Kuhusu matukio mengi ya ajali za barabarani, ukiachana na uzembe wa madereva barabara zetu ni changamoto

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,612
Ukiachana na kuendelea kuwalaumu madereva, bado barabara zetu ni changamoto kubwa kwa usalama wa watumizi wa barabara hizo, barabara nyingi ni ni nyembamba (unforgiving roads )zisizo kuwa na mbadala ambazo zinashindwa kupunguza idadi ya vifo na majeruhi pale ambapo dereva atafanya makosa.
-
Japokuwa ukweli ni kwamba siku zote binadamu hata acha kufanya makosa, sheria za barabarani ni lazima zifuatwe na mamlaka husika kuwa macho kushughulikia utekelezaji na kuchukua hatua stahiki pale ambapo ukiukwaji utajitokeza.
-
Moja kati ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya madereva wazembe ni kuwanyang’anya leseni, lakini je,hii itakuwa na faida gani pale ambapo bado miundo mbinu ni mibovu na hatarishi?

Kwa mfano barabara ya morogoro ni kati ya barabara ambazo zimegharimu maisha ya watu wengi sana ndani ya muda mfupi. Hii ni kutokana na ongezeko la watumizi wa barabara hiyo ambayo imekuwa nyembemba sana na imekua ngumu kwa madereva ku over take bila kusababisha ajali. Barabara hii ikipanuliwa ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana
-
Mashimo, viraka bumps kubwa na wembamba wa barabara ndio vyanzo vikubwa vya ajali za barabarani kwa sasa, je mtazamo wako ni upi kuhusu suala hili?
 
Sababu kubwa ni kiwango duni cha elimu dunia.

Basis of cognition power - ni elimu dunia. Hii ndiyo inayomfanya kuwa mstaarabu. Mstaarabu hawezi kuendesha gari achilia mbali lori bila breki.

Angalizo: Si elimu ya uendeshaji gari wala kinachoitwa elimu ya usalama barabarani.

Wasomi kibao wasiokuwa na ajira wangechangamkia fursa hii wakaonyesha mfano.

Minimum formal education si jambo la kubeza.
 
Pia madereva wanaendesha hovyo hovyo bila kujali na kufuata sheria za barabarani.

Inahuzunisha na kusikitisha kuona magari mengi Yana paki Bar bila uwoga wakimaliza kunywa wanaendesha tu
 
Madereva wengi sahv wanaendesha ovyo

Wakati wetu tu naendesha ajali zilikuwa syo kama sasa

Ova
 
serikali yenu sikivu huwa inakwepa sana lawama za ajari barabarani ila kiukweli barabara zetu zinachangia sana ajari, kwanza ni nyembamba pia lami ina mawimbi sana, yule shujaa aliyekufa kwa moyo alituhujumu sana
 
Ukiachana na kuendelea kuwalaumu madereva, bado barabara zetu ni changamoto kubwa kwa usalama wa watumizi wa barabara hizo, barabara nyingi ni ni nyembamba (unforgiving roads )zisizo kuwa na mbadala ambazo zinashindwa kupunguza idadi ya vifo na majeruhi pale ambapo dereva atafanya makosa.
-
Japokuwa ukweli ni kwamba siku zote binadamu hata acha kufanya makosa, sheria za barabarani ni lazima zifuatwe na mamlaka husika kuwa macho kushughulikia utekelezaji na kuchukua hatua stahiki pale ambapo ukiukwaji utajitokeza.
-
Moja kati ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya madereva wazembe ni kuwanyang’anya leseni, lakini je,hii itakuwa na faida gani pale ambapo bado miundo mbinu ni mibovu na hatarishi?

Kwa mfano barabara ya morogoro ni kati ya barabara ambazo zimegharimu maisha ya watu wengi sana ndani ya muda mfupi. Hii ni kutokana na ongezeko la watumizi wa barabara hiyo ambayo imekuwa nyembemba sana na imekua ngumu kwa madereva ku over take bila kusababisha ajali. Barabara hii ikipanuliwa ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana
-
Mashimo, viraka bumps kubwa na wembamba wa barabara ndio vyanzo vikubwa vya ajali za barabarani kwa sasa, je mtazamo wako ni upi kuhusu suala hili?
IMG-20220328-WA0289.jpg
 
Mabus ni ovyo sana barabarani mpaka unajiuliza yapo above the law au?
 
Mi naona labda wangeweka umri wa dereva wa lori kuanzia tone fulani au gari la abiria uwe angalau umri fulani wa mtu mzima hii angalau ingesaidia kupunguza maana anakuwa na hafu hata ya familia

Lakini hii unakuta dereva wa lori ana miaka 20 ana drive mlori unaenda nchi jirani huko hawezi kuwa na hofu wala mawazo ya familia anaendesha kama akili inavyomtuma hizi ajali hazitakaa ziishe kwa mtindo huu.

Kingine hii style ya kampuni kuweka sheria lori aendeshe dereva haku a kuwa na kondakta nayo inachangia maana dereva kuna kuchoka akili kwa upweke hadi anasinzia wakati anaendesha
 
Tatizo linguine magari yamechoka

Ajali ya mbeya Lori number A

Tanga namba A

Geita namba A

Gari ikitokea Japan ukaguzi ni lazima ikiingia ndani ndio umetoka hiyo, gari odometer imefika mpaka mwisho bado tu ipo barabarani
 
Mkuu sikupingi kwa ulichokiandika, ila binafsi nasisitiza nidhamu ya hali ya juu sana tuwapo barabarani!

Upanuzi wa hizo barabara utachukua muda mrefu sana, sasa kwanini sisi wenyewe tusiwe na nidhamu juu ya matumizi ya barabara ili kupunguza madhara wakati tunasubiri upanuzi?

Utovu wa nidhamu unamchango mkubwa sana kwenye hizi ajali!!

HATUNA NIDHAMU BARABARANI..
 
Ajali sio barabara kama ni hivyo na sisi watembea kwa miguu kila siku tungeanguka maana mashimo na madimbwi tunayaona ila tunayakwepa kwa usalama wetu ila kama akitokea mtu kaanguka ni mzee sana hana balance

Sasa huyo mzee ni sawa na gari bovu
Magari mengi hayabadilishwi matairi wala break pads kwa mda mrefu sana

Hilo kusababisha ajali za kizembe
Shock ups mbovu akidumbukia kwenye Shimo dogo tu lazima gari au pikipiki iache njia

Lingine ambalo nalo ni kubwa zaidi ni udereva
Jamani udereva ni taaluma pia unajifunza tahadhari zote

Huku kama unataka kuchukua leseni unaingia training ya uhakika

Kwanza magari makubwa ndio balaa
Mtihani wake unakariri na kusoma maswali 900 halafu multiple choices yanakuja maswali 100 katika hayo 900
Lazima ufaulu 87%

Halafu kuna Hazard perception ya video unaangalia gari likienda halafu una clic hazards unayoiona nayo kupasi marks ni 67
Baada ya hapo unajifunza kuendesha halafu unaingia mtihani wa reverse peke yake halafu ukiwa tayari kuingia barabarani unaulizwa maswali kuhusu gari

Ndipo unapelekwa road kwa saa moja hiyo unalipa 1m ya kibongo ukifeli kuanza upya

Sasa ukinolewa hivyo na gari huwezi kuendesha bila MOT kuvhunguzwa hitilafu kila mwaka

Sasa laumu madereva wabovu wasiojua kuendesha kwa nidhamu na kutokujua wapi akimbize na wapi aende polepole
Wapi apishane na wapi asubiri
 
Back
Top Bottom