Kuhusu Tatizo la Uchafu Dar, Madrassatul Abraar tuna wazo litakalokuwa suluhu ya kudumu

Naomba kwanza tumsikilize Mkuu wa Mkoa.

View attachment 1822533

Video clips zinachelewa kupanda lakini In shaa Allah tutazipandisha, ni muda tu.

Baada ya kumsikiliza mkuu wa mkoa na tatizo la uchafu na biashara kuwa kiholela mitaa ya Dar. AlhamduliLllah Madrassatul Abaraar darasa la vifaa vya ujenzi tumekuja na suluhisho la kipekee, la kudumu, na lisilo na gharama kubwa na kutakuwa na mvuto wa kipekee kwenye jiji la Dar na sehemu yoyote vitapotumika Abraar Kiosk.

Abraar maana yake ni Waja wema. Na ndio jina la tulivyovipa vinbanda vyetu kwa kuwa Mkuu wa Mkoa kaongea kwa hisia kubwa sana, hauna shaka kabisa kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mja mwema na anaendana kabisa na fikra za waja wema. Kwani tunaamini kuwa usafi ni imani, asie na imani hafikirii usafi na asiye na imani hawi Mja Mwema aka Abraar.

Kuanzia viosk, vibanda vya walinzi wa usiku madukani, vibanda vya mawakala wa kampuni za simu, vinabda vya mawakala wa banks, vibanda vya ATM, vibanda vya wauza soda na juisi, vibanda vya vinyozi, vinabda vya sokoni. Mapipa ya taka ya kudumu. Vibanda vya matangazo ya biashara, vibanda vya stand za mabasi, vibanda vya stand za dala dala. Ni bidhaa ya ubunifu wa hali ya juu.

Vibanda vitatengenezwa kwa aina ya msonge (mduara) wa zege linalohamishika na hakuna sehemu au pahala ambapo havitahitajika. Kuanzia vibanda vya walinzi wa Mabenki, Maduka ya Fedha, Vituo vya mafuta. Vibanda vinaweza kuwa na ghorofa moja, juu na chini na vikahamishika kwa urahisi, vyote vitakuwa ni vya kuunganisha kiurahisi tu.

Havihitaji ufundi wa hali ya juu, vimeshapimwa mzunguko wa mduara kutoka vinapoundwa darasani kwetu. Ni kupanda tu zege letu kavu, hakuna kukosea vipimo kwani tayari tumeshavipima na aneviweka anavipachika tu.

Pia tumebuni aina kadhaa za kuviezeka kwa urahisi na kwa mvutio wa kipekee.

Vifaa hivyo vyote vinatengenezwa kwa asilimia zaidi ya 60 na akina mama, asilimia iliyobaki ni vijana wetu wanojifunza ujenzi hapa Madrassatul Abraar.

Vifaa hivyo kwa mzunguko mdogo (diameter ndogo) vinaweza kuwa mapipa ya kuudu ya taka, hakuna kuibiwa wala kuharibika na vinaweza kuwa maitained hapo hapo vilipo vikawa vinapendeza daima. Maisha ya Abraar Kiosk au Abraar Pipa vikiwa kazini ni miaka 50 mpaka 100 na vinahamishika ki wepesi bila hasara yoyote ya kuvibomoa itapohitajika kuhamishika kupisha maendeleo.

Kwa wawekezzaji wa kibiashara ni fursa hiyo kuleta mitaji yenu tuvizalishe kwa wingi gharama zipungue nanyi mpate faida mkiviuza. Vinaweza kutumika Tanzania nzima, si lazima iwe Dar Pekee.

Tumeshaanza kuviunda vya sample na kabla hatujavimaliza kuna mama lishe hapa Madrassatul Abraar kishaanza kukitumia, anasema yeye hangoji kiishe.

Wasiliana na Mzee Abdul Ghafur kwa maelezo zaidi 0625249605
Vinajengwa kama vile vya CocaCola na TCC ?
 
Hilo ndilo suluhisho lililotakiwa miaka yote ila kwasababu waliona kupiga faini ni chanzo cha mapato hawakutaka kusikia. Unamwambiaje mtu asitupe taka hovyo na huku sehem za kutupa ni za kuzitafuta?
Kama mkuu wa mkoa atakuwa seriuos kweli atakubaliana na wazo lenu. Au atafanya njia mbadala inayofanana na hiyo.
 
Of course, share tunayo hapo, kila Muislam, hujaona kuwa ni wazee wa Madrassa? Unafikiri zinajinedesha zenyewe?
Kwani kuna shida gani huko?.
Hajatajwa mtu wamejibiwa kama wote!.

👉🏾Hii ndiyo tunaita jiwe gizani.
 
Kwani kuna shida gani huko?.
Hajatajwa mtu wamejibiwa kama wote!.

👉🏾Hii ndiyo tunaita jiwe gizani.
Haswaa, hillo jiwe la kizani alikuwa anatupiwa ndege au ngedere?

Fumbo mfumbie mjinga mwenzio.

Sisi ndio wadau wa Madrassa, hilo jiwe lako limenipiga. Wewe ulietupa jiwe, dini yako inakufundisha kutupa mawe kizani?

