Yahitaji busara sana ili usiumize his ego mana wanaume bwn hakuna anaependa Kuonekana kazidiwa,litafakari kwanza,we unamjua mumeo, akiwa in a good mood siku mmetulia au mnaweza kutoka/kusafiri mwambie kwa unyenyekevu,nna jambo sikuwahi lisema mana sijui utalichukuliaje ila naona ni vema nikwambie km mume wangu,Mwambie kipato chako na salio ulilonalo na unatamani mfanye nini mf kuongeza nguvu mjenge,kulipa Ada nk nk,then heshima yako kwako isije kushuka hata siku mojaa,iweke mbele kama Tai,then sikiliza mwongozo wake
Akinuna overtime mtulize na usigusie tena habari za hela yako endelea kusave tu akiba haiozi ipo siku itasaidia family yenu
Nami naona hivo hivo wengi wao hawapendi kuzidiwa, sasa na huu uwokovu???
Mama yangu aliniambia wanaume wengine wakiona umemzidi hela, ataanza kuwa na akili ya kutaka kukufilisi. Ama atakupumbaza na kukuaribia mipango yako na hata atataka uache kazi, ili akumiliki ama akutawale.
Shangazi yangu aliniambia kuhusu pesa zangu mwenyewe nisimuoneshe wala kumpa mwanaume, mwanaume akijua unazo pesa ataomba umkopeshe halafu hakurudishi.
Shangazi yangu amejenga nyumba yake mwenyewe, lakini anaishi kwa mumewe. Na mumewe anajua mali za mkewe. Na huyu mwanaume anatumia hizi mali za mkewe na mke anatumia za mume. Naomba kwa mungu familia yangu iwe hivi hivi.
Kwa sababu dada yangu mkubwa alijenga nyumba na mumewe, baada ya miaka 15 yule mume alifariki. Yule mume alioa na kuzaa mtoto mmoja kabla ya dada yetu.
Vile vile alizaa na mchepuko watoto mapacha.
Jamaa wa mume wakatumia majambazi kumfukuza dada yetu na watoto wake wanne.
Wale jamaa wa mume wakajazana na kuenjoy life katika ile nyumba.
Mahakama wakasema waridhi wa nyumba ni watoto, hivo warudi mahakamani mpaka mtoto wa mwisho atimize miaka 18. Mtoto wa mwisho alikua na miaka 2 na nusu.
Mke akifariki kwanza mume hasumbuki, ila mume akifariki kwanza mke atatabishwa na watoto.
Jamaa wa mume walitumia wale watoto 3 kama chambo cha kumfukuzia yule dada. Tamaa ya mali mungu wakamsau,
Mahakama inaangalia situation na kufuata sheria zao, haifuati sheria za mungu.