Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za Binadamu, Wakili Onesmo Olengurumwa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Rufaa Na. 165 ya mwaka 2021 kuhusu kupinga vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vinavyoruhusu washtakiwa kushtakiwa kwenye mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza kesi hizo (committal Proceedings) imeahirishwa mpaka itakapopangiwa siku nyingine ya kusikilizwa.
Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa leo February 12, 2024 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania,jijini Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani Mhe. Jaji Sehel, Mhe. Jaji Kente, na Mhe. Jaji Masoud saa 3:00 asubuhi
Upande waleta rufaa baada ya kufika mahakamani wameomba ahirisho kutokana na Jaji mmoja kati ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya Rufani (Mhe. Jaji Masoud) kuwa alikuwa katika sehemu ya majaji wa mahakama kuu walioshiriki katika kesi hiyo ambayo uamuzi wake umekatiwa rufaa kwenye mahakama ya rufani kabla hajateuliwa rasmi kuwa Jaji wa mahakama ya rufani.
Akifafanua kuhusu ombi hilo Wakili Paul Kisabo amesema kuwa taratibu za kimahakama zinamnyima nafasi Jaji huyo kushiriki tena kwenye uamuzi akiwa Jaji wa mahakama ya Rufani kama alikuwa sehemu ya majaji wa mahakama kuu waliosikiliza kesi hiyo.
Upande wa Jamhuri kupitia mawakili wake wamekubaliana na ombi hilo ambapo Mahakama itapanga siku nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kwa kulingana na ombi husika.
Itakumbukwa Rufaa hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania masijala ya Dar es Salaam uliotolewa mwaka 2020 ambapo Mahakama kuu ilitupilia mbali kesi hiyo.
Vifungu vinavyolalamikiwa ni kifungu namba 178, 243, 244, 245, 246, 247, 248, 249, 250, 256, 257,258 na 259 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Katika Mahakama Kuu Wakili Olengurumwa aliitaka mahakama itoe amri ya Kubatilisha vifungu hivyo vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai akidai vinakiuka Katiba na haki za binadamu kwa mfano haki ya kusikilizwa kwa usawa, usawa mbele ya sheria pamoja na haki nyingine ambazo zipo katika Ibara ya 13 (1) (2) na (6) (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app