Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,242
- 113,627
Siyo mjuzi sana wa habari za idara ya usalama wa taifa, Tanzania.
Lakini katika pitapita zangu humu JF, nimekutana na mada kadhaa zilizonishangaza kidogo.
Mtu akienda dukani akikuta bidhaa ambayo haipendi, lawama anabebeshwa usalama wa taifa.
Msanii Diamond umaarufu wake ukianza kupungua, lawama zinaenda kwa usalama wa taifa!
Timu za mpira za Tanzania zisipofanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, lawama kwa usalama wa taifa!
Ni mimi tu ambaye sielewi dhima nzima ya usalama wa taifa au inakuwaje?
Kwa mfano, usalama wa taifa wanahusikaje na uwepo wa bidhaa za Kenya kwenye maduka ya Tanzania?
Kwa akili zangu hizi za panzi, waamuzi wa mafanikio ya bidhaa ni wateja/ wanunuzi.
Kama wateja/ wanunuzi wanaona bidhaa fulani ni bora kuliko bidhaa ingine, basi wataendelea kuiunga mkono kwa kuinunua.
Na ubora wa bidhaa sidhani kama unahusiana chochote na idara ya usalama wa taifa.
Ubora wa bidhaa unatokana na ubunifu wa mzalishaji. Mzalishaji anapotengeneza bidhaa iliyo bora halafu akaitangaza kwa umma, umma huo ndo utaamua mafanikio ya hiyo bidhaa.
Sasa kama makampuni ya Tanzania hayatengenezi bidhaa zilizo bora kutokana na kushindwa kuwa wabunifu, lawama kwa usalama wa taifa zinahusikaje?
Hmm…..yawezekana ni mimi tu na hizi akili zangu za panzi ndo maana labda sielewi.
Wajuvi na wajuzi wa mambo nijuzeni, tafadhali.