Tumeanza na Mzee Abdul kupitia hapa hapa JF kuanzia miaka inakaribia 10 sasa kama sio zaidi, toka alipoanza mkewe ku introduce Aunt Zainab's Natural Super Clay, akaja mzee Abdul na SACCOS ya Kimataifa. Tupo nae, na sasa anabuni mambo ya ujenzi, tupo nae na In shaa Allah tunaendelea kuwa nae, kwani kajidhihirisha kuwa ni mtu mbunifu, mchapa kazi, na hakuna kinachomkwamisha.

Vineno vyenu vya kijinga hivyo kama yeye hana muda wa kuvijibu basi elewa kuwa tupo sisi wadau wa miradi yake tutawajibu.

Tunafahamu kuna watu mliosomea ujinga roho zenu zinazidi kuungua mkiona jinsi wazee wa Madrassa wanayozidi kuwa pioneers, tokea kabla ya Uhuru mpaka leo hii. Si siasa si huu ubunifu wa Abdul, yote imeasaidia kunyanyua maisha ya jamii nzima.

Mtakufa navyo vijiba vya roho.

Unalo zaidi?

cc: Mohamed Said
 
Una kimbelembele we Bibi wewe , pimbi kabisa @@£&&())))***""':!!!!!@€$¢¢¢
Wewe usiye na adabu, mamako alikuzaa kinyuma nyuma? Jilete wewe kinyume nyume, watu kama wewe licha ya maneno ya kina waleee hata ID zenu zinaonyesha kuwa ni waleee, hamuwezi kujificha.
 
Maalim, kwanini usitume hapa, uko whatsapp utawatumia wangapi aisee, huoni kama ni mzigo,

tuma hapa kwa faida ya wengi/wote
Najaribu sana, huku tulipo mtandao wetu si mwema sana ku upload video clips.

Ngoja nijaribu kuzi screen shot video clips nipandishe picha. Hakuna kisichowezekana.

Pia mtu anaweza kujiunga na Telegram Messenger au Whatsapp group zetu tuna update mara kwa mara.
 
Picha chini zinaonesha kina mama wapo katika kuandaa jalala la pili la taka za kuchomwa. Ambazo badala ya kuwa ni iero na uchafuzi wa Mazda ngira zinageuka kuwa ni mbolea na dawa ya asili ya baadhi ya wadudu wanmazqo.

Jalala la kwanza ni a plastiki (polymers) ambazo ni hatari zaidi Kwa mazingira. In Shaa Allah siku za usoni tutaelekeza jinsi ya kujipatia pesa Kwa kutumia uchafuu huo wa mazingira wa plastiki zilizotumika na taka za kuchomwa badala ya kuzitupa hovyo na kuchafua mazingira.

Abraar Bricks Nyumba kwa Wote ni ujenzi wenye ubora wa Hali juu kwa gharama nafuu kwa faida ya wengi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.
20210624_082511.jpg
20210624_082503.jpg


20210624_082458.jpg
 
Naona kama unafanya style fulani kutoipandisha
Video ya vizimba hivyo humu jf,unalazimisha watu waione whatsap
Sijui kama ni kweli unashindwa ku upload humu

Ova
tumeanza kupandisha humu kila hatua tunayokwenda nayo.

Haulazimishwi kufungua whatsapp, umeambiwa ukipenda au ukihitaji kujua zaidi.

Utuwie radhi sana sana kama hilo limekuudhi, nafahamu kuwa yote hiyo ni shauku ya kuona "wazee wa Madrassa wana kipi kipya" Kuna wengi wamekuja whatsapp na tumewarushia video cloips kadiri tuwezavyo.

Ni kweli kabisa kuna nyakati mtandao huku kwetu, hususan kukiwa na mawingu, unakuwa tabu sana ku upload video clips. Sio kuwa inashindikana bali inakuwa vigumu kwa kuwa inabidi tuache kufanya mambo mengine tusubirie zinapanda taratibu sana.

Pitia pitia uzi huu mara kwa mara utaziona hizo za ubunifu tuliouandika humu na ubunifu mwengine mwingi tu.

Abdul: 0625249605
 
tumeanza kupandisha humu kila hatua tunayokwenda nayo.

Haulazimishwi kufungua whatsapp, umeambiwa ukipenda au ukihitaji kujua zaidi.

Utuwie radhi sana sana kama hilo limekuudhi, nafahamu kuwa yote hiyo ni shauku ya kuona "wazee wa Madrassa wqwana kipi kipya" Kuna wengi wamekuja whatsapp na tumewarushia video cloips kadiri tuwezavyo.

Ni kweli kabisa kuna nyakati mtandao huku kwetu, hususan kukiwa na mawingu, unakuwa tabu sana ku upload video clips. Sio kuwa inashindikana bali inakuwa vigumu kwa kuwa inabidi tuache kufanya mambo mengine tusubirie zinapanda taratibu sana.

Pitia pitia mara kwa maara utaziona hizo za ubunifu tuliouandika humu na ubunifu mwengine mwingi tu.

Abdul: 0625249605
Kwa kukuweka sawa tu
Wala sioni tatizo au shida nyie wazee wa madrasa kufanya jambo kama hilo

Ova
 
Bila picha ya kibanda siwezi changia kwa kweli
naona ni vizimba vya kuwekea uchafu
Sasa swali langu kwake hivyo vizimba vinahishika,kubebeka au watu wakishatupa
Hapo taka,wakandarasi wa taka wanakuja hapo
Kubeba taka kutoka hapo

Ova
 
Back
Top Bottom