Kuna ubaya mwanamke akikuzidi kiuchumi?

Kuna ubaya mwanamke akikuzidi kiuchumi?

Yahitaji busara sana ili usiumize his ego mana wanaume bwn hakuna anaependa Kuonekana kazidiwa,litafakari kwanza,we unamjua mumeo, akiwa in a good mood siku mmetulia au mnaweza kutoka/kusafiri mwambie kwa unyenyekevu,nna jambo sikuwahi lisema mana sijui utalichukuliaje ila naona ni vema nikwambie km mume wangu,Mwambie kipato chako na salio ulilonalo na unatamani mfanye nini mf kuongeza nguvu mjenge,kulipa Ada nk nk,then heshima yako kwako isije kushuka hata siku mojaa,iweke mbele kama Tai,then sikiliza mwongozo wake
Akinuna overtime mtulize na usigusie tena habari za hela yako endelea kusave tu akiba haiozi ipo siku itasaidia family yenu
 
wewe ndiyo mwokovu? Unayeomba ushauri wa njia gani nzuri ya kudanganya?

Kweli shetani anakutumia bila wewe kujijua, hata Anania na safira walikuwa wanamtumikia shetani bila wao kujijua wakificha sehemu ya fedha na kuwadanganya watumishi wa Mungu.

Nyie ndiyo wale wanaojazana katika makanisa ya maombezi, siyo mnamtaka Huyu Yesu, bali ni wapenda maombi na kuombewa, ila kubadilika hamtaki.

Na ninyi ndiyo mnasababisha jina la Bwana linatukanwa kwa matendo yenu yasiyoendana na wokovu.

Ushauri wangu kwako:
mrudie Mungu kwa toba. Alafu anza kuishi kama neno la Mungu linavyotaka uwe. Siyo kuwa Mbuzi badala ya Kondoo.

Mwisho:
uwe muwazi kwa mumeo usikubali shetani akutumie kumdanganya maana mwisho wake ni Haibu na kumdhalilisha Yesu kwa mumeo na watu.

Usipende kuishi maisha ya kuiga watu. Na kushauriwa mambo yasiyojenga bali ubomoa nyumba yako.

Hishi maisha matakatifu.kwa kulifuata neno la Mungu Soma Kitabu cha Mithali 31: ujifunze sifa ya mke mwema.

Ndio maana nikasema nataka niwe mkweli kwa mume wangu, kila kitu kitawezekana kwa jina la yesu.
Kuwa mlokole sio kujua kila kitu kwa siku moja, na ndio maana tunaenda kanisani kuelimishana neno la mungu ili tusipote. Na kunawakati tunapotea bila kujijua, na tunaitaji ushauri. Nami niliona naitaji ushauri niliona kama sipo sahihi,

Asante kwa ushauri,
 
anawaza sana..
wewe ule uvae watoto
wasome na kodi..

atachoka
atazeeka mapema
mwisho atakufa kwa mawazo

kwa ubinafsi wako watoto watakosa baba,..toa kidogo kwa ajili yake angali hai hata kama si chote atafurahi ataongeza siku za kuishi na wewe
Umeniskitisha Benny, its true jamani imagn akifa kwa mawazo halafu ww unarundika hayo mahela utafkiri utazikwa nayo hayo makaratasi. Muonee hurumaa bana
 
we dada umeokoka afu unaishi bila ndoa
shenz type..

maana ungekua umeolewa wala usingekuja na hii thread..

maana majority ya ndoa ni umoja,,na wanandoa inatokea automatically tu kila mtu mnajua mnapata kiasi gani mnapanga budget yenu vizuriiiiiiii
 
Mimi nimeokoka na nishakuwa mtu mzima, nataka niwe mkweli kwa mume wangu, ila sipendi ajue kama nimemzidi kipato. Sijui nifanyeje!!!!

Mfano mwanaume hakulizi chumo lako au pato lako kwa mwezi, lakini unajua pato lake kwa mwezi, unajua kinachotoka na kinacho ingia katika account yake.

Anakulisha na kukununulia nguo na vitu unavo penda.
Na haja omba nunua kitu au changia kitu, hadi kodi ya nyumba analipa yeye, peke yake.

Una nunua gari, mume hakulizi, anajua pesa umezitoa kwenye kijikampuni chako.
Kwa mfano una miliki milion 50 benki, ila mume hajui. Unanunua gari lenye thamani ya milion 35, mume anafikiri umebangaiza bangaiza huku na kule kwa tabu. Unamiliki, shamba kubwa moja na kiwanja kimoja. Na nyumba moja mbovu yenye thamani ya milion 30.

Mume anachopata ni milion 2 hadi 3 kwa mwezi.
Anamiliki milion 8 benki.
Gari yake milion 10.
Mume ana kiwanja kimoja na shamba moja.

Lakini munaishi nyumba ya kupanga sehemu. Kodi analipa yeye, laki 4 kwa mwezi.

