Kuna under 30 anayemiliki gari na nyumba?

Webb

JF-Expert Member
Oct 4, 2016
425
883
Wakuu naomba kuuliza hivi humu JamiiForums kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba. Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa. Lakini kila siku zinavyosogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazoota.
 
Wakuu naomba kuuliza hivi humu jamiiforum kuna kijana yeyote ambaye yupo chini ya miaka 30 ambae anamiliki gari na nyumba.Yani ambae ametafuta kwa jasho lake bila kupewa au kurithi.

Nimeuliza hivi kwa sababu mimi nina miaka 25 na ndoto zangu ni kumiliki gari na nyumba kabla Sijaoa.Lakini kila siku zinavyo sogea naona ndoto inakua ngumu kutimia.

Nikipita barabarani au kwenye kumbi za starehe naona vijana wadogo wamepaki magari yao, basi roho yangu inaumia sana.

Hivi inawezekana kweli au ni ndoto za mchana hizi ninazo ota.

Mkuu Usipoiba kwa kipindi kilichobaki Haki ya Mungu sikudanganyi ... Labda ukatoe kafara
 
Njoo 'machimboni' ujionee unaweza kujutia ni kwanini nilienda chuo kusoma mavitu magumu kinoma wakati short cut ya maisha ipo huku! Yaani miaka 22 wewe tayari ni 'fogo' unaye itwa 'mzee' 'mkurugenzi'
Hmm.. Huko mambo ya kufukiwa hapana asee. Yaan uhai wangu utoke kwa ajili ya manufaa ya watu wengine.? Big Noo
 
Huo umri wasomi wapo shule, ila wajanja wa mitaa wanamiliki hivyo vitu. ..na wanaona ni kawaida sana kumiliki...hakuna shidaa...hata mm vipo....kuviona na kuvitumia ni bure...vigezo na masharti kuzingatiwa
Na hio 25yrs ndio umri sahihi wa kumiliki hizo Mali....otherwise jitafakari!!!
 
Back
Top Bottom