Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,189
- 12,365
Wakina Msukuma hawawez kukubaliNi jambo jema!
Merry Christmas.
Wakina Msukuma hawawez kukubaliNi jambo jema!
Merry Christmas.
Ni likesi la Samia la kubumbabumba sasa wanapanga misamahaUnataka kusema hii kesi in mkono wa Samia na sio ugaidi Kama inavyosemwa?
Rais mstaafu Zuma kaenda jela, je imempunguzia umaskini Mzulu nanm Xhosa?Kenya na Tanzania is like day and night, mambo ya mafisadi au watawala kujifanyia wanavyotaka kama kubambikia watu kesi , wizi wa kuraau kuonea watu Kenya wamemaliza huo upuuzi, muulize Zuma na uraisi wake kaenda jela
UshahidiJitihada za kumaliza kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, zinaendelea “nyuma ya pazia,” ambapo taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amekutana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani.
Haijaweza kufahamika kama jitihada hizo ni za Mnyika binafsi au zina baraka ya chama hicho, ambacho kwenye mitandao ya kijamii kimetanabaisha kuwa hakitaki suluhu yoyote kuhusiana na kesi hiyo.
Taarifa hizo zinaeleza kwamba kimsingi Mama Samia Suluhu aliridhia ombi la kuachiwa kwa Mheshimiwa Mbowe na ilitarajiwa aachiwe kwa “nolle prosequi” (tamko la nia ya kutoendelea na mashtaka) ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) lakini “yaliyojiri kabla, wakati na baada ya mkutano wa vyama vya siasa huko Dodoma” yalipelekea mpango huo kukwama.
Licha ya jitihada hizo za Mnyika, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Masoud Othman nae aliwasilisha maombi ya Chadema kwa Mama Samia, na akashauri Mheshimiwa Mbowe aachiwe bila masharti yoyote.
Uamuzi wa Chadema kususia mkutano huo wa vyama vya siasa huko Dodoma ambao ulifunguliwa na Mama Samia, inatajwa kuwa moja ya sababu zilizopelekea kukwama kwa mpango huo wa kumwachia Mheshimiwa Mbowe.
Taarifa hizi zinakinzana na kauli zinazoongewa na viongozi na wafuasi wa chama hicho kuwa “hawako tayari kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe” kwa sababu wanaamini kuwa hana hatia na mashtaka dhidi yake ni ya kutungwa.
Yawezekana tofauti hizo kati ya “kinachoendelea faraghani” na “kinachoongelewa hadharani” zikawa ni mkakati wa Chadema hasa ikizingatiwa kuwa wafuasi wengi wa chama hicho hawaafiki kabisa wazo la kuomba Mheshimiwa Mbowe aachiwe. Moja ya sababu zinazochangia “msimamo huo mkali” ni shinikizo la “wanaharakati wa mtandaoni” ambao wanapinga vikali siasa za maridhiano kati ya chama tawala CCM na vyama vya upinzani.
Hata hivyo, suala hilo la kesi ya Mbowe “limevamiwa” pia na kundi moja ndani ya CCM linalompinga Mama Samia, na ambalo linaiona kesi hiyo dhidi ya Mheshimiwa Mbowe kuwa yenye manufaa kwa kundi hilo kwa sababu inatoa taswira mbaya kuhusu Mama Samia.
Nihitimishe kwa kutanabaisha kuwa haitokuwa jambo la kushangaza endapo Mheshimiwa Mnyika atakanusha taarifa hizi kwa sababu “zinaweza kumletea tabu” katika chama chake.
Jumanne njema
Merry ndio nini mama?Ni jambo jema!
Merry Christmas.
Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, amekutana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Athumani
Nchi nzima wananchi wameongeza chuki dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Wafe tu. Ikibidi na huyu naye kama analeta ukuda. Unatafuta Magufuli kumisiwa. Hakuna mpenda haki anayem-miss Magufuli. Alikufa na aoze huko aliko. Naona sasa mnapumuawww.jamiiforums.com
We JU.HA hivi unajua DPP anamuwakilisha nani huko kwenye mahakama?Katiba imemruhusu wapi rais anafutaga kesi?
Hao watu wana mamlaka gani kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi kuingikia kesi iliyoko mahakamani? —Hatutaki Mbowe atoke kwa ushawishi na mazungumzo na mtu yeyote, tunataka aachiwe bila masharti, hana kosaKama hili jambo limeingiliwa ili kuleta Suluhu na kulisawazisha, na jambo hilo limeshikiliwa na Viongozi wa Kiislamu, basi litakwisha kwa kheri na utulivu. Hawa ndugu zetu wanajua kutatua matatizo kwa haki na wanaustaarabu wenye utu. Tutegemee mema