Kiongozi Mwandamizi wa CHADEMA akutana na Kikwete, Kinana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa

Mama alitoa hivyo vyote kama hisani au rushwa??! Na Mbowe anaonewa ili kuonesha makucha na mapembe ya mama? Usitutukanie mama yetu! Suala ni moja tu, kama anahusika ni kosa, kama hahusiki ajitabainishe!
Anayekuja kiungwana, unamhandle kiungwana. Anayekuja kipumbavu, unam handle KIPUMBAVU zaidi!! Nyoko zenu
 
Yaani ukiingia humu Mara Tweeter Ni Mbowe tu, ata Samia afanye mazuri yapi watu Wana muignore, lakini acha kumtetea ameyataka mwenyewe na hii kesi aliibariki
Kuna wahuni walimuingiza mkenge Ili achukiwe na watu bila sababu maana hyo ilimfanya Hadi akakosa nafasi ya kukutana na kina Biden sifa nzuri na mwanzo alioanza nao vikaharibika, mi nashauri hii case ifutwe tu ina mharibia mno, maana hata ushahidi huko mahakamani ni ujinga mtupu, mbona kikwete aliruhusu wapinzani kubwabwaja Hadi wakachoka, tena aliruhusu siasa ni kuwaacha hata Wana ccm wapambane na wapinzani huko wenyewe na wao waache makundi ndani ya chama Ili apumue
 
Mkuu kuna points katika unayosema. Lakini kinachotushangaza baadhi yetu ni harakati zinazoshika kasi za kutaka Mbowe na CHADEMA wamuombe msamaha Rais SSH (hadharani) ili afute kesi hiyo ya ugaidi na Mbowe kuwa huru. Ni kama vile SSH anataka sana kuifuta hiyo kesi (almost desperate)!

Kwanza, kuna dharura yoyote au umuhimu mkubwa kiasi hicho kwa SSH kesi hiyo ikifutiliwa mbali?
Hata UAMSHO walipokuwa ndani Kuna watu waliwapigania sana watoke. Hata Babu Seya Kuna watu walihusika kumuombea atoke na wanaye
 
Kuna wahuni walimuingiza mkenge Ili achukiwe na watu bila sababu maana hyo ilimfanya Hadi akakosa nafasi ya kukutana na kina Biden sifa nzuri na mwanzo alioanza nao vikaharibika, mi nashauri hii case ifutwe tu ina mharibia mno, maana hata ushahidi huko mahakamani ni ujinga mtupu, mbona kikwete aliruhusu wapinzani kubwabwaja Hadi wakachoka, tena aliruhusu siasa ni kuwaacha hata Wana ccm wapambane na wapinzani huko wenyewe na wao waache makundi ndani ya chama Ili apumue
Kikwete alikuwa mjanja sana, aliwaacha wakabwabwaja yeye pesa mabeberu wanammwagia na sifa kemkem, kina Obama, Bush, Xin p wote walikuja bongo, Samia hakuna nchi ya ulaya inayomuamini Tena, ndo akome yeye alihukumu siku Ile ya BBC, siwez mtetea
 
Acha kujishushia heshima.....

Acha kuishushia heshima ofisi ya mh.Rais....

Kwanza umeongopa.....

Halafu unamtaja kuwa ni MSHAURI hapohapo unamuita mtoa MAELEKEZO.....are you serious?!!!!

Ni lini MSHAURI akawa mtoa MAELEKEZO?!!!
Poyoyo mwenzako wa Lumumba huyo. Hajui hata nani ni nani. CCM mmejazana vilaza wa kutupwa.
 
hawa chadema sometimes ni wa ajabu Sana . sasa unahangaika kwa wastaafu sijui kikwete. Mara kinana Mara warioba kuwaambia mbowe hana hatia. Harafu inatokea chance Kama ya juzi ya kuonana na mtesi wao wanasusa mkutano . hivi mfano chadema wangehudhuria juzi harafu wakayaongea hayo mbele ya rais huoni kuwa wangekuwa wamefanya jambo la maana zaidi. Sasa wanahangaika na wazee sijui akina mangula , butiku waende wakamwambie rais aifute kesi . rais huyohuyo akitaka kuonana nao ili asikilize malalamiko yao uso kwa uso hawataki. Chadema hii mbinu sidhani Kama itasaidia .
"hawa chadema sometimes ni wa ajabu Sana".
Nawe umeamini!!!???
Pole sana.
 
