Kero ya uunganishwaji holela wa umeme kwenye masoko ya jioni jijini dar es salaam

Pyremethazine

New Member
Dec 21, 2018
2
0
Habarini wakuu.
Kumekua na masoko mengi jijini dar es salaam. Ambayo kutokana na kadhia wanazopata wakati wa mchana kutoka kwa mamlaka za jiji. Wafanyabiashara wa masoko hayo. Wao wameamua kufanya biashara zao nyakati za usiku.

Hivo kua na uhitaji wa umeme katika maeneo hayo. Lakini pamoja na kutoa huduma hizoo za uuzaji mahitaji mbalimbali .Kumekua na changamoto ya uunganishwaji holela wa huduma ya umeme kwenye vibanda hivyo.

Inakadiriwa vibanda 15 au zaidi. Vyote vikawa vinategemea sehemu moja ya kuchukulia umeme. Na ambayo haina uwezo wa kugawa kwenye vibanda vyote hivyo kwa ufanisi.

Uunganishwaji huo umekua ni hatari kiasi kwamba unahatarisha maisha ya wao
wafanyabiashara,mali zao na watumiaji wa masoko hayoo.

Waya na vifaa vingine vinavotumika kuunganishia umeme huo ni vyenye uwezo mdogo na visivyo na ubora kabisaa. Pia namna ya uunganishwaji imekua ni mbaya kiasi kwamba viungo vya waya hizo hufungwa na mifuko ya plastic na kupitishwa kwenye njia ambapo watu hupita.

Na ikizingatiwa kwa kipindi kama hiki ambacho Mvua zinanyesha. Inapelekea kua na hatari zaidi kwa watumiaji wa maeneo hayo .Hivyo mamlaka husika kuna umuhimu wa kufuatilia na kuangalia ni namna gani wanaweza kutatua changamoto hiyoo.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom