Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

gari yangu ya kwanza nimemiliki nikiwa na miaka 19 peke ake ni bito mgongo wa chura
 
Niliiba hela ya mzee kwenye chimbo lake nikaenda kununua IST nyeupe nikiwa na miaka 10... baada ya kuipeleka hom mzee ana shangaa nimepata wapi hela..... Akaninyanganya funguo kimepaki hadi leo kimekuwa historia.. Kuhusu nyumba bado sijafikiria kujenga..
 
Duuh kwa hiyo kama una 30+huna nyumba wala gari na una diploma let's say ya clinical medicine afu unataka ukasome degree MD for 5 years n wa 6 intern you have to think properly,mmmh kaz kwel kwel nna miaka 31 sina hela sina nyumba sina gari sina degree na heslb wanabana mkopo,poor me
Acha fix danganya wajinga wengine degree huna bodi walikupa mkopo wa diploma au?? Huu uzi 90% ya comment ni fix tupu
 
Ni wachache sana mdogoangu ila kwa tawala zilizopita, ila atakuwa amefanya figisu somewhere aidha kukwepa kodi, kutapeli, kuiba au njia yoyote isio halali.
 
Naona mjadala ni mzito. Kabla ya kuendelea tukubaliane gari na nyumba zinazoongelewa hapa ni za thamani gani. Kwangu mimi natangaza wazi gari ya chini ya 15m inakosa uhalali wa kuingizwa hapa... nyumba yenye thamani chini ya 40m pia haipaswi kujadiliwa maana ipo chini ya kiwango. Tukubaliane kuwa gari la kuanzia 15m na nyumba iwe kuanzia 40m ndo zimemaanishwa. Kwahiyo kwa mliosema mna nyumba na gari zenye thamani ya chini ya hapo mnaweza ku-edit comments zenu kama sio kuzifuta kabisa.
 
Nilianza kuajiri watu wengine nikiwa na miaka 26 , achilia mbali kumiliki hivyo unavyosema .
 
Back
Top Bottom