Maisha ni malengo. Kamwe usishindane wala kujilinganisha na mwingine. Our struggles are different.
Kwa kijana wa kawaida wa Kitanzania (ambao ndo tuko wengi), ambaye ametoka kijijini akabahatika kuingia University, its is obvious atamaliza degree ya kwanza at the age of 25-27. Baada ya hapo aanze kutafuta address mjini. By the time anaanza kupata sense of stability he is already 30! Na mishahara ya serikali yetu (hata Private sector), you can see that struggle is real. coupled na extended families mambo yanakuwa magumu zaidi.
Hapo linganisha na yule ambaye ni mjasiriamali. Alimaliza form four/six akaingia uraiani. Wengine walifanikiwa. wengine hawajafanikiwa. Wengine unayatamani mafanikio yao. Wengine wanatamani ya kwako. Ilimradi kila mtu anauelewa wake nini maana ya mafanikio.
Ushauri kwa wadogo zetu. Msishindane na wengine. Maisha hayana specific plan. Na mjue kabisa usione vyaelea vimeundwa/tafutwa. Kikubwa muwe na bidii/juhudi na muwe waaminifu katika majukumu yenu. Uaminifu ni silaha.
Ukiona mtu anaendesha gari. Don't panic! ukiona ana nyumba nzuri don't panic! be inspired. Mimi nimenunua gari 10 years after University. Kuna kipindi mpaka jamaa zangu wakawa wananicheka (by then nilikuwa hata naazima IST ya wife). But I knew what I wanted. At the end of the day nimenunua gari ambayo najua ni jasho langu. Its a beautiful car which I dreamed all along! Chuma cha Mjerumani. and that gives me inner satisfaction. Sijaanza kujenga nyumba yangu (nimeshawajengea wazazi though). Lakini some of my friends wamejenga mpaka maghorofa. Nawatembelea, we drink together and we are close as ever.
But I know when time comes, God allowing, I will build house (in a nice place ;-) and friends and foes alike will admire it. Huu utaratibu wa kujenga simply kwa sababu fulani amejenga "anakaa kwake" niliukataa. Au kwenda kununua kiwanja ni the middle of nowhere....kusudi tuu niwe na nyumba...nilikataa..(bora kurudi kujenga kijijini kwetu). Honestly kuna nyumba nyingine unaziangalia mpaka unasema Lord Have Mercy kwa huu ujenzi.......lakini unakuta yote yanafanyika kwa sababu watu wanaishi kwa kufuata pressure za wengine............! I reject this notion..I have got one life to live.
I determine my own pace of movement. Sitaki pressure za walimwengu. At the end of the day sishindani na mtu. Maisha niliyonayo ni haya tuu. I simply want to be happy and fulfilled.