Abiria watakiwa kupaza sauti kwa Madereva wasiofuata Sheria za Usalama Barabarani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Abiria wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya wametakiwa kupaza sauti kwa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Hayo yamesemwa Disemba 21, 2023 na Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mrakibu wa Polisi Hussein Gawile mara baada ya kuwasili katika Stendi ya Mabasi Tarafani iliyopo katika Mji mdogo wa Mbalizi.

Mrakibu wa Polisi Gawile amewataka abiria wanaosafiri kwenye mabasi kutoka Mbeya kwenda maeneo mengine kutofumbia macho vitendo vya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na badala yake amewataka kupaza sauti kukemea na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
424cb71d-bc75-4da6-a73a-d9acb043ece9.jpeg

c84d4296-93c5-4658-9828-51fe814fca16.jpeg

c5dfdb2a-8230-467a-956b-dd45e2cba2bf.jpeg
Aidha, amesisitiza na kuwataka madereva kutoa wa mabasi ya abiria kutoa Tiketi kwa abiria wao kama sheria na taratibu za usafirishaji abiria zinavyoelekeza.

Naye, Afisa habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya Koplo Esther Kinyaga alipata wasaa wa kuzungumza na madereva na kuwataka kila dereva kuhakikisha anakuwa na kifaa cha kuzimia moto (Fire Extinguisher) ndani ya gari yake ili endapo tukio la moto likitokea kiweze kusaidia katika kuzima moto huo.

Vilevile, Koplo Kinyaga amesema kuwa "Ni vema madereva na abiria kuwa na namba ya dharura ya Zimamoto na Uokoaji 114 ambayo kimsingi itakuwa njia rahisi ya kupata msaada mara baada ya ajali ya moto kutokea" alisema Koplo Kinyaga.

Balozi wa Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya ndugu Yona Mbeleka amesema kuwa ili kupunguza ajali za barabarani ni vema abiria wakawa mstari wa mbele kupaza sauti kwa kutoa taarifa za madereva ambao ukiuka sheria za usalama barabarani ili wachukuliwe hatua za kisheria kabla ya kusababisha ajali.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia dawati la elimu kikosi cha usalama barabarani kwa kushirikiana na mabalozi wa usalama barabarani, chama cha kutetea haki za abiria linaendelea kutoa elimu ya usalama kwa madereva huku abiria wakisisitizwa kupaza sauti kupitia kampeni ya Abiria Paza Sauti (APS) ili kuepuka ajali za barabarani.
 
Back
Top Bottom