fungi06
JF-Expert Member
- Jul 1, 2020
- 633
- 857
Ajali za barabarani zimekuwa zikileta kilio kwenye familia zetu nyingi hapa Tanzania na kupoteza wapendwa wetu wengi.
Huu mwaka tuu nimepoteza marafiki na ndugu watatu kwa ajali tuu za barabarani na wote wameacha watoto na familia zinazowaangalia. Hii ni kwangu na ninajua kwa wastani wa nchi yenye watu milioni 60 na zaidi, sio mimi pekee niliekumbwa na misiba ya wahanga wa ajali barabarani. Familia nyingi zitakuwa zinaugulia mfano; ndugu yetu pia aliegongwa na kunusurika na mwendo kasi miezi kazaa hapo nyuma.
============
Njia itakayosaidia mno kupunguza ajali;
1. Mifumo ya cctv za barabarani
Naona serikali imejitahidi na taasisi zake za barabarani kwa kuweka mafungu ya pesa kwaajili ya kuandaa walimu na syllabus kufundishia namna yakupunguza ajali barabarani.
Sikatai kuwa ni smart moves lakini hiyo kamwe haitopunguza ajali barabarani milele, labda itaongeza kujitambua mapema kwa wanafunzi walengwa. Ila tukiangalia hata nchi zilizo endelea zenye wasomi wa hali ya rocket kwenda Mars sio elimu tuu inayotolewa bali pia na kamera zinafungwa kila barabara kuzuia uendeshaji mbovu.
Kwanini kamera?
Psychology inaonyesha kuwa mtu akijua anaangaliwa au anarekodiwa hupunguza error kutokea na kuongeza kujitambua kwa kiasi.
Tumekuwa tukiona baada ya saa 22 jioni watu wakishajua polisi wamepumzika basi wao huwa ndio muda wa kupima uwezo wa gari kukimbia na kujiamulia kuvunja sheria kwa sababu wanakuwa hawaonekani.
Mfano, marehemu rafiki yangu aligongwa na magari ya mzigo huko Holili Moshi pembeni ya barabara ila hawakumkamata msababisha ajali, inasemekana gari lilikuwa linausajili wa namba za Kenya🤔.
Inauma sana kupoteza kaka, rafiki, baba, ndugu kwa kuporwa nafsi yake na dereva asie makini na bado dereva huyo akafanikiwa kukimbia!
Huu ni muda wa kuwekeza nguvu mno kwenye teknologia, tunaitaji safety control measures, CCTV kamera zikifungwa basi itakuwa rahisi mno kwa polisi na madereva kupunguza ajali vile vile pia kupunguza vifo na bajeti za hospitali za gafla.
Mimi huwezi niambia mtu alale hospital miezi 9 na kuacha kuihudumia familia yake kwa kosa la dereva mzembe ambae angejua anaangaliwa na kamera angebehave kama human.
Kamera za barabarani ni mwarobaini wa ajali za barabarani, elimu inafwatwa after discipline tendered.