Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,589
- 28,755
Ni vyema ukamwambia, wanaume sometimes huwa wanajua mambo mengi sana kuhusu wake zao lakini wanajitia kutokujua lolote.
Achana na kumwambia kipato chako ila toa hela unapoona gap na kufanya maisha ya familia yawe bora, mambo ya kumtajia mshahara unaweza kumsababishia mumeo kutojiamini, ukifanya chochote ataona unamdharau kwa sababu umemzidi kipato. Funga mdomo wako kwa habari ya kipato chako labda aulize.Mimi nimeokoka na nishakuwa mtu mzima, nataka niwe mkweli kwa mume wangu, ila sipendi ajue kama nimemzidi kipato. Sijui nifanyeje!!!!
Mfano mwanaume hakulizi chumo lako au pato lako kwa mwezi, lakini unajua pato lake kwa mwezi, unajua kinachotoka na kinacho ingia katika account yake.
Anakulisha na kukununulia nguo na vitu unavo penda.
Na haja omba nunua kitu au changia kitu, hadi kodi ya nyumba analipa yeye, peke yake.
Una nunua gari, mume hakulizi, anajua pesa umezitoa kwenye kijikampuni chako.
Kwa mfano una miliki milion 50 benki, ila mume hajui. Unanunua gari lenye thamani ya milion 35, mume anafikiri umebangaiza bangaiza huku na kule kwa tabu. Unamiliki, shamba kubwa moja na kiwanja kimoja. Na nyumba moja mbovu yenye thamani ya milion 30.
Mume anachopata ni milion 2 hadi 3 kwa mwezi.
Anamiliki milion 8 benki.
Gari yake milion 10.
Mume ana kiwanja kimoja na shamba moja.
Lakini munaishi nyumba ya kupanga sehemu. Kodi analipa yeye, laki 4 kwa mwezi.
Mahusiano yenu hakuna anaefuatilia chumo la mwenzie sana, kinachopatikana asante mungu, kinachokosekana asante mungu. Akiba ipo, itafaa siku ya dhiki.
Mume hajui unamzidi milion 5 kwa mwezi mfano.
Hivi ikitokea mume anataka kujua ulicho nacho, na akagundua umemzidi pato, je inakuwaje?
Kuna mtu ana experience humu ndani, ya hii kitu?
anawaza sana..
wewe ule uvae watoto
wasome na kodi..
atachoka
atazeeka mapema
mwisho atakufa kwa mawazo
kwa ubinafsi wako watoto watakosa baba,..toa kidogo kwa ajili yake angali hai hata kama si chote atafurahi ataongeza siku za kuishi na wewe
Achana na kumwambia kipato chako ila toa hela unapoona gap na kufanya maisha ya familia yawe bora, mambo ya kumtajia mshahara unaweza kumsababishia mumeo kutojiamini, ukifanya chochote ataona unamdharau kwa sababu umemzidi kipato. Funga mdomo wako kwa habari ya kipato chako labda aulize.
Inawezekana tayari anahisi una kipato kikubwa lkn ameamua kuwa mume na baba wa familia anatimiza majukumu yake. Kuondoa mgogoro wowote unaohofia uwe unatoa kwa ajili ya familia, ufidie vile anavyojinyima ili kuitunza familia.Asante, niliwaza labda mapenzi yake kwangu, yatapungua akijua!!!!! nitakaa kimya, ila nahofia siku akiniuliza tu, nitatetemeka,,,, nimjibu vipi? sijui? sijapiga mahesabu? inabidi nijibu kitu ambacho kisiwe cha uongo, na ambacho hakita mfanya hasijiamini, sijui unanishauri vipi?
Kama issue yako ni kuogopa kuulizwa usitengeneze mazingira ya kuulizwa basi, mkiwa na furaha mwambie kwa upole kwamba kwa kuwa na wewe ni mfanyakazi unaona usaidie katika kutunza familia, unaweza kusema utashughulikia mambo ya kuhakikisha nyumbani kuna chakula, nyumba iko katika hali nzuri maybe na mavazi. .. mf. Ishu za kupendezesha nyumba sijui mapazia, mashuka, decor n.k wakati yeye analipia watoto ada n.k unaweza kuchangia kodi mara moja moja usizidishe ataona unatishia uanaume wake katika familia... Inawezekana anahisi una hela ila ukimwambia utakuwa umemhakikishia na namna fulani umetangaza kitisho kwa uwezo wake wa kukutawala kwa mumeo. Ila ukijichagulia majukumu ya nyumbani hapa na pale hatakuwa na sababu ya kukuuliza unapata sh. Ngapi. Atashukuru tu kupata mke mwema asiye mzigoAsante, niliwaza labda mapenzi yake kwangu, yatapungua akijua!!!!! nitakaa kimya, ila nahofia siku akiniuliza tu, nitatetemeka,,,, nimjibu vipi? sijui? sijapiga mahesabu? inabidi nijibu kitu ambacho kisiwe cha uongo, na ambacho hakita mfanya hasijiamini, sijui unanishauri vipi?
Kama issue yako ni kuogopa kuulizwa usitengeneze mazingira ya kuulizwa basi, mkiwa na furaha mwambie kwa upole kwamba kwa kuwa na wewe ni mfanyakazi unaona usaidie katika kutunza familia, unaweza kusema utashughulikia mambo ya kuhakikisha nyumbani kuna chakula, nyumba iko katika hali nzuri maybe na mavazi. .. mf. Ishu za kupendezesha nyumba sijui mapazia, mashuka, decor n.k wakati yeye analipia watoto ada n.k unaweza kuchangia kodi mara moja moja usizidishe ataona unatishia uanaume wake katika familia... Inawezekana anahisi una hela ila ukimwambia utakuwa umemhakikishia na namna fulani umetangaza kitisho kwa uwezo wake wa kukutawala kwa mumeo. Ila ukijichagulia majukumu ya nyumbani hapa na pale hatakuwa na sababu ya kukuuliza unapata sh. Ngapi. Atashukuru tu kupata mke mwema asiye mzigo