Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani SACP Ng'anzi asema "Toeni taarifa za Madereva wasiotii Sheria na Kanuni za Usalama"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi amewataka abiria wanaosafiri ndani na nje ya Mkoa Ruvuma kutoa taarifa za baadhi ya madereva wanaokiuka Sheria za Usalama Barabarani.

Hayo amesema Desemba 23, 2023 alipotembelea Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo nje ya Mkoa ya Shule ya Tanga iliyopo Manispaa ya Songea ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya moto Mkoani Ruvuma.

Pia kwa upande wa Madereva wa mabasi amewataka kuendesha kwa kujihami na kuchukua tahadhali wakati wote wawapo safari ili kulinda usalama wao, abiria na watumiaji wengine wa barabara.
50c44833-74bb-4594-beff-f566e4faa7aa.jpeg

aa6305b7-3f95-4789-88fc-c6009b57902b.jpeg

d5f4d5d6-5242-4422-9d81-8cce6a3f6e71.jpeg
Aidha, alimalizia kuwasisitiza Madereva wote ambao wanaosafiri kwa umbali mrefu kuhakikisha wanatii Sheria za Usalama Barabarani sambamba na kuachana na matumizi ya vilevi kwani chanzo cha ajali nyingi husababishwa sababu hizo.

Sambamba na hilo SACP Ng'anzi kwa kushirikiana na askari wengine wa Kikosi cha Usalama Barabarani alimalizia kwa kukagua mifumo mbalimbali ya mabasi ikiwa pamoja na Mfumo wa breki, Mataili, ubora wa magari pamoja na kuwapima ulevi madereva wote kabla ya kuwaaruhusu kuanza safari zako.
 
Na vipi kuhusu vijana wake wala rushwa kote nchini! Taarifa tunapeleka wapi? Au wamehalalishwa kula hizo rushwa.
 
Back
Top Bottom