KERO Wilaya ya Ubungo kinara wa uchafu jiji la Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jebel

JF-Expert Member
Jul 10, 2021
336
2,218
Salaam,

Natambua vema kuwa kuna maeneo mengi tu jijini Dar Es Salaam ambayo ni machafu mfano Tandika sokoni, Vingunguti sokoni……n.k lakini wilaya ya UBUNGO inabakia kinara wa UCHAFU kwa hoja zifuatazo;

1. Umeshawahi kupanda daladala za Makumbusho-gerezani/Mnazi/au Posta? Kama ndivyo je daladala ishawahi kusimama kwa sekunde kadhaa pale kwenye mataa ya u-turn ya Shekilango? Kama ndiyo basi bila ubishi utakubaliana nami kuwa 15% ya harufu mbaya hapa DSM inatokea eneo lile la MACHINJIO YA KUKU- SHEKILANGO

2. Je, kuna anayefahamu soko la MANZESE, MACHINJIO YA KUKU SOKONI MANZESE? Ndugu yangu kama wewe ni mwanamke na una mimba changa tafadhari usithubutu kusogea karibu na soko lile. Na kama umepita na kagari kako kenye hakana ac please kubaliana tu na joto kwa kupandisha vioo la sivyo uvundo utakaoupata pale kuisha kwenye gari ni baada ya week nzima. Soko lile linazalisha 20-25% ya harufu mbaya hapa jijini DSM

3. Je, ushawahi kufika MAHAKAMA YA NDIZI NA MATUNDA- MABIBO? Hapa sintaandika chochote

4. Kama bado unabishia hoja zangu basi pita eneo la big-brother kuelekea uzuri ile njia inayotokea Tandale ujionee mifereji ya maji machafu…(yanayotumika kumwagilia mchicha unaolimwa eneo la NHC Ubungo).

Pendekezo binafsi la SULUHUSHO.
Siyo ukomavu kuibua kero bila kutoka pendekezo la suluhisho
- BINAFSI naona kuna haja na ulazima wa mamlaka za usafi wa mazingira, uongozi wa wilaya na mkoa kuungana kwa pamoja na KUPIGA MARUFUKU UCHINJAJI WA KUKU katikakati ya mji. Honestly huu ni ushamba sana na ukosefu wa vision kuruhusu uchinjaji wa wanyama katikati ya mji. Yaani karne hii kweli KUKU wanachinjiwa mjini?

Ukifanya utafiti mdogo utagundua kuwa kuku wanaochinjiwa katika masoko ya Manzese na Shekilango na maeneno mengine ya jiji la Dar wanaletwa kutoka Kibaha na mikoani. Sasa mamlaka zinashindwa kweli kuwaamuru wafanyabiashara ya KUKU kuingiza mjini kuku waliokwishachinjwa. Kwamba wafanyabiashara hawawezi kumdu kujinunulia mafreezer ya kutunza nyama ya KUKU na kuiuza kama nyama nyingine. Ni lazima kuku waletwe mjini wakiwa hai?

- BINAFSI nadhani hata ng’ombe na mbuzi ingepigwa marufuku ya kuwaingiza mjini wakiwa hai badala ya au litengwe eneo nje ya jiji ambapo shughuli zote za uchinjaji zitafanyika na nyama tu ndo iingizwe mjini. Yaaani kweli ng’ombe aletwe kutoka Murusagamba hadi Segerea?

MAMLAKA CHUKUENI HATUA.

Mlale salama, na mfungo mwema kwa wale waliobahatika kuwa Waislam.
 
Bado sisitizo litakuwa lile lile Cha kwanza ni elimu Cha pili elimu na tatu ni elimu chanzo Cha uchafu na harufu mbaya kwa dar ni wakazi wake wenye ambao kwa makusudi huchafua maeneo either wanayokaa au Yale wasiyokaa kwa kutengeneza taka hovyo na kuzitupa hovyo tuanze na elimu ya utunzaji wa mazingira shuleni tutengeneze sheria Kali kudhibiti uchafu
wazo lako la uchinjaji kuku ni zuri nadhani tuanze utaratibu wa kuuza nyama ya kuku kutoka kiwandani na sio kuku hapa Nina maana kuwa kunakuwa na kiwanda sehemu flani ambacho kitaandaa kuku na wauzaji wataenda pale na kununua Kisha kusambaza kwa walaji kwa kupitia masoko hivyo basi haitaruhusiwa kuwa na uchinjaji wa kuku sokoni ni au umnunue mzima shambani au nyama buchani
 
Dar karibu yote ni chafu, kuna maeneo machache sana kama Masaki, Oysterbay, Mikocheni (ushuani), Msasani (ushuani), Mbezi Beach (ushuani) na baadhi ya sehemu za Mbweni, Ununio ndio walau kunatazamika...
 
Back
Top Bottom