Wanashitaki watu kwa kuwashinda hoja. Hivi vyama vinavyojiita vya ukombozi afrika vimegeuka na kuwa wakoloni weusi. Vinaongozwa na watu wa hovyo wasiojua kujenga hoja hata ya kumshawishi mtoto wa nursery awasikilize. Wamebakia kuteka, kuua na kubambika kesi. Hovyo kabisa.
 
hawa chadema sometimes ni wa ajabu Sana . sasa unahangaika kwa wastaafu sijui kikwete. Mara kinana Mara warioba kuwaambia mbowe hana hatia. Harafu inatokea chance Kama ya juzi ya kuonana na mtesi wao wanasusa mkutano . hivi mfano chadema wangehudhuria juzi harafu wakayaongea hayo mbele ya rais huoni kuwa wangekuwa wamefanya jambo la maana zaidi. Sasa wanahangaika na wazee sijui akina mangula , butiku waende wakamwambie rais aifute kesi . rais huyohuyo akitaka kuonana nao ili asikilize malalamiko yao uso kwa uso hawataki. Chadema hii mbinu sidhani Kama itasaidia .
"hawa chadema sometimes ni wa ajabu Sana".
Nawe umeamini!!!???
Pole sana.
 
Haina ubishi wanufaika wakubwa wa siku 100 za kwanza za Rais SSH ni CDM, Mbowe na Mdude kwa maelekezo, falsafa na haiba ya Samia. Mpaka tukaandika threads nyingi za kusema "Mama anaupiga mwingi

Ningetegemea Mbowe na Lissu watumie busara katika madai yao kwa kuwa wasikivu na wavumilivu pale Samia aliposema suala la Katiba lisubiri ajenge uchumi

On the contrary Mbowe na Lissu wakaanza kumfokea Rais kama vile ni mbunge wa BAWACHA?? Na Mdude akasema " nitamnyoa mama yenu kwa wembe uleule nilio mnyolea mtangulizi wake

Nini kikiwapata hawa watu ambao kwa Mwendazake waliufyata miaka 5. Mwendazake kawapiga risasi, kavunja Bilicanas na kavunja na mashamba yake, kamchukulia na fedha kwenye akaunti. Hajawahi hata kulalamika

Samia kamrudishia akaunti, kesi zao za kubambika zikapigwa chini pamoja na ya MDUDE. Halafu wao ndiyo wa kwanza kusema HATUWEZI KUMBEMBELEZA Samia
Lisu angeufyata mngempiga Risasi?
 
Anayekuja kiungwana, unamhandle kiungwana. Anayekuja kipumbavu, unam handle KIPUMBAVU zaidi!! Nyoko zenu
Kama mlivyomhandle Lisu siyo?. Putin alisema kweli kumbe. Mpe mtu mweusi bunduki atafanya unyama mbaya sana kwa mweusi mwezake kuliko ambao angefanaya mweupe.
 
Kama mlivyomhandle Lisu siyo?. Putin alisema kweli kumbe. Mpe mtu mweusi bunduki atafanya unyama mbaya sana kwa mweusi mwezake kuliko ambao angefanaya mweupe.
Hata yeye mwenyewe Vladmir Putin si mvumilivu kihivyo kwa upinzani. Yeye ndiye mteja mkubwa wa polonium
 
Haina ubishi wanufaika wakubwa wa siku 100 za kwanza za Rais SSH ni CDM, Mbowe na Mdude kwa maelekezo, falsafa na haiba ya Samia. Mpaka tukaandika threads nyingi za kusema "Mama anaupiga mwingi

Ningetegemea Mbowe na Lissu watumie busara katika madai yao kwa kuwa wasikivu na wavumilivu pale Samia aliposema suala la Katiba lisubiri ajenge uchumi

On the contrary Mbowe na Lissu wakaanza kumfokea Rais kama vile ni mbunge wa BAWACHA?? Na Mdude akasema " nitamnyoa mama yenu kwa wembe uleule nilio mnyolea mtangulizi wake

Nini kikiwapata hawa watu ambao kwa Mwendazake waliufyata miaka 5. Mwendazake kawapiga risasi, kavunja Bilicanas na kavunja na mashamba yake, kamchukulia na fedha kwenye akaunti. Hajawahi hata kulalamika

Samia kamrudishia akaunti, kesi zao za kubambika zikapigwa chini pamoja na ya MDUDE. Halafu wao ndiyo wa kwanza kusema HATUWEZI KUMBEMBELEZA Samia
🤣🤣 🤣 🤣 Atoe hoja ya kipuuzi ya kusema anajenga uchumi kwanza ndiyo afikirie mambo ya katiba halafu watu wenye akili wakae kimya? Upeo wako ni mdogo sana. Yaani unadhani unafiki ni bora kuliko ukweli? .
 
Jitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amekutana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani.

Haijaweza kufahamika kama jitihada hizo ni za Mnyika binafsi au zina baraka ya chama hicho, ambacho kwenye mitandao ya kijamii kimetanabaisha kuwa hakitaki suluhu yoyote kuhusiana na kesi hiyo.

Taarifa hizo zinaeleza kwamba kimsingi Mama Samia Suluhu aliridhia ombi la kuachiwa kwa Mheshimiwa Mbowe na ilitarajiwa aachiwe kwa “nolle prosequi” (tamko la nia ya kutoendelea na mashtaka) ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) lakini “yaliyojiri kabla, wakati na baada ya mkutano wa vyama vya siasa huko Dodoma” yalipelekea mpango huo kukwama.

Licha ya jitihada hizo za Mnyika, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman nae aliwasilisha maombi ya Chadema kwa Mama Samia, na akashauri Mheshimiwa Mbowe aachiwe bila masharti yoyote.

Uamuzi wa Chadema kususia mkutano huo wa vyama vya siasa huko Dodoma ambao ulifunguliwa na Mama Samia, inatajwa kuwa moja ya sababu zilizopelekea kukwama kwa mpango huo wa kumwachia Mheshimiwa Mbowe.

Taarifa hizi zinakinzana na kauli zinazoongewa na viongozi na wafuasi wa chama hicho kuwa “hawako tayari kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe” kwa sababu wanaamini kuwa hana hatia na mashtaka dhidi yake ni ya kutungwa.

Yawezekana tofauti hizo kati ya “kinachoendelea faraghani” na “kinachoongelewa hadharani” zikawa ni mkakati wa Chadema hasa ikizingatiwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho hawaafiki kabisa wazo la kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe. Moja ya sababu zinazochangia “msimamo huo mkali” ni shinikizo la “wanaharakati wa mtandaoni” ambao wanapinga vikali siasa za maridhiano kati ya chama tawala CCM na vyama vya upinzani.

Hata hivyo, suala hilo la kesi ya Mbowe “limevamiwa” pia na kundi moja ndani ya CCM linalompinga Mama Samia, na ambalo linaiona kesi hiyo dhidi ya Mheshimiwa Mbowe kuwa yenye manufaa kwa kundi hilo kwa sababu inatoa taswira mbaya kuhusu Mama Samia.

Nihitimishe kwa kutanabaisha kuwa haitokuwa jambo la kushangaza endapo Mheshimiwa Mnyika atakanusha taarifa hizi kwa sababu “zinaweza kumletea tabu” katika chama chake.

Jumanne njema
Mkutano jwa uzi uliofanyika dodoma nikama vile ccm walitaka kuomba msamaha Ili kuridhiana na wapinzani lakini wanapita njia siyo

1,wanashindana kukiri kufanya foulo uchaguzi 2020
2. Wanashindwa kusema hadhsrani kuwa mikutano yakiasas ruksa

3, wanashindwa kukubali tumehuru na katiba mpya
4. Wanashindwa namna ya kumtoa huru mh. mbowe na kufuata kesi ya michomgo
 
Ni Mnyika ambaye alihimiza taifa lipewe taarifa rasmi za Alipo mkuu wa nchi !

Mnyika ni "dhaifu".
 
Kikwete alikuwa mjanja sana, aliwaacha wakabwabwaja yeye pesa mabeberu wanammwagia na sifa kemkem, kina Obama, Bush, Xin p wote walikuja bongo, Samia hakuna nchi ya ulaya inayomuamini Tena, ndo akome yeye alihukumu siku Ile ya BBC, siwez mtetea
Kikwete alijuaga kula na kipofu na alikuwa anawaruhusu hata wapate wabunge hamsini majimboni mengine anawakata, aliruhusu uhuru tofauti na jiwe yeye aliiba Hadi ikawa ujinga serikali ikakosa hela nyingi kwa kutokuwa smart, ila na CDM nao waache ukaidi maana hata mbowe hakutumia busara tulitoka msibani tena mkubwa uliokuwa shock tulikuwa kwenye transition ngumu wao wakaanza harakati za katiba mpya, huku enzi za Magu waliufyata ikawa too much, Yani tumetoka msibani watu waanze kuandamana nchi nzima nchi isingetawalika kabisa, ndio maana akadakwa huyo kiulaini, all in all Kikwete alikuwaga mjanja bana siasa zilikuwaga Raha na ushindani kiasi ccm ilijitahidi kutumikia wananchi
 
Back
Top Bottom