Mahusiano yenu hakuna anaefuatilia chumo la mwenzie sana, kinachopatikana asante mungu, kinachokosekana asante mungu. Akiba ipo, itafaa siku ya dhiki.
Mume hajui unamzidi milion 5 kwa mwezi mfano.

Hivi ikitokea mume anataka kujua ulicho nacho, na akagundua umemzidi pato, je inakuwaje?

Kuna mtu ana experience humu ndani, ya hii kitu?

Mi nilijua walokole hawaongopi [emoji15]
Hadi leo unamwongopea mumeo loh
 
kuna mtu nilikuwa nabishana nae kuwa mwanamke akiwa anafanya kaz ni sahihi mwanaume kubeba majukum yote au ni vzur kusaidiana,jamaa akawa anasema wanawake wa sasa hawana nia ya kumsaidia mwanaume financialy,hata kama ana mill we una laki atataka akale na hako kalaki kako,akasema bora ukomae uwe na kipato kikubwa kumzid ukave majukum yote.sasa na humu tena naona maoni tofaut,interestng
 
Huyo siyo mke bali mwanamke kunatofauti kubwa sana.
Mke atawaza na kufocus kuijenga Nyumba ya familia from kipato cha mume na chake bali mwanamke atamnyonya mume na kipato chake vyote atajenga kwao.
Mtoa mada ukimfuatilia kwa karibu atakuwa kajenga kwao kimyakimya. Ndiyo maana nasema alikuwa hajawahi kuwa mke wa jamaa bali mwanamke kama wanawake wengine tendo la ndoa siyo sababu coz jamaa anaweza lipata kwa wanawake wengine hivyo hakuna tofauti.
Mke ni zaidi ya tendo la ndoa vivyo hivyo kwa mume.
 
Hakuna mwanaume mjinga kiasi hiko,
Hapo anakuangalia tu, lini utajirudi mpange maisha pamoja
 
Kama unaona mumeo ana kuhusu kwanin usimwambie hilo pato lako na hivo vihela unavyo ficha benki???anajua unahongwa ndio maana ameamua kukaa kimyaa.
 
Mwanzo nilikuwa simpendi sana, Ila sasa najisikia nampenda sana na sana, sijawai kuwa na wivu namna hii toka nizaliwe, lakini sasa wivu wangu kwake unapamba moto, hata kanisani nimeanza kuwakasilikia wanawake wanao jaribu kuongea nae.
Hapo mwanzo alikua anaongea na kila mtu, ila siku hizi nawivuuuu akiongea na mwanamke na hata mke wa kaka yake, roho inaniuma, natamani kulia naona wivu. Hadi najishangaa.

Ndio nimeokoka na sipendi ajisikie kushuka thamani yake, ama anione hawezi kunitunza eti kwa sababu namzidi pato. Au kama wewe ungefanyaje kwenye situation kama hii?
Somoe, sasa naanza kukuelewa if those you're talking/writing are truth.
Umesema kwa sasa unampenda mmeo na kumuoneo wivu sana kuliko wakati wowote, hii inaonyesha there're things big and nice anakufanyia, sasa mtu anayekufanyia mazuri ukafurahia kwanini nawe usimfurahishe hadi naye akuonee wivu sana?

Mwanamke kumzidi kipato mwanaume siyo jambo geni wala hujaanza wewe na hii dhambi ya kumficha ni mbaya sana hata inafanya ibada yako isiwe na thamani mbele za Mungu.

Kuwa wazi kwa mmeo, wanaume hawajioni vibaya wake zao kuwazidi kipato, bali ujiona vibaya pale wenza wao wanapotumia hicho kipato chao kuwadharau nakuwanyanyasa waume zao.

Nimewahi kuwaona wanandoa, mke akiwa na Shahada na mmewe akiwa na Diploma, mke mshahara wake ulikuwa ni mara 7 ya mshahara wa mme lakini mme hakuwahi kujisikia vibaya kwasababu ya heshima aliyokuwanayo yule mwanamke. Kipindi wanajenga karibia pesa yote ya ujenzi aligharamia mwanamke lakini hakuna fundi yoyote aliyejua kuwa pesa anatoa mwanamke. Siku wanayokwenda wote site kabla hawajafika site mama anatoa kiasi cha pesa inayotakiwa anampa mme wake wakifika site jamaa anatoa pesa mfukoni kwa mbwembwe na mikwara mingi na kuwalipa wafanyakazi.

Nakushauri umwambie ukweli mmeo hasa kama hiyo pesa unayoipata yote ni ya halali kama ni magumashi hacha hayo mambo, nafsi yako haikuhukumu kwa hiki unachomtendea mwenzako, kuona yeye pamoja na kipato chake kidogo anajitahidi kutimiza majukumu yote ya nyumbani pamoja na kukhudumia wewe japo una kipato kikubwa kumzidi?

Women you have to change your thinking about men, waoneeni huruma waume zenu mtawapunguzia magonjwa ya Kiarusi, msongo wa mawazo na vifo vya mapema.
 
