuvaa nguo kali kali, kupiga misele na Celebrities, kua na mademu wakali... nilivyopata hivyo vyote nikaja kugundua ni utoto tu, jambo ambalo nimelipa kipaumbele ni kujipa na kujipa tena knowledge, nilikuja kugundua kua na knowledge kamwe hautafilisika, nilikuja kugundua network ni jambo la msingi sana sana ili uwe sustainable milele, zaidi ya yote the most powerful thing ni kuwainua wale ambao bado wapo chini...

Boss, wekeza kwenye knowledge, jipe elimu afu jipe tena. Nina 23 yrs, nasukuma luxury car, nasafiri popote duniani bila kuhofia kufilisika, sijajenga bado, lkn siku nikijenga basi nina uhakika itakua ni hekalu fulani... hakuna mtu amewahi kufilisika knowledge!!

Na ukipata usipigie watu kelele... stay humble, usidharau watu, usiite watu kwa miruzi... just remain cool and be cool
Binafsi nilipopata uwezo wa kununua gari hata ya Tsh 45m at 25 yrs two yrs ago nikaona isiwe shida wacha nijiendeleze kielimu zaidi knowledge is power aisee nakubaliana na wewe with knowledge nothing is impossible.
 
Sio lazima utoboe kwa hela za wazazi. Nina mifano kama 3 real. Kuna rafiki yangu under 30 kaacha kazi mwaka jana pale World vision anamiliki mark x kali na nyumba. Hajarithi chochote. Mwingine alivyomaliza chuo kapiga ymachinga kariakoo kisha kashirikiana na wenzie kupanga chumba kariakoo, sasa hivi anapiga biashara china, india, tz. Kama unajua kodi ya chymba pale kariakoo utaelewa, Hajarithi kokote.
Mwingine ni ndugu yangu kabisaa, mwanajeshi sasa hivi anamalizia mjengo kigamboni, napiga nae story anasema mwezi wa saba ananunua gari. Naye hajarithi chochote na ni under 26.
Kiukweli sometime miaka tunayotumia kwenye elimu zetu hizi za calculus, zinatucheleweshea maendeleo kutufanya watafuta kazi
Na %kubwa ya waliofanikiwa chini ya huo umri either kuna support walioyoipata kutoka Kwa ndg jamaa au marafiki mpaka kufika hapo walipo,ila ukisimama ww mwenyewe Kwa miguu ya aisee 30 unagonga vizur kbs bila hivyo vitu ndg
 
Kila comment inatoa ushuhuda wa jinsi alivyofamikiwa under 30 ,

Ukweli ni kwamba wengi ni waongo japo wapo waliofanikiwa na wengi ni wale ambao hawajakaa shule muda mrefu (hawana degree) Ila ni wachache sana
 
Baba kuwa makini sana . Ulianza shule na miaka mitano ni chekechea au darasa la Kwanzaa. Let's say ni darasa la kwanza then plus 7 yrs ya primary ni 12 , plus 4yrs ya o level tayari ni 16, plus 2yrs ya advance tayari ni 18, plus 3yrs first degree tayari ni 21. Be careful not to that extent
Hata mm bado na walakini na hizo no aiseee
 
Mm nilifukuzwa nyumbani nikiwa 19 yrs nikaowa wen i was 21 nikiwa na escudo bro nikahama bara zima la africa na wife nikiwa 26 yrs nimejenga kigamboni tuna watoto 2 na sijutii uamuzi wakuowa na changamoto zake she is all i needed in life and she has sharpen my mind get a wife utapata vyote .....and more
I hear you bro [emoji41]
 
Inawezekana mkuu tena sana.
Ni plan zako tu na kufocus unachokitaka, Kila la kheri
 
Duh hii mada inatujeruhi wengine jamani, pole pole aisee. Naomba assessment kwangu. Nina nyumba moja uswahilini ya kawaida tu ila eneo kubwa, nina viwanja viwili vilivyopimwa, nina shamba moja heka nane, nina plot mbili zisizopimwa, nina gari ndogo ya kawaida na hapo umri umesonga balaa, nina 40yrs. Je nipo sawa au sio sawa. Kama sawa ni kwa asilimia ngapi. Naumia sana ninavyoona vijana wadogo kwangu wana maendeleo makubwa kunizidi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom