Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,604
Wanabodi
Nijitambulishe tena na tena, kuwa japo mimi Paskali Mayalla, ni mwandishi tuu wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, na kwa sasa mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kupitia uzoefu wangu wa utangazaji, navuananasheria wangu, ninawaletea kipindi kipya cha TV kiitwacho "KMT" .

Hivyo nina mamlaka ya kuikosoa mahakama kwa kutotenda haki, na nimekuwa nikiandika sana makala kutoa elimu ya katiba, sheria na haki kupitia safu yangu ya kwa Maslahi kwa Taifa, sasa safu hii haishii kuandika tuu magazetini na mitandaoni, safu hii sasa inakwenda hatua moja mbele, inakwenda hewani kupitia kipindi cha TV cha KMT- "Kwa Maslahi ya Taifa", kitakuwa kinarushwa hewani kila siku za Jumapili Saa: 3:00 usiku na marudio siku za Jumatano Saa 9:30 alasri kupitia Channel Ten, ni kwa kuanzia tuu, baadae kipindi hiki pia kitarushwa na TBC, ITV, Star TV, na Azam TV, ili elimu hii ya Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, iwafikie Watanzania wengi zaidi.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=uSiW3_dfU58l3B-V

Kipindi cha kwanza ni mahojioano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Elieza Mbuki Feleshi kuhusu uwezo wa Mahakama zetu kutenda haki.

Siku za nyuma niliandika makala 5 mfululizo za kilio cha Haki, na miongoni mwa hoja zilizoniibua kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Jaji Feleshi, ni baada ya moja ya makala hizo ku challenge uwezo wa Mahakama zetu kutoa uamuzi wa haki. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Mtamsikia wenyewe AG, Jaji Feleshi akijibu, ila hii hali ya Mahakama zetu kutotenda haki kwa kitu kinachoitwa legal technicalities, kinaendelea! na mfano mzuri wa haki kutotendeka kwa legal technicalities ni hii hukumu ya kina Halima Mdee na wenzake 18!

Kwa kawaida kesi ikiwa inaendelea Mahakamani, hairuhusiwi kujadiliwa ili kuepuka kuingilia uhuru wa Mahakama, lakini baada ya hukumu kutoka, ni rukhsa kuijadili kesi husika.

Jana Mahakama Kuu imetoa uamuzi kuridhia uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafuta uanachama wa wabunge wake 19 wa viti maalum wa Chadema kwa kosa la kughushi kujiteua. Ila Mahakama imewakubalia kwa kupinga uamuzi wa Baraza Kuu, Chadema kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema huo hivyo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiitishwe upya kusikiliza rufaa zao.

Uamuzi wenyewe ni huu
1. The Prerogative Order of Certiorari is granted to quash the decisionpassed by the Governing Council of the 1st respondent on the 11thday of May 2022 and formally published on the 12th May, 2022.
2. The Prerogative Order of Mandamus is granted to compel the 1strespondent to observe the due process and Principles of NaturalJustice in determining questions/matters affecting the applicants'rights.
3. No order is made as to costs. Right of appeal is fully explained

Kwa maoni yangu, uamuzi huu wa Mahakama sio uamuzi wa haki hata kidogo! kwasababu msingi wa wabunge hao kufungua shauri mahakamani ni kupinga kufutwa uanachama, kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni. Baada ya kikao cha Baraza Kuu Chadema kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema kuwatimua, ndipo wabunge hao wakakimbilia mahakamani kutafuta haki kwa kupinga uamuzi wa Baraza Kuu Chadema kuridhia uamuzi wa CC Chadema kuwatimua!.

Japo Mahakama imepindua uamuzi wa Baraza Kuu Chadema,
Mahakama ni kama iimewapa ushindi Chadema, kuwa CC ya Chadema imewatimua kina Mdee kihalali!. Na kuwa wabunge hao hawakupinga uamuzi wa CC wa kuwatimua bali wamefungua kesi kupiga uamuzi wa Baraza Kuu kuridhia uamuzi and CC ya Chadema kuwatimua, mahakama imebatlisha uamuzi wa Baraza Kuu, kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema hivyo wengi kuwaona kina Mdee kama washindi wakati mahakama ni imebariki kutimuliwa kwao!. Sababu Mahakama ilizotoa kupindua uamuzi wa Baraza Kuu Chadema, ni very silly reasons!. Kwa mujibu wa katiba ya Chadema iliyoridhiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, wajumbe wa CC ya Chadema ni wajumbe halali wa Baraza Kuu Chadema na wabunge halali wa Mkutano Mkuu Chadema!, Mahakama haina uwezo kuwapangia Chadema wajumbe wa vikao vyao halali kwa mujibu wa katiba yao!