Umeniskitisha Benny, its true jamani imagn akifa kwa mawazo halafu ww unarundika hayo mahela utafkiri utazikwa nayo hayo makaratasi. Muonee hurumaa bana
Kweli kabisaa...
vyote tutaviacha hapa kwa kidogo
tunachopata familia iwe ya kwanza
 
Labda kama ni hawara ndio unaweza kumficha lakini sio mume.
 
Hivi mnaishije hivyo kwa kufichana maana ya ndoa in nini.mweleze ukweli tena kwa upole na upendo vinginevyo hawa wenzetu wana ule msemo mwanamke akiwa nacho anakua na kiburi. So usimpe hiyo picha ya yy kutamka maneno hayo.
Chako chake chake chako bana kaeni muongee
 
Asante, niliwaza labda mapenzi yake kwangu, yatapungua akijua!!!!! nitakaa kimya, ila nahofia siku akiniuliza tu, nitatetemeka,,,, nimjibu vipi? sijui? sijapiga mahesabu? inabidi nijibu kitu ambacho kisiwe cha uongo, na ambacho hakita mfanya hasijiamini, sijui unanishauri vipi?

Uongo ni gojwa ktk ndoa usithubutu kudanganya
 
Kwa kipato hicho ni ujinga km bado mnaishi nyumba ya kupanga. Alafu we inaelekea ndie unaetaabisha familia yako mwenyewe, thamani ya mume hujajua bado. Umesahau kuwa maendeleo yoyote ktk familia ni ya kwako kabisa na watoto wako pia. Sasa sijui unamtegea nani hapo km unaona mume atafanya kila kitu hapo umechelewa. Iko Siku unataka kumshirikisha mmeo lakini utakuwa umechelewa sana
 
we dada umeokoka lakini ni mjinga na mpuuuuzi wa kutupa.

unasema mmeoana na kila mtu anamiliki vitu vyake kwenye familia moja na wewe gari la mil. 30 yeye 10. kabisa seriously unaongea hivyo mbele za watu na unajiita umeokoka, shame on you.

mwenzio anakuhudumia kila kitu akijua wewe yako ya kufanyia maendeleo. ndo maana wanaume wanatoka nje kwasababu akipata mtu anayemthamini hata kidogo lazima atembbe naye.

furaha haipo kwenye gari wala vitu.

mi napata mshahara 1.5ml na mke wangu anajua na tunakaa mezani tunapanga maendeleo yeye ana degree lakini anasimamia tumiladi. wewe ficha sasa unadhan kupata mil. 7 ni mali kubwa wakati ni pesa ndogo sana

najua thread yako inayofata itakuwa "mume haeleweki" au "mume anatembea na mdogo wangu au house gal"
 
Shikamoo dada Somoe,

Kwa upeo wangu, hapo upo kwenye mtihani mzito. Unaweza kumweleza ukajenga, au ukaharibu. Inategemea yeye ni mtu wa aina gani.

Nionavyo, ni vyema ukamuandaa ajue chumo lako unalipataje huku ukiwa tayari na wazo la kumshirikisha namna ya kulisawazisha na lake ili muwe sawa. Hii itamfanya akuthamini. Lakini kusema umwambie tu ajue kuwa unachuma zaidi yake, then what?!

Mungu akujaalie wakati unamweleza, ukweli usio na chembe ya shaka utawale.

Kila la heri.
 
we dada umeokoka lakini ni mjinga na mpuuuuzi wa kutupa.

unasema mmeoana na kila mtu anamiliki vitu vyake kwenye familia moja na wewe gari la mil. 30 yeye 10. kabisa seriously unaongea hivyo mbele za watu na unajiita umeokoka, shame on you.

mwenzio anakuhudumia kila kitu akijua wewe yako ya kufanyia maendeleo. ndo maana wanaume wanatoka nje kwasababu akipata mtu anayemthamini hata kidogo lazima atembbe naye.

furaha haipo kwenye gari wala vitu.

mi napata mshahara 1.5ml na mke wangu anajua na tunakaa mezani tunapanga maendeleo yeye ana degree lakini anasimamia tumiladi. wewe ficha sasa unadhan kupata mil. 7 ni mali kubwa wakati ni pesa ndogo sana

najua thread yako inayofata itakuwa "mume haeleweki" au "mume anatembea na mdogo wangu au house gal"
Yaani hapo ndo tunapojishusha hadhi wanawake tulioolewa mtu unafanya kazi au shughuli yoyote ya kukuingizia kipato then hujui mnatumia umeme wa sh.ngapi. Kumsaidia majukumu mume kunaonesha umuhimu wako ndani humo na heshima yako kama mke inavyoongezeka. Tatizo wanaingia kwenye ndoa na mindset ya ndoa itakuja kuvunjika siku na kila mtu anaficha mali zake. Kama mtu umeamua kushare naye maisha yako na umempa uhuru na mwili wako na anaweza kukudhuru kirahisi kwanini unamficha mali zinazotafutwa na ambazo zinakuja na kuondoka?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom