Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Usijidanganye na hawa watu. Ela za wazazi na mitaji ya ndugu na kurithishana. Kuunganishwa na washua makazini.

Kama una hizo mambo bas utannua..pia iantegmea gharama za nyumba nk.

Bila mkono wa mtu...as in any help. Hutoboi. Kwahyo relax. 30yrs ni ndogo sna.
Sio lazima utoboe kwa hela za wazazi. Nina mifano kama 3 real. Kuna rafiki yangu under 30 kaacha kazi mwaka jana pale World vision anamiliki mark x kali na nyumba. Hajarithi chochote. Mwingine alivyomaliza chuo kapiga ymachinga kariakoo kisha kashirikiana na wenzie kupanga chumba kariakoo, sasa hivi anapiga biashara china, india, tz. Kama unajua kodi ya chymba pale kariakoo utaelewa, Hajarithi kokote.
Mwingine ni ndugu yangu kabisaa, mwanajeshi sasa hivi anamalizia mjengo kigamboni, napiga nae story anasema mwezi wa saba ananunua gari. Naye hajarithi chochote na ni under 26.
Kiukweli sometime miaka tunayotumia kwenye elimu zetu hizi za calculus, zinatucheleweshea maendeleo kutufanya watafuta kazi
 
mimi isingekuwa my extended family na shida nyingi hizi, basi hadi kufikia umri huo ningekuwa na gari na nyumba and more Nashukuru Mungu niliwahi kusoma na kupata kazi nzuri katika umri mdogo, nilimaliza my master degree at the age of 24. Nikapata kazi ya kunilipa mshahara mzuri sana at the age of 25, now nina miaka 27. Namshukuru Mungu napata mshahara si haba, nikijibana naweza nunua gari, nikajenga nyumba na nyongeza kabla ya kufikia 30. Lakini doo, mshahara ukitoka tuu unapukutika hatare, Umtumie bi mdashi home, shangazi sijui mjomba nini na nini basi najukuta naendelea kuwa maskini tuu bila kupenda. saivi ndo nipo nawajengea wazazi nyumba, nimalizanane nao ndo nianze kujijenga mimi.
 
Inategemea na familia inayokuzunguka. Kama ni wategemezi sana kwako, safari bado ni ndefu. Binafsi nilikuwa sana na tegemewa. Hadi leo hii nafikisha 30 sina nyumba wala gari zaidi ya kumiliki trekta, daladala na canter
 
Mimi niliweza kufanya hivyo vyote nikiwa na Umri wa miaka 27 Aisee Vision yangu ilikuwa kupata numba yangu kabla haya ya hayo Magari Kwa uwezo wa Mungu niliweza kufanikisha hilo ndipo nikaingia hatua ya pili ya Gari tena kipindi hicho Escudo ambayo ilikuwa inaogopwa kwa Bei za Spea. Ila nikikwambi hela nilikuwa nazipataje siwezi kukwambia.

Lazima ujitoe Kafara kwa Muda fulani..

Ila kipindi hiki cha Magu haki ya Mungu tusidanganyane
Ha ha ha bora umekuwa muwazi..namna ya kupata pesa kila mtu ni siri yake!!
 
Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.
Usikate tamaa ndugu, pambana na changamoto zinazokuzunguka utatimiza ndoto yako siku moja
 
Back
Top Bottom