Nimeisoma hukumu,
1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CC ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!. Niliuliza humu Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?. Hili pia niliuliza humu A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!. Hapa nilimpongeza Halima, "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji, Jee kitendo cha Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team of Kangaroos?.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.

Paskali.
 

Attachments

  • In the Matter of an Application for Orders of Certiorali Mandamus and Prohibition by Halima Ja...pdf
    2.4 MB · Views: 3
Kipindi hicho kitazungumzia kuhusu masuala ya Elimu ya Katiba, Sheria na Haki au kitazungumzia juu ya Suala la Hukumu ya Kesi ya akina Halima Mdee?? Mbona unajichanganya?? Mada ni elimu ya Katiba, Sheria na Haki, lakini ukifanya content analysis kuhusu hili bandiko lako unaona kwamba umejikita zaidi kuzungumzia suala la kesi ya wale Wabunge 19 na Chama cha Chadema. So, which is which?
 
Wanabodi
Nijitambulishe tena na tena, kuwa japo mimi Paskali Mayalla, ni mwandishi tuu wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na mtangazaji wa kujitegemea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea,

Paskali.
Hongera sana mkuu.

Naomba ufafanuzi; unamaanisha nini unaposema ni wakili wa kujitolea? Unatoa msaada wa kisheria bila malipo?
 
Mzee Paskali, kwenye hoja namba 3 ondoa neno CCM umeiweka kimakosha nadhani ulikusudia CC.
Inasomeka "kikao cha CCM ya CHADEMA" kitu ambacho nadhani hakipo au pengine mimi ndio sijui.
 
Mkuu wewe unajulikana ni mwana CCM damu, ndio maana umeandika "CCM ya Chadema!"

Kutokana na hilo ushauri wako kwa Chadema hauwezi kuchukuliwa kuwa wenye nia njema au usio egemea upande! Kimsingi unaweza kuizungumzia CCM vizuri zaidi kuliko mpinzani wako.

Mkuu wewe mwenyewe kwenye andiko lako hili unakiri kuwa kuna shida kwenye maamuzi ya mahakama zetu kama alivyowahi kusema kada mkongwe mwenzio ndugu Rostam Aziz!

Mkuu kuwa makini usiharibu mapishi ya Makala yako hayo ya kwenye TV. Maana Dibaji yako hii inafikirisha........
 
Hongera mkuu, kwa nafasi yako najua tutapata uhondo wa mahojiano na watu muhimu nchini.

Pamoja na hilo ni muhimu CDM wajifunze kufuata taratibu zao wenyewe, kama hizo tu zinawashinda je wataweza kufuata na kutii katiba ya nchi ikiwa wataingia madarakani??
 
Kipindi hicho kitazungumzia kuhusu masuala ya Elimu ya Katiba, Sheria na Haki au kitazungumzia juu ya Suala la Hukumu ya Kesi ya akina Halima Mdee?? Mbona unajichanganya?? Mada ni elimu ya Katiba, Sheria na Haki, lakini ukifanya content analysis kuhusu hili bandiko lako unaona kwamba umejikita zaidi kuzungumzia suala la kesi ya wale Wabunge 19 na Chama cha Chadema. So, which is which????????
Eti huyu naye ni wakili
 
Kipindi hicho kitazungumzia kuhusu masuala ya Elimu ya Katiba, Sheria na Haki au kitazungumzia juu ya Suala la Hukumu ya Kesi ya akina Halima Mdee?? Mbona unajichanganya?? Mada ni elimu ya Katiba, Sheria na Haki, lakini ukifanya content analysis kuhusu hili bandiko lako unaona kwamba umejikita zaidi kuzungumzia suala la kesi ya wale Wabunge 19 na Chama cha Chadema. So, which is which?
Mkuu John Wickzer Mulholland , kwanza asante kuchangia uzi wangu, kipindi ni kuhusu elimu kwa Umma kuhusu katiba, sheria na haki, kesi ya kina Halima Mdee imeingia kama mfano hai, a living example jinsi Mahakama zetu zinavyo finyanga haki kupitia legal technicalities.
P
 
Back
Top